Elections 2010 Kwa mambo haya uchaguzi hautakuwa "free and fair"

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Nikiangalia mambo haya napata wasiwasi kama uchaguzi utakuwa free and fair kwa tafsiri yoyote kwani chama tawala:-
1. Kinatisha wapiga kura kwa kutumia wanajeshi
2. Kimeshatangaza matokeo ya kura na nec hawajawakoromea maana yake wamekubaliana nayo
3. Kutumia vyombo vya umma kujinadi, huku vyama vingine vingipewa negative coverage
4. Mgombea wao wa urais kuvunja sheria za uchaguzi kwa kila siku kuhutubia zaidi ya muda unaoruhusiwa
5. Kutumia magari na rasilimali nyingine za serikali kufanya kampeni
6. Kutumia bajeti kubwa ya uchaguzi kuliko iliyokubaliwa na vyama na tume ya uchaguzi huku tendwa akiangalia
7. Kutoa rushwa waziwazi na takukuru wakiangalia
ningeshauri vyama vingine vilalamikie hali hii
 
Mkuu umeshaona kila jitihada za malalamiko zinavyotupiwa kapuni na watendaji wa serikali (NEC na Tume ya Msajili wa vyama vya siasa). Njia moja kati ya nyingi zilizopo ni kuendelea kuwafahamisha wananchi juu ya ukweli, na ukweli wenyewe ni kuhakikisha viongozi wababaishaji wanawekwa kando. Nchi iongozwe na viongozi wenye maono na moyo wa kuthubutu. Itakuwaje Tanzania bila JK???
 
Tanzania yenye upendo inawezekana pale tu ambapo kutakuwa na hali sawa katika kugawana keki ya taifa bila upendeleo na ubinafsi katika vipaumbele vya taifa.
 
Back
Top Bottom