Kwa mara nyingine serikali imenisikitisha sana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mara nyingine serikali imenisikitisha sana!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vakwavwe, Feb 21, 2012.

 1. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Leo nadiriki kusema kusema Serikali ya CCM inadhulumu wananchi, YAmenikuta leo sina hamu na nina hasira mbaya sana.
  Leo majira ya saba nilikuwa nimepark pale TRA manzese kwa lengo la kulipia kodi ya mkataba wa pango.

  Hamadi watu wamenyanyua gari yangu na kwenda nayo maeneo ya Sinza....watu walioshuhudia wakaniambia ni watu wa manispaa. kwa kuwa siwajui nikaona ni vyema nikareport kuibiwa gari pale polisi manzese...cha kushangaza nikaambiwa niwahi sinza mara moja kama vile ni utaratibu wa kawaida. Nikakamata bomba kwenye daladala mpaka sinza nakukuta nasubiriwa kwa hamu kama fisi anayesubiri mzoga....nilipowauliza mbona pale pana nafasi nzuri ya kupark na palijengwa intentionally kuwa daladala zipark ila hazipark tena kutokana na mazingira yale kuwa na bank na ofisi za TRA? nikajbiwa kwa jeuri sana na kutakiwa kulipa faini ya TZS195,000/= nikapata ganzi ya ghafla,195K? nikasisitiziwa kuwa serikali yao ndo imeauthorize malipo hayo!!!!

  kuitoa gari Manzese na kuipeleka Sinza about 5KMs nadaiwa that much???! nikiwa pale amekuja mama mwingine ana mtoto analia na kwamba alikuwa amepark nje ya hospitali wakanyanyua gari yake na wanamtaka alipe faini hiyo!!Unyang'anyi huu unaofanywa na serikali utawarudi vibaya sana tena ni soon...maana baadaye wamekuja watu kadhaa ambao wamekuwa wanafukuzia magari yao kwa nyuma na kuwasihi wabebaji wawaachie lakini hawakufanikiwa....hasira tulizokuwa nazo hazina mfano! ndiyo maana nasema UNYANG'ANYI HUU UNA MWISHO NA MWISHO WAKE UKO KARIBU SANA.

  195K ni seheme kubwa sana ya mapato yangu ya mwezi, na nimejiridhisha kuwa walionipora pesa hizi wametumwa na serikali, kwa leo nanyamaza ila kunyamaza kwangu siyo BURE...nimewalipa kwa kuwa gari ni ya kampuni na nilitoka lunchtime mara moja kwenda kulipa kodi ila mapambano yanaendelea.
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  lakini mkuu umevunja sheria au la?
   
 3. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa moshi nikitu chakawaida that is why we are the cleanest town in this country.

  minaona watanzania tujifunze utaratibu wakupenda miji yetu and this is a good to make our towns clean. so pole bro lakini jifunze kuheshimu parking kaswababu nchi kama Poland ungelipa mara 70 yake iyo.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Issue ni kuwa ata izo parking hazitoshi!
  Alafu unakuta hakuna ata sign post yoyote inayosema hakuna parking apa!
  Ivi mkimsubiri mwenye gari na kumpa onyo na kumwambia aondoe gari mnapungukiwa na nini.
  Kama ni kukusanya mapato mngeenda Barrick Gold au hawa wanaobadilisha majina ya mahotel kila leo.
  Walishawai kulikamata langu ila hawakuliburuta niliwatoa kimtindo wakasepa
   
 5. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi nafuata sana sheria na ninaziheshimu....nasikitika sana ninapoviziwa. pale kuna bank na ofisi za TRA na hiyo ndiyo parking pekee ukiacha service road ya kupark magari mawili au matatu hivi....nimeambiwa hao jamaa zako wanajificha mahali ili upark, ukifunga mlango tu wamefika hata kama unawaona wanakukatalia,hata utoe machozi ya damu lazima wanyanyue gari na wanazinyanyua vibaya sana na wanazidamage board. wangekuwa wanafuata haki wangeweka bango ili watu wasipark,tatizo ni kwamba kwao hiyo ni kitega uchumi ndo maana hawaweki bango na hawawezi kumuelimisha mtu.

  Tujaribu kuwa realistic hata kwenye adhabu zenyewe, kukokota gari na migari yao mibovu ile kunacost that much in less than 15Min????
   
 6. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Wakuu japo halijanikuta lakini ningependa kupata ushauri wa kitaalamu ili niweze kujua haki yangu pale kinapotokea.

  Parking sehemu yeyote nilipowahi kupita ikiwapo ULAYA inaongozwa na sheria za barabarani. Na hivyo inaeleza wazi kama
  kuna parking au la na sehemu ingine inaonyesha muda unaoruhusiwa kupaki.

  Vile vile uzoefu unaonyesha kwamba sehemu za parking lazima zichorwe ili kumsaidia mtu anayepark gari. Na sehemu zote ambazo haziruhusiwi kupaki gari ndio kunawekwa ONYO:

  Sasa basi napenda kufahamu je hao waliopewa hayo mamlaka ya kufuatilia gari zilizopaki sehemu ambazo hawaruhusiwi wanazingatia hilo.

  Pili kampuni hiyo imepewa hiyo kazi na mamlaka gani na wanandesha shuguli hiyo kwa kutumia sheria gani?

  Mwisho ikitoke mimi nimejirizisha kwamba sijavunja sheria (AMBAYO NDIO CONCERN YANGU) ninaanzia wapi kufuatilia
  haki yangu niliyoporwa?

  Nawakilisha
   
 7. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo manzese kulikua na bango linaloonesha NO PARKING?
   
 8. L

  LISAH Senior Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana bro wanakera sana hawa watu.
  Si dhani kama serikali ndiyo inapanga hiyo bei ni uroho wa hawa tuliowapa madara ni vibiashara vyao binafsi sasa mdhibiti wa bei hayupo wanajipangia tu. Kwa petrol gani sana sana wangekupa adhabu hata ya 30 thou. mh 195, mshahara wa mwezi huo!

  Na nikweli kabisa vibao hakuna ni mitego tu!
   
 9. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  halipo mkuu, lingekuwepo nisingepark...na hao jamaa wanaleta jeuri kuwa mbona nimepark wakati hakuna bango linaloniruhusu kupark?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Si huwa mnaiita Serikali "legelege" usahihi ni (regerege), sasa leo imekuwaje tena? unavunja sheria usipochukuliwa hatua unalalamika, ukichukuliwa hatua serikali mbaya! unanshangaza! - courtesy FF.

  Kuwa ukikuwa utaacha. Nakuuliza swali, utaenda kupaki tena hapo?
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  na bado.....
  ndo maana kibajaji changu nikikipaki ofisini trip za mjini nakwea daladala
  hadi hapo itakapoeleweka wapi ni parking wapi sio...
  maana huu utaratibu wa kupora hela za walalahoi kinguvu si mzuri....
   
 12. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumeshalingoa bango kwa ajili ya kuuza "Chuma Chakavu"

  "HAYA NDIYO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 13. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni serkali za mitaa, i mean manispaa ya kinondoni ndio wanaopitisha huo ******.
  katika hizo pesa wao wanapata 50,000/ kwa mujibu wa breakdown waliyoibandika pale ofisini kwao.
  unavyomnyang'anya mtu pesa nyingi hivyo unategemea aishi vipi? watu wakikata tamaa hapatakalika hapa nasema ukweli jamani!!!!nilikuwa naenda kulipa kodi na biashara ninayotaka kufungua inaweza kuniingizia faida ya kama 150,000 kwa mwezi halafu wao wamekula 195,000 already. inauma sana na inaumiza pia
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  fungueni kesi mahakamni kupinga sheria hiyo dhalimu
  mahakama ikishatamka ni batili mtakuwa huru
  tafuteni mawakili wafungue shauri kupinga legality ya hao wahuni madalali na manispaa
   
 15. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi sitapark tena kwa kuwa najua kuna wakabaji pale ila wewe ambaye hujui unaweza ukapark kama una gari lakini....kama wanafikiri huko ndo watapatia sifa ya kuwa serikali makini wamepotea sana. ulegevu tunao usema ni comments za mawaziri kuwa polisi ni majambazi na serikali haikanushi...na sasa ndo nimeamini serikali yenyewe ni majambazi sio polisi tu peke yao.
   
 16. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,634
  Trophy Points: 280
  Haya yametokea kariakoo juzi,
  Mkanda ulikuwa hivi, jamaa wa parking walipiga gari pingu wakati mwenyegari yupo ndani, kushutuka, akaotoka nje kwamba wafungue gari yake, wale watu wakakataa, jamaa kaingia ndani ya gari kakoki bastola akawaamulu kufungua bila mafanikio ndipo alipoamua kufyatua lisasi mbili hewani, mgambo, polisi wote wakaanza kutimua mbio kali, si unajua pale kariakoo wingi wa watu, watu kuona mgambo polisi wanakimbia wakazani majambazi, basi nao wakaanza mbio kali, maduka yakafungwa kwa nguvu wakizani ni majambazi watu wengi wameumia vibaya kwa kukanyagana wengine wamepasuka na kushonwa nyuzi tatu, maduka ya vioo yamevunjika na makomputer kuaribika, si unajua vijana pale nje wanatengeneza simu na kuingiza nyimbo. Hadi vibaka hawakuchukua kitu, wengine walizani magorofa yanaanguka hivyo walikimbia kutoka kwenye raound about mpaka TBL
   
 17. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Je usingelipa hyo 195k wangefanyaje gari lako? Wangelipiga mnada?
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mkuu, tafuta mwanasheria upambane nao. Kulalamika tu hakutoshi na watendelea kufanya hayo hayo kwako na kwa wengine pia. Mabadiliko huanzia kwa na mtu mmoja mmoja.
   
 19. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwanza Vakavwe pole sana na yaliyokukuta.

  Chali wa Moshi, si kweli kuwa faini za Poland ni mara 70 ya hizo. Chinga (Msumbiji) wetu hapa Warsaw walimvutia gari lake na akalipa 550PLN ambazo kwa haraka haraka ni kama Tsh laki tatu. Ila gari likilala kila siku wana charge kwa kulala.

  Tukija kwenye sehemu ya kupark, ni lazima pawe na kibao na kama hakuna kibao, basi kama una muda na nafasi, nenda na Mwana sheria, na muangalie pande zote kama kuna alama yoyote ya usipark. Si lazima waandike kibao cha usipark hapa ila kuna zile Road Sign ambazo zinaonyesha usipark kuanzia hapa hadi hapa. Inawezekana hizo zipo sehemu fulani nyuma na ndizo wanatumia.

  Kama hakuna, basi nendeni muwashitaki mahakamani kwani na wao wana makosa. Kama hizo alama zipo, basi Laki mbili kama faini ni kitu cha kawaida sana duniani.
  Nchi zenye faini kubwa na za kutisha ukizidisha Speed ni hizi hapa chini. Mara nyingi hata kosa la kupark vibaya wanalichukulia kama ndiyo kosa kubwa na faini yake inakuwa ni ile ya mwisho.

  Soma hapa: The World's Highest Speeding Fines

   
 20. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  pole mkuu!
   
Loading...