Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
KWA MANTIKI YA KISHERIA DC KIHONGOSI AMEKOSEA, LAKINI KWA MANTIKI YA WAJIBIKAJI YUKO SAHIHI
Na Elius Ndabila
0768239284
Jana na leo kuna mjadala mkubwa juu ya uhalali wa Mh DC wa Arusha Mh Kihongosi kuwatandika fimbo watu wanaotajwa kuwa ni wafanyabishara kwa kosa la kuiba viti vya shule.
Staki kuingia kwenye hoja ya uwizi, hii ni kwa kuwa tukianza kujadili hili tutaingia kwenye mambo mengine ya kisheria ambayo si wajibu wangu leo kuyazungumzia. Mimi nataka tuzungumze facts in issue iliyopelekea wao kuchapwa. Tujikite kuangalia makosa na usahihi wa hizi fimbo kwa mkutadha wa kinadharia ili kujenga Taifa.
Unapokuwa kiongozi unakuwa na malengo yako, hasa unapofanya kazi. Unatamani kama ni shamba ulime kwa wiki moja. Unapokuta mtu mliyekubaliana naye kuwa alime kwa wiki moja kuna siku hajaenda shambani na yupo kilabuni bila shaka utavunja mkataba naye kwa kuwa utakwazwa na kitendo cha kunywa pombe badala ya kwenda Shambani. Ijapo pengine ungemsikiliza huenda angekuwa na hoja.
Unapokuja kwenye issue ya Kihongosi kuwachapa fimbo, yule ni DC na amepewa kazi pia ya kuhakikisha shule zinakuwa na madawati. Unapotengeneza Dawati then unasikia kuna watu wameziiba na kuharibu lazima kama DC utachukua hatua kali kabla ya mamlaka zingine kwa kuwa ni ready heanded. Umewachapa viboko kwa kuwa yeye ni kiongozi na halali usingizi kwa sababu ya kazi hizi. Lakini hata Mh Rais alisema bora kufanya kosa kwenye kuwajibika, kuliko kuto fanya maamuzi. Kihongosi amefanya uamuzi yanayoonyesha alikerwa na jambo hili.
Kuchapa viboko watuhumiwa bila kuwafikisha kwenye vyombo vyenye maamlaka hiyo ni kosa, lakini kufanya kosa ambalo lina maslahi mapana ya Taifa ni jambo la kupongezwa na linaonyesha namna serikali ilivyo serious na watovu wa nidhamu.
Sasa tukubaliane kuwa kuiba ni kosa kwa mjibu wa sheria ya nchi lakini hata kuchapa bila kuzingatia sheria ni kosa. Lakini kuchapa fimbo kwa kupeleka ujumbe kwa wezi wengine ni jambo la baraka. Kwa mstari huu ninaungana na Kihongosi kwa watu wanaosadikiwa ni wezi. Ninaungana na Kihongosi kwa mkutadha wa Uwajibikaji na si kwa mkutadha wa Kisheria.