Kwa mara nyingine tena mahakama ya tanzania yaonyesha uhuru wake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mara nyingine tena mahakama ya tanzania yaonyesha uhuru wake.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Mar 9, 2012.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kwa mara nyingine tena mahakama zetu zimezidi kujionyesha wazi jinsi zinavyotumiwa na serikali kama mdoli wake
  kwa kutoa hukumu saa kumi za usiku bila hata ya mshtakiwa kupewa muda wa kutosha kuweza kufika mahakamani.

  kwa wale mliokuwa na chembe chembe za imani na mahakama zetu nafikiri hili linaweza kuwa game changer. mpaka mlango wa wanasiasa kuwazawadia vyeo majaji utakavyofunga msitegemee mahakama huru Tanzania hasa kwa issue zinazouhusu serikali kama ilivyokuwa kwenye swala la mgombea binafsi.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kiutawala mahakama inaruhusiwa kufanya walivyofanya kwa kuzingatia maslahi ya wananchi sio ya serikali wala madaktari. Kama madaktari walikuwa na kesi, chombo hicho hakikuwakataza kufikisha madai hayo kwa sababu ndio kazi yake. Na ukiona mahakama imeingilia na kutoa maamuzi kama haya uje lazima madaktari walikiuka utaratibu, kanuni ama sheria..

  Kinachonishangaza ni kwamba watu wengi humu JF mnaikomalia serikali tu. Je hao madaktari wamepitia hatua zipi za kisheria hadi kufikia maamuzi ya mgomo? Hamjui! - isipokuwa tu Mponda na Nkya lazima wawajibishwe! Why hamjui ila madaktari ni wasomi kuliko watu wote hivyo lazima madai yao ndio yana msingi..
  Mbona Pinda kawakatalia pia yale waloyataka kwa nini yeye pia asijiuzuru? Na sii ajabu hata JK hakubaliani nao hao kina Mponda na Nkya wanawakilisha tu msimamo wa serikali ambao mimi na wewe hatuufahamu zaidi ya kuwa serikali haiwezi kuwasimamisha Mponda na Nkya..
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  maslahi ya wananchi kuwakingia kifua wanasiasa wawili ?? kati ya utitiri ya wanasiasa ambao hatuwaitaji anyway.
  unaposema madaktari walichukua hatua gani za kisheria kabla ya kugoma una maana gani?? waende mbele ya jaji wamuombe awaongezee mishahara au vipi? wamekwenda kwa kumuajiri wao serikali amewatolea nje maombi yao, kinachofuata nini ?? ni ku send message kumuonyesha umuhimu wako kulinganisha na wanasiasa anaowakingia kifua.
   
 4. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jaji mwenyewe ameshindwa hata kipengele kidogo kuwa sheria huwa haifanyi kazi kinyume- the law shall nary apply retrospectively in whatever matter brought before the court. Hata tukiangalia vipengele vinavyoruhusu mahakama kusikiliza shauri upande mmoja au exparte bado kuna utata ukiachia mbali timming ya hukumu husika. Inashangaza ni kwanini jaji alijiruhusu kusikiliza suala ambalo kisheria si kosa. Kugoma katika Tanzania si kosa la jinai. Bwana Rweyemamu kama kweli hataki kudhalilisha taaluma na mahakama, alipaswa kufikiri upya ingawa maji yameishamwagika kwa upande wake. Je Mahakama itajiruhusu kudhalilishwa kutokana na maamuzi ya kisiasa na si kisheria?
   
Loading...