Kwa makato haya ya Bodi ya Mikopo kwenye mishahara, Magufuli na Serikali yako mmetukosea watanzania!

Makato haya yanahitaji kuwa revisited. Hata hii sheria iliyopitishwa inayohusu mikopo hii ya elimu ya juu ina mapungufu mengi sana ambayo yote yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

Watu wengi wanakatwa hela nyingi sana kiasi kwamba inaonekana kama hii mikopo imekuwa ya biashara na sio ya elimu. Ni kama waliopata hii mikopo wamezalisha hela nyingi sana wakati wengi wana ajira zinazowawezesha kujikimu tu maisha yao ya kila siku huku wakisongwa na majukumu mengi ya familia za kitanzania zilizo very extended families.

Kuna wakati ukitafakari sana unaona kama ni wachache wamelimbikizwa malipo ya wengi ambao kwa sasa hawana ajira na hawajaanza kurudisha hii mikopo. Serikali haina hela au maamuzi yameshafanyika?

Naamini serikali sikivu inaweza kusikiliza kilio hiki cha watanzania wengi na kukifanyia kazi.
 
Makato ya bodi ya mikopo elimu ya juu umepandisha, malimbikizo ya mshahara hujatulipa.

Msemakweli mpenzi wa Mungu nakuchukia sana
We nae...kasema ivi mchague kwanza ili akurekebishie mshahara wako!!
 
Yaaani huu mkopo ni shida. Nilipewa mkopo jumla 8m miaka 5 baadae nimeanza kulipa umefika 15m. Hapo ni kwenye slary slip. Nilipoenda bodi kupata barua nikakutana na deni la laki 7. Nikafurahi mwenyewe...nadhani tunawalipia na wale ambao hawapo kwenye ajira rasmi.
 
Makato haya yanahitaji kuwa revisited. Hata hii sheria iliyopitishwa inayohusu mikopo hii ya elimu ya juu ina mapungufu mengi sana ambayo yote yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

Watu wengi wanakatwa hela nyingi sana kiasi kwamba inaonekana kama hii mikopo imekuwa ya biashara na sio ya elimu. Ni kama waliopata hii mikopo wamezalisha hela nyingi sana wakati wengi wana ajira zinazowawezesha kujikimu tu maisha yao ya kila siku huku wakisongwa na majukumu mengi ya familia za kitanzania zilizo very extended families.

Kuna wakati ukitafakari sana unaona kama ni wachache wamelimbikizwa malipo ya wengi ambao kwa sasa hawana ajira na hawajaanza kurudisha hii mikopo. Serikali haina hela au maamuzi yameshafanyika?

Naamini serikali sikivu inaweza kusikiliza kilio hiki cha watanzania wengi na kukifanyia kazi.
Hii serikali sikivu kwa lipi?Waelezeni ukweli hata kama ni mchungu pasipo kuwapa sifa za uongo vinginevyo haya mambo hayataisha.
 
Hivi hili deni nitakuja kulimaliza? Nilihitimu 2017 likiwa 12 M. Nimeomba statement mwaka huu baada ya kujiajiri ili nianze kulipa nikakuta limefikia 16M.
 
Kwenye kupewa mliweka na sherehe familia nzima, linapokuja swala la kulipa mnaweka matanga tena??
Lipa deni, Ebo!!
 
Back
Top Bottom