Kwa mambo yanavyoenda kuna ulazima mkubwa wa kuwa na wagombea binafsi

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,630
2,000
Kwa mambo yanavyoenda na siasa zetu zinavyoenda naona tunahitaji sana kuwa na wagombea binafsi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Rais.

Vyama vya siasa vimekuwa ni njia ya watu kutafuta vyeo kwa njia yoyote ile, lengo ni vyeo na si kwamba wanaamini katika sera za vyama vyao. Chama cha siasa ni kundi la watu wenye mawazo yanayofanana ya namna ya kuendesha nchi, haiko hivyo tena, ni kundi la watu wanaotafuta vyeo tu.

Kama kila mtu ana haki ya
kuchaguliwa, iweje alazimishwe kuwa member wa chama fulani cha siasa ndiyo apate hiyo haki? Hii haijakaa sawa.

Pia mtu aliyedhaminiwa na chama kugombea basi lazima ataweka maslahi ya chama kwanza. Lazima afikiri kulingana na chama maana ndiyo kimeshika cheo chake. Kama ni mbunge au diwani basi anawakilisha maslahi ya chama kwanza na baadaye wananchi. Tupate wagombea binafsi ambao maslahi ya wananchi ndiyo yatakuwa kipaumbele.

Tupate tume huru na turuhusu mgombea binafsi. Si kila anayetaka kugombea awe kwenye hivi vyama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom