kwa mageuzi haya ni dhahiri kwamba CCM imekuja na mwarobaini wa matatizo ya watanzania

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
Na

Augustine Chiwinga.

Chama Cha Mapinduzi CCM Leo tarehe 12 March 2017, kimefanya mkutano wake mkuu maalumu ambao ulikua na lengo kuu moja la kupitisha mapendekezo ya maboresho ya katiba yake.
Maboresho hayo ya katiba kiukweli yamekuja katika kipindi muafaka kulingana na hali ya kisiasa na kijamii tuliyonayo Tanzania kwa hivi sasa.
Mageuzi ambayo CCM imeyafanya leo ni mwarobaini wa matatizo ya muda mrefu ya watanzania kwani yanalenga katika kuleta ufanisi wa kiutendaji kwa watumishi wa serikali wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi pamoja na watumishi ndani ya chama.
Kwa wasiojua ni kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeingia mkataba na wananchi wa kuwatatulia kero zao na kuwaletea maendeleo, na katika kutekeleza masharti ya mkataba huo ilikua ni lazima kwa Chama Cha Mapinduzi kufanya mageuzi kama haya katika zama hizi ambazo wananchi wana matarajio makubwa kabisa na CCM.
Mageuzi inayoyafanya CCM ni pamoja aina ya viongozi inaowataka kwa maaana ya kua na viongozi waadilifu, waaminifu,wanyenyekevu, wachapakazi,weledi na wenye kujitolea nafsi zao kwa ajili ya chama na serikali inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi.
CCM ni chama kinachounda dola na kwa hivyo ililazimika kufanya mageuzi haya ili kupata viongozi wasio wapokea wala watoa rushwa , wasio wabadhirifu ,wasiojilimbikizia mali na wasiotumia dhamana ya uongozi waliopewa kunyanyasa wengine au kujinufaisha wao na familia zao.
CCM imefanya mageuzi makubwa haya sio kwa bahati mbaya bali ni kwa makusudi kabisa baada ya kuona kwamba mdudu unaoitwa rushwa na ufisadi ndio unaokwamisha upatikanaji wa maendeleo ya haraka kwa nchi hii.
Miaka ya zamani watu wengi haswa wapinzani walisema kwamba huwezi kupigana na rushwa bila ya kuondoa kwanza mfumo wenyewe wa rushwa.
Kupitia mageuzi haya makubwa kabisa Chama Cha Mapinduzi kimeondosha kabisa mfumo huo uliokua unatoa mwanya kwa wenye pesa kutumia rushwa kupata uongozi.

Pia mageuzi haya ambayo kwa sasa mtu mmoja sasa anaruhusiwa kua na cheo kimoja tu yanalenga katika kuleta ufanisi kwa chama na serikali kwa maana ya kwamba inampunguzia mtu mmoja kubeba majukumu mengi hivyo kusababisha kufifisha shughuli za kimaendeleo katika maeneo husika. Pia inaondoa mgongano wa kiutendaji baina ya viongozi.
Kwa maana ya kwamba sasa mtu mmoja atakua anatumikia cheo kimoja hivyo atawekeza nguvu na raslimali zake zote katika jukumu hilo moja tofauti na miaka ya zamani ambapo ilimlazimu mtu huyu kujigawa muda wake katika kutekeleza majukumu mengi aliyojitwisha.Kwa hivyo imeondosha kabisa uwezekano wa mtu kujirundukia vyeo vyingi ili kutumia kama kichaka cha kujilinda ili asiguswe pale anapokiuka miiko ya uongozi .

CCM sasa imerudishwa kwa wanachama , wanachama ndo wenye maamuzi ya mwisho kwenye CCM, mageuzi haya yanafanya viongozi wa CCM kuisimamia serikali kikamilifu katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mageuzi mapya ya CCM katika kujenga uchumi wa kati wa viwanda pia yameelekeza viongozi wa CCM na serikali kushiriki na kuhimiza wananchi wafanya shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na ufugaji wa kisasa.CCM imeondoa kabisa mfumo wa umangimeza wa viongozi kukaa ofisini tu na kusubiri kuletewa report badala ya kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa haraka.Sasa ni lazima viongozi wanaotokana na CCM kushughulika na kero za wananchi moja kwa moja kama vile mageuzi mapya yanavyotaka.
Hii ndio CCM mpya kwa ufupi na jinsi ilivyokuja na mwarobaini wa kuipaisha kimaendeleo Tanzania.
Asanteni wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa kupitisha kwa kauli moja mabadiliko haya ya katiba kwa maslahi mapana ya CCM na taifa.

Augustine Chiwinga.
 
Mnatia kinyaa sana!! Hakuna watu hopeless na wanaotia kinyaa kama sisi!! Sijasikia ajenda yoyote ya kuwaletea unafuu wa Tanzania huko Dodoma zaidi ya kujadili namna ya kusalia madarakani!! Cha ajabu mijitu yenye akili za kimbwa inasifu eti unafuu kwa wananchi.... Hayo mabadiliko yataboresha vipi uchumi wetu?

Sisi ni mazalia ya laana tupu!
 
Bure kabisa kama bashite.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom