Kwa majibu haya kero za wananchi zitatatuliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa majibu haya kero za wananchi zitatatuliwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kivato, Jul 12, 2011.

 1. k

  kivato Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  MAJIBU YA MAWAZIRI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TNZANIA DHIDI YA KERO ZA WANANCHI

  1. Swali alilouliza mbunge ni kweli lipo na serikali ina taarifa nalo
  2. Suala hili ni nyeti na hasa kwa usalama wa nchi yetu
  3. Hata hivyo katika ziara yake Mh. Rais ameonana na wafadhili na kufanya nao mazungumzo na wameahidi kutusaidia
  4. Lipo kwenye sera ya chama
  5. Serikali ni sikivu
  6. Mchakato utakapokamilika litatatuliwa na litakuwa historia kwa wananchi wetu
  7. Kama ilivyotolewa ufafanuzi kwenye jibu la msingi, upembuzi yakinifu umekamilika
  8. Utekelezaji unategemea fedha za wafadhili
  9. Kadiri fedha zitakavyotolewa na wafadhili
  10. Waheshimiwa muwe wavumilivu naamini kabla ya mwaka 2015 mradi utakuwa umekamilika
  11. Nashangaa watu wanaobeza jitihada za serikali
  12. Kwenye mwaka huu wa fedha ni mradi uliotengewa bilioni .... za fedha
  13. Kufanya tathmini upya ya wananchi watakaofidiwa na fedha hii inategemea kutolewa na wafadhili na serikali ya ...... (marekani) imekubali kutoa hela
  14. Kutambua nchi hii ni kubwa na vipaumbele ni vingi
  15. Serikali inafikiri kabla ya kuanza ..... tunahitaji kupitia sheria zetu na kuona namna ya kulitekeleza
  16. Serikali haina taarifa nalo
  17. Ikibanika serikali itachukua hatua kali
  18. Serikali inafikiria ni namna gani ya kuwasiliana na wadau wake kuona namna gani
  19. Mchakato wa katiba mpya
  20. Ni kati ya vitu ambavyo ni vya kujivunia ambavyo serikali yetu imevifanya
  21. Wananchi wapewe fursa bila kuingiliwa
  22. Kabla ya uchaguzi mkuu ujao
  23. Ni tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali yetu
  24. Suala hili liko mahakamani na haturuhusiwi kuingila uhuru wa mahakama
  25. Lipo kwenye ilani ya CCM
  26. Kwenye hotuba ya Mh. Rais kwenye hotuba ya ufunguzi wa bunge
  27. Kujitafutia umaarufu wa kisiasa
  Changamoto

  1. Kwa majibu haya kero za wananchi wetu zitatatuliwa?
  2. Wanafunzi wetu wakitumia mtindo huu mashuleni tutegemee kuwa na kizazi gani?
  3. Je nchi za wenzetu hasa Afrika Mashariki majibu yanayotolewa na mawaziri wao yanalingana na haya ya mawaziri wetu?
  4. Umakini wa serikali yetu katika kutatua kero za wananchi unaweza kupimwa na viongozi waliopo katika serikali hii kwa majibu haya?
  5. Ukitathimini majibu haya unapata picha gani?
   
 2. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  copy and paste replies, simply tune to this and try that and see the reaction!
   
 3. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Serikali ikiishadharau wananchi na kuwaona ama hawana uelewa wa mambo ama wengi wao wana uchu wa kuambulia chochote ama hawana ubavu wa kuiondoa madarakani, hutoa majibu muflisi (na ya kejeli) ya aina hiyo.
   
Loading...