Kwa Manufaa ya Nchi Serikali ilipe deni na Kununua machine za Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Manufaa ya Nchi Serikali ilipe deni na Kununua machine za Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Feb 26, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,111
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Watanzania kama kweli tunaipenda nchi yetu tuache siasa na tujali nchi. Serikali inatakiwa kufanya yafuatayo

  1. Kama Dowans walitoa huduma kweli za umeme pale ubungu basi walipwe pesa ya huduma tu. Hii siyo pesa ya kesi bali ni ya huduma iliyotolewa na thamani ya huduma ni ya kitaifa kama ilivyokubaliwa mwanzoni mwa huduma. Serikali isilipe pesa zaidi ya pesa za huduma iliyotolewa.
  2. Serikali inunue mitambo kama ni bei ya kihalali ya hivyo vifaa vya Dowans. Watafute wataalamu wa kuhakiki thamani ya vifaa na wanunue kutoka kwa Dowans. Hii inaweza kufanya kwa kuangalia bei ya vifaa kama vya Dowans inavyoenda kwenye soko. Hii inamaana kama vifaa kama hivyo vinauzwa $50M na Dowans wakasema $45 basi tunajua tuna deal nzuri.

  Hii itasaidia kuepusha gharama za usafiri wa vifaa vingene kuja Tanzania. Vilevile hivi vifaa vitakuwa vya Tanesco hivyo kuweka uhakiki wa umeme. Vilevile gharama za uendeshaji wa machine za Dowans ni ndogo kwasababu zinatumia Gas na zile za IPL zinatumia mafuta!. Gharama ni kama nusu.

  Tanzania imesainishwa mikataba mibaya ya rushwa lakini sasa tuko kwenye shimo na tujaribu kutoka kwenye hili shimo kwanza bila kuumia njiani. Tuache politics za kila siku na tutafute ufumbuzi wa janga la umeme. Pamoja na kuwa mkataba wa hii kampuni una ulakini hii ni step nzuri Tanzania inaweza kufanya. Uamuzi mwingine wowote wakati huu utakuwa mbaya.
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lipa na pesa yako pamoja na Kikwete, Pinda, Makamba na familia ya Rostam. Fanya petitions itawasaidia. Unaonekana aufahamu lolote kuhusu swala la Downs Tanzania ni kupoteza muda na wewe, labda ulikuwa Alaska umerudi leo.
   
 3. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 510
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kwanini mitambo ya do ones tu? Tanesco ni wazembe, tangu issue ya Dowans ilipoanza wangefanya mchakato wa kununua mitambo mipya ingeshafika. Mgao wa umeme siyo emergency kwe Tanzania. Upo tangu 1993. Miaka yote hiyo Tanesco wanafanya nini? Poor planning on there side is not necessarily an emergency on our side. Uzembe tu.

  Matatizo ya mgao wa umeme wa kulaumiwa ni Tanesco. Wanasiasa mnawaonea tu. After all wanafanya vizuri sana kazi yao ya siasa=UONGO
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mi nilidhani utaanza na kushauri serikali iwalipe wakandarasi wa ujenzi wanaoidai mabilioni ya shilingi huku miradi ya ujenzi ikiwa inasuasua. Then ishauri iwalipe wazee wa Afrika mashariki ambao mahakama imeamuru walipwe lakini serikali hailipi. Deni la Dowans kama ni halali liwe la mwisho kulipwa kama kweli na halali kwa mujibu wa upeo wako mdogo.
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi wewe unafikiri matatizo ya umeme nchi hii yataisha kwa kununua mitambo ya Dowans?? PLEASE!!!
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata wakinunua dowans kumi, hulka chafu!
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,111
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Mimi nashangazwa na mawazo ya ndugu zangu wengine. Sasa hivi tunavyoongea serikali inatumia pesa nyingi kuwalipa IPTL bei ya mafuta kuendeleza mitambo yao. Mitambo ya IPTL ya mafuta ni ya zamani na inatumia pesa nyingi kwasababu si ya Gas kama ya Dowans hivyo jazba hazitatui tatizo lolote!. Pesa tutatumia tu kwani sasa anayefaidika ni IPTL na serikali ikila hasara kwenye uwekezaji na mzunguko wa pesa!. IPTL yenyewe ni mkataba mbovo lakini tunawapa pesa nyingi za wananchi kuendeleza mitambo ya mafuta yanayotoka nje wakati tuna gas yetu pale ubungo!. Bado nafikiri wazo langu ni la msingi.
   
 8. M

  Mwamatandala Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwanza inaonekana una speculate tu wewe.je unajua mitambo ya dowans inatumia nishati gani?.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Walitoa huduma kwa mkataba gani?

  Tayari serikali imeshalipa Dowans mara tatu ya gharama za mitambo hiyo. Tukiwalipa na hizi bilioni 94 tutwakua tumelipia zaidi ya mara nne ya gharama za mitambo, na tukinunua tutakuwa tumelipa karibu mara sita ya mitambo hiyo hiyo! Ndicho unachotaka? Kwanini usishauri tununue tu mitambo mipya kabisa toka kwa Watengenezaji na tumuache Al Adawi na Rostam wahamishe mitambo yao Oman?
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  WEZI WA KUKU....SIMU...BATA....TWAWAUA, KWANI WAKIENDA MAHAKAMANI HUACHIWA ......ILA WIZI MKUBWA UNALINDWA NA WAKUBWA ILI PUBLIC ISICHUKUE SHERIA MKONONI ....ETI MPAKA MAHAKAMA ITHIBITISHE.....ISIPOTHIBITISHA(kama mara zote inavyokuwaga) wanaachiwa kwani hawana hatia ya kujibu....!
  THE LAW IS BLIND TO BIG GUNS.....BUT THE LAW IS MSUMENO TO VIDAGAAZ
   
 11. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Napata kisirani kua pamoja na makelele yote haya kuna watu mmeweka pamba masikioni...Unataka DOWANS ilipwe mara ngapi?
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,591
  Likes Received: 18,576
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, suala la dowans ni mbio za sakafuni, tumeshasokomezewa ukingoni na kulazika kumkubali baniani m-baya kwa sababu kiatu chake dawa!.
  Kwa hali ya umeme ulivyo sana,we have no choice bali kukimeza kidonge kichungu cha dowans ili angalau tuweze kurudisha pumzi ndipo fikra za suluhisho la kudumu litafutwe.
  Kule nyuma niliwahi sema kwenye issue ya dowans, RA was just a front. Kikulacho ki nguoni mwetu!. Kuna siku itafika, miti itazunguza!.
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,438
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Controversial kanjanja Pasco umeshikia bango mitambo ya Dowans weeee........ Project mliyopewa mkiifanisha mtalipwa kiasi gani? Nyie ma-kanjanja mwapenda mno fedha za bure yakhe..... ndio maana mnatumia mpaka pingu kudai fedha.
   
Loading...