Kwa majibu haya ya Waziri Mkuu leo sidhani kama kutakuwa na ongezeko la Mishahara Novemba

jayec

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
599
477
Ni dhahiri hakutakuwa na nyongeza ya mshahara mwezi huu wa NOVEMBA/2017,hii ni kulingana na majibu ya Mh. Wazir Mkuu leo bungeni akijibu swali la Mbunge wa Kilindi lililotaka jibu la serikali kuhusu nyongeza ya mshahara kwa watumishi.Kwa kweli watushi muendelee kufunga mikanda.

Fungua link hii kwa taarifa zaid.Hakikisha unamsikikiza mpaka mwisho
 
Hakuna kitu, wawe wanasema ukweli tu hatupandishi basi hizi siasa sio vizuri, kama watanzania wangepewa roho kama yangu hawa wanasiasa na siasa zao zingefikia mwisho, kura sitoi kwa mambo yao
 
aibu hii ccm mnatuangusha
Wanawakwanza sana watumishi kwa matamshi yao yanayokanganya,yule mkubwa alisema hiv,siku chache zilizopita mwingine alisema vile,na mara na huyu kasema haya
 
Yani kila siku ni kuhakikiki,,kuhakikii madeni,,malipo hamna!!Ivi kuhakiki gani kusikoisha?aah tushawazoea!!Ccm ndio zenu kenge nyie!
 
porojo nyingi awamu hii. Hata pale kiongozi mkuu na msemaji wake mkuu Hassan Abasi walipo jidai kuwa wamelipa kwenye mifuko ya jamii madai yote ya wastaafu hii si kweli. Walicho lipa ni deni la serikali waliloikopa mifuko hiyo wakati wa kampeni mwaka ,2015. Madeni ya madai ya wastaafu hayaja lipwa kabisa. Afisa mwandamizi upokeaji micchango wa PPF aliwathibitishia wastaafu ATCL kuwa hakuna pesa iliyopokelewa toka serikalini wala ATCL kwa ajili ya kuwalipa madai yao hata baada ya uhakiki kufanyika ATCL na PPF na hata baada ya kikao kati ya serikali.ATCL. na PPF na serikali kuahidi kulipa. Serikali iseme ukweli kwa wananchi na siyo kutafuta kiki. Wastaafu wanao umia wana watu wengi wanaowategemea wapeni haki zao. Mbona wallipo kuwa kazini mliwaheshimu na kuwabembeleza kuchangia hiyo mifuko na walifanya hivyo bila hiyana leo wananyanyasika. Kumbukeni nanyi ni wastaafu watarajiwa ipo sehemu mtakuja sumbuliwa.
 
Utumishi wa Umma ni kaa la moto, tuliopo tunatamani toka, walio nje wanatamani ingia. Ahadi na matamko kibao, Waziri mkubwa amekataza matamko ila na yy kaja na tamko la kuvuruga upepo. " Uongo una mwisho wake"
 
Back
Top Bottom