Kwa mahitaji ya Mfumo unao endelea kutoa umeme katika nyumba baada ya umeme wa tanesco kukatika (Electricity backup)

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Un interupted Power Supply (UPS) au powe nack up Ni mfumo ambao unasaidia upatikanaji wa umeme hata baada ya umeme wa Tanesco kukatika.

Mfumo huu unaweza kutumia vyanzo mbadala vya nishati kama Solar power,Wind power au Generator.

Lakini pia mfumo huu unaweza kutumia nishati hiyo hiyo ya Tanesco kama nishati itakayo tumika wakati umeme wa tanesco umekatika.

MFUMO WA KUHIFADHI UMEME WA TANESCO NA KUUTUMIA BAADAE KAMA UKIKATIKA.

Mfumo huu unakuwa ukihifadhi (banking),kiasi cha umeme wakati umeme wa Tanesco upo.Na baadae umeme huo utaweza kutumika kama nishati mbadala baada ya umeme kukatika.

Mfumo huu unatumia battery kuhifadhi umeme huo,ikiwa na maana wakati umeme wa tanesco upo unakua ukichaji battery hizo na umeme wa tanesco ukikatika battery hizo ndiyo zitatumia chaji iliyohifadhiwa katika kusambaza umeme katika nyumba.

Uwezo wa battry kutoa umeme unatofautiana kulingana na vifaa vitakavyo tumika kipindi ambacho umeme umekatika.

Kwa kawaida batteries inaviwango vyake binafsi katika kutoa umeme.Hivyo ukubwa wa bettery ndiyo hasa msingi mkuu wa uwezo wa mfumo huu.

Ifuatayo ni mchanganuo wa battery na uwezo wake katika kusambaza umeme katika nyumba au vifaa vyako.

1.Battery 100AH moja (yenye volt 12).
Watt 50 AC = muda wa masaa 17
Watt 100 AC = muda wa masaa 8
Watt 150 AC = muda wa masaa 5
Watt 200 AC = Muda wa masaa 3

2.Bettery 200 AH (yenye volt 12)

Watt 50 AC = muda wa masaa 35
Watt 100 AC = muda wa masaa 17
Watt 150 AC = muda wa masaa 10
Watt 200 AC = Muda wa masaa 7
Watt 300 Ac = Muda wa masaa 4
Watt 400 AC = Muda wa masaa 2

3.Battery 400 AH (yenye Volt 12 )

Watt 50 AC = muda wa masaa 75
Watt 100 AC = muda wa masaa 35
Watt 150 AC = muda wa masaa 23
Watt 200 AC = Muda wa masaa 17
Watt 300 Ac = Muda wa masaa 10
Watt 400 AC = Muda wa masaa 7

4. Battery 600 AH (Yenye volt 12)

Watt 50 AC = muda wa masaa 115
Watt 100 AC = muda wa masaa 55
Watt 150 AC = muda wa masaa 35
Watt 200 AC = Muda wa masaa 26
Watt 300 Ac = Muda wa masaa 18
Watt 400 AC = Muda wa masaa 13
Watt 500 AC = Muda wa masaa 11
Watt 600 AC = Muda wa masaa 8
Watt 700 Ac = Muda wa masaa 7
Watt 800 Ac = Muda wa masaa 6
Watt 900 Ac = Muda wa masaa 5
Watt 1000 Ac = Muda wa masaa 4

NB kuanzia watt 1500 na kuendelea inveter itatumika ya Volt 24 hivyo itakua inatumia bettery 2 kwa kila AH ili kupata 24 Voltage.


Unaweza kufunga ukubwa wowote kulingana na uwezo wako


Gharama za ufungaji ni kama ifuatavyo

BATTERY

Battery ya 100Ah = 280,000/= kwa moja
Battery ya 200Ah 500,000/- kwa moja

Utanunua idadi ya bettery kulingana na kiasi cha AH ambacho unataka system yako iweze kutoa.

WIRERING

Gharama za Inveter,Control chager Cables na service charge.

100 - 300 watt Tsh 300,000/- pamoja na modifide sinewave inveter

400 -500 watt ts 450,000/- pamoja na modified sine wave onveter

500 - 1000 watt Tsh 750,000/- pamoja na pure sine wave inveter

2000 -3000 Watt Tsh 150,000/- pamoja na pure sine wave inveter

4000 - 5000 watt Tsh 2,000,000/- pamoja na pure sine wave inveter

Kwa maswali ya zaidi au ya kitaalamu uliza hapa jukwaani nitajibu.

au piga 0629068815
 
Safi, mimi binafsi backup yangu ni solar power. Niliweka system mbili solar na umeme wa kawaida.

Hii back up yako naona ghali na pia ni solution ya muda mfupi tu.
 
Unaweza kununua kila kitu mwenyewe (japo guarantee sitakupa)Then mimi nikakuchaji gharama ya wirerjng tu bei itapungua sana.
Safi, mimi binafsi backup yangu ni solar power. Niliweka system mbili solar na umeme wa kawaida.

Hii back up yako naona ghali na pia ni solution ya muda mfupi tu.
 
Back
Top Bottom