Kwa makusudi kabisa serikali imewapuuza vijana

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Vijana ni taifa la leo ila sio Tanzania, serikali ya Tanzania makusudi kabisa imeamua kuwapuuza vijana, serikali imeshindwa kuwaendeleza vijana wake na kuacha vijana hawa wakimezwa na mitaa, tumekuwa na vijana ambao wanahitimu shule za msingi ambao wanashindwa kuendelea na masomo ya sekondari lakini hakuna utaratibu maalumu unaoandaliwa kwa ajili ya vijana hawa hata kuweza kupewa elimu ya ufundi wanaachwa tu mtaani, wapo vijana wanaohitimu elimu ya sekondari kwa sababu ya ubovu wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia vijana hawa nao hufeli lakini serikali haiandai programu maalumu kwa ajili ya kuwasaidia vijana hawa wanaachwa.

Wapo vijana wamekosa mikopo vyuo vikuu ndoto zao zimezimwa wengi ni wale waliopitia mafunzo ya Jkt nao wanaachwa tu mtaani, hivi vijana hawa ambao wamefunzwa mbinu za medani na matumizi ya silaha wakiwa majambazi tutamlaumu nani? Kwanini vijana hawa wasitafutiwe njia nzuri ya kuendelezwa kama njia ya kuwapatia mikopo imeshindikana.

Wapo vijana maelfu wanahitimu vyuo mbalimbali wanahitimu vyuo mbalimbali hawa nao wanarudi mtaani bila shughuli zozote, lakini serikali haihusiki nao wanaachwa tu, hivi kwanini serikali haitengenezi mazingira mazuri kwa vijana hawa ikiwemo kuwapatia msaada na mafunzo ili waweze kujiajiri, haingii akilini unampatia mtu mkopo wa milioni kumi kusoma halafu mtu huyo akimaliza anarudi mtaani kukaa bila ajira.

Baadala ya kuwapa mikopo ya kwenda vyuo vikuu vijana hao wangelipewa mikopo ya kibiashara na hata wengine kupewa mikopo kwa ajili ya kilimo wakiwa chini ya uangalizi wa maafisa biashara na afsa kilimo, lakini vilevile serikali ingejenga vyuo vya ufundi stadi kwa kila kata kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana hasa mafunzo ya ufundi stadi ili vijana wengi waweze kujiajiri.

Lakini suala la muhimu ni kuvutia wawekezaji hasa wa Viwanda kwa ajili ya kujenga viwanda nchini ili vijana wengi waweze kuajiriwa (sera ambayo serikali imeshindwa kuitekeleza), matokeo ya kushindwa kuwaendeleza vijana tutatengeneza mateja wengi, vibaka wengi, majambazi lakini yale yatatokea Nigeria na Somalia yanaweza kuja kutokea huku kwetu.
Tukumbuke vijana ni taifa la leo tusiwapuuze, kuwapuuza vijana ni kulipuuza taifa.
 
Serikali kipaumbele chake ni viwanda na ununuz wa ndege, kazi ya jufkr kuwasaidia vjana kwa kuwaajiri na kuwapa mafunzo naona wanaona watamaliza hela za ununuz wa ndege,

Hakna anaesikilza hili, wizara ya utumishi haitak kupunguza wahitimu kwa kuwaajiri ina kazi 1 tu ya UHAKIKI mwaka mzima, hakika mioyo ya vjana ikifunuliwa ilivyojaza chuki na serikali ni hatari, naamn wakiingia boko haramu ktafta jeshi 90% vijana watajiunga maana hawaoni matumaini!

Vjana wengi sasa wawaza negatively, mabinti miili yao waigeuza kitega uchumi, kiume sasa kaz kubeti hii ndo Tanzania!

Wimbo wao wa kampeni 2015 unasadifu waliyoyasema! Acha namba isomeke! Hii sio Tanzania Bali ni Tanzagiza!
 
Sizonje a.k.a Baba Fulani kalewa madaraka. Yeye kusaidia vijana ni kuwa acha Machinga wauze vitu Barabarani.
 
Tatizo lipo kwenye mfumo wa elimu tunaoufuata... Tunaona vijana wengi wanahangika hata baada ya kupitia shule ni kwa sababu elimu tunayoifuata inakuelekeaza uwe mtu fulani au ufuate mfumo fulani, haikupi mwanya wa kufikiria nje ya box...


Ukisoma vyuo vya nje au kupata elimu ya nje... Utakutana na kozi zingine ambazo huku hujawahi kuzisikia lakini kwao zinaajira kibao... lakini huwezi kuzisoma kwa sababu hatupo kwenye mfumo huo...

Tuna safari ndefu sana...
 
Hapa ndo naona ni aina gani ya vijana tunao hapa nchini. Sasa kama mmepuuzwa mmeshafanya kipi ili kudai haki yenu zaidi ya kulalama tu nyuma ya keyboard. Siku mtakapojielewa na kuacha kulialia na kujipendekeza ndipo mtaanza kuthaminiwa.
 
Hapa ndo naona ni aina gani ya vijana tunao hapa nchini. Sasa kama mmepuuzwa mmeshafanya kipi ili kudai haki yenu zaidi ya kulalama tu nyuma ya keyboard. Siku mtakapojielewa na kuacha kulialia na kujipendekeza ndipo mtaanza kuthaminiwa.
Utafanya nn ukiwa una hisi njaa 24/7, vijana wasio hisi njaa ndio kina Mwigulu Nchemba, Paul Makonda na Anthony Mtaka ambao ndio kwanza ukidai haki yako watakuja na askari na silaha nzito.
Wakati huo ninyi mwenye njaa mna bango "tunaomba serikali itukumbuke sisi wahitimu" wao wana amrisha askari kutupa mabomu.
 
Hivi mbowe kuwafukuza kina Mwambigija na kuwaleta akina Lowassa,Kingunge,Sumaye ndio sera ya vijana chadema,Kuwateka kina saanane?
 
Back
Top Bottom