GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,073
- 107,565
Hakuna tabia naichukia kama hii ya Madereva Bodaboda kila wakikuona tu wanakupigia Honi ya kutaka Kukufuata na wakupeleke utakako hata kama huna Safari yoyote ile.
Hivi inaingia Akilini kweli Madereva Bodaboda wanakuona kabisa umefungua Geti huku ukiwa umeshika zako mfagio na mkasi unafanya Usafi nje wa Fensi yako tena Umevalia Kinyumbani ( Kikawaida na Sometimes hata na Suruali yako Chafu au iliyotatuka ) halafu Wanakuja kama Saba hivi na Pikipiki zao na Kukupigia Misele huku wakikutimulia Vumbi na Kukuuliza kama unaenda Mjini?
Kwa majibu ( Kauli ) ambazo huwa ninawapa kutokana na Kero yao hi ambayo inanikera nina uhakika tayari Mwenyezi Mungu ameshaniandalia Kuni zangu ambazo si tu za Kunichoma bali za 'Kunibanika' kabisa Siku akiniita Kwake Mbinguni.
Je, Wenzangu JF huwa mnawajibu vipi?