Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Akihutubia mkutano mkuu wa CHadema hivi karibuni Mbowe alisikika akisema kwamba nchi yetu yote ya Tanzania ilishamwagiwa mafuta ya petroli na yeye ndiye mwenye kibiriti.
Na kwamba uvumilifu utakapomwishia atawasha hicho kiberiti kwenye mafuta hayo kitakachotokea wasimutafute!
Kwa maneno haya makali na ya vitisho ina maana kwamba huyu mtu bado tu hajatambua kwamba:
1. Watanzania ni watu tofauti sana na ambavyo huwa anawafikiria. Wamekomazwa sana kisiasa kuanzia baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kichama kimoja cha ki-saccos cha kisiasa kamwe hakiwezi kuwaparanganisha.
Hivi ni mara ngapi Mbowe amekuwa akijaribu kuhamasisha na kuratibu maandamano ya machafuko nchi nzima (yenye majina tofauti tofauti) na mara zote kugonga mwamba?
Hajatambua tu kwamba Watanzania wameshazichoka hizo hamasa zake (= kuwasha kiberiti)?
2. Hivi Mbowe hajatambua tu hadi sasa kuwa hii awamu ya tano ni tofauti kabisa na zile alizozoea kuzitisha tisha?
Kwamba hii awamu haitishwi na mtu au kikundi cha watu chochote. Ni awamu ambayo haitaki ujinga jinga (nonsenses)!
3. Hivi hajatambua tu kwamba awamu hii ya tano imedhamiria kwa dhati kunyoosha mambo mbalimbali nchini ambayo yalikuwa yamekaa sivyo yakiwemo hayo ya kwake ya kisiasa? Inahakikisha kila mtu anafuata sheria za nchi tulizojiwekea.
4. Hivi bado tu hajatambua... (endeleza na wewe).