Kwa maoni yangu "kuapisha pekee ndio kazi aipendayo"

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Utasikia kaapisha makatibu wa wizara, baraza jipya la mawaziri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, majaji wanawake..... Mbona sisikii alieiba hela za serikali akajulikana na hata kuzirudisha TIB kashitakiwa kwa kosa la KUHUJUMU UCHUMI?

Naomba mwongozo kwa wanasheria, Nyerere na Sokoine walikua wanatumia sheria gani kuwatia mbaroni na hata wengine kuikimbia Tanzania hadi mauti ilipomkuta Nyerere kama Mkono?. Wako wapi viongozi wenye kuMfanya MTanzania kua mzalendo kwa nchi yake kwa kua anaongozwa na Mzalendo?

Sasa hapa nikimuita JK dhaifu ntafungiwa JF?

Hapa kuna shaka katiba ijayo ikamruhusu raisi kama JK kuapisha hadi wajumbe wa nyumba kumi, madiwani, mwenyekiti wa mtaa na hata kila harusi raisi awe mgeni mwalikwa.
 
ha ha ha leo thread zitaanzishwa mpaka basi hivi Naibu Spika hakujua amefanya udhaifu wa Kikwete ujulikane na wengi sasa
 
Back
Top Bottom