Kwa Mafuriko yale ya Nape Anapaswa Kupita bila Kupingwa 2020

Tunutu kiwavi

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
528
215
Katika uchaguzi uliopita 2015 ndugu zetu wanamadiliko uchwara walitudanganya eti Nape hakubaliki katika jimbo lake La Mtama. Ndugu zetu hawa walidiriki kututengezea picha za bandia zikionesha kuwa eti wanaccm wanarudisha kadi zao za uanachama. Huku wakiendelea kujifurahisha eti Nape katika mikutano yake alikua anajaza watu kwa malori. Hatimae matokeo ya uchaguzi yaliwaacha midomo wazi na kudhihisha uongo wao kwa Nape kushinda kwa kishindo dhidi ya wapinzani wake. Kama kawaida ya wanamadiliko wetu uchwara bila aibu waliendelea kusingizia kuwa waliibiwa kura.

Mkutano wa jana umedhihirisha umma kuwa ni jinsi gani Nape anavyokubalika katika jimbo lake. Hili halina ubishi tena kwani hata wale, nyumbu, wafia chama, chadema asilia, chadema in blood, UKAWA orijino, UKAWA feki na CCM kwa kwa pamoja wameungana na kukubali kuwa nape katika jimbo lake si tu hana mpizani bali ni moto wa kuotea mbali anayeonesha kwamba yoyote atakaye tia pua dhidi yake atakiona cha mtema kuni 2020.

USHAURI

Vyama upinzani 2020 msijaribu kuweka wagombea wenu jimbo la mtama mtapata aibu

Mwacheni tu ndugu Nape Moses Nnauye apite bila kupingwa.
 
Hii ishu ya Nape 2017 ni kama ya Lowassa 2008 lakini Nape naona anajiingiza mwenyewe choo cha kike. Wanaompinga JPM watataka kumtumia Nape ili kufanikisha maovu yao. Bado Nape siyo potential kihivyo na nina uhakika hadi december 2017 atakuwa amesahaulika na drama zake binafsi.
 
Potential ni Nani kwa sasa
 
We UOTE="Cannibal OX, post: 20577615, member: 243249"]JPM.[/QUOTE]
We jamaa unazingua.Sasa huwezi kumuingia mkuu wakati yeye ndio mwenye nchi.Kwa wengine Nani ni potential
 
Mkuu kujaza watu mkutano wa nape hakuna uhusiano na siasa za vyama. wana mtama walifika kwa wingi kusikiliza nini kilichomfika mbunge wao, na hasa baada ya tukio baya la kuhuzunisha la kuonyeshwa mtutu wa bastola ili kumziba mdomo asipate nafasi kufikisha ujumbe wake kwa jamii. kuingiza siasa kwenye tukio hilo ni kujaribu kuwagawa watu kwenye kipindi hiki ambacho taifa linaingizwa kwenye taharuki ya matukio utekaji na kuonyeshana silaha za moto hadharani
 
Anaweza asiwe mwana ccm wakati huo.
Jipe moyo
 
Kumbuka mkutano wa jana uliandaliwa kwa pamoja na Chadema kwa kushirikiana na wabaya wa Magufuli.

Lile jimbo Chadema ndio walishinda, ila Nape akatumia uccm wake kupiga goli la mkono.

Nappe alichangia kufungwa jela yule mwenyekiti wa Chadema lindi ambaye ndio alikuwa mshindani wake.....Ambaye kiuhalisia ndio mshindi wa lile jimbo....

Ila kwa sababu siasa za Tanzania ni za Uchwara Uchwara , leo Chadema wale wale ndio wapambe wa Nappe na ndio waliofanikisha kwa kiasi kikubwa ule mkutano.

Yale maigizo ya udhalilishaji wa Nape kupita juu ya matako ya akina mama mtama yaliandaliwa kwa ustadi ilimradi ionekane Nape anakubalika .

Lakini ukweli wenye akili wanajua...

146c6638fb57b57be0281f84a7ae56ec.jpg
 
Hii ishu ya Nape 2017 ni kama ya Lowassa 2008 lakini Nape naona anajiingiza mwenyewe choo cha kike. Wanaompinga JPM watataka kumtumia Nape ili kufanikisha maovu yao. Bado Nape siyo potential kihivyo na nina uhakika hadi december 2017 atakuwa amesahaulika na drama zake binafsi.
Kwa maoni yangu mimi ningemshauri akae kimya tu. Akiendelea na mwendo huu anaokwenda nao, mimi nahisi atajivunjia tu heshima yake na hatimaye atapotea kabisa.
 
Siasa za tz ni dynamic huwez jua nn kitatokea siku zijazo esp kat ya nape na ccm na nape na ********...
Tusiongee yooote tukayamaliza sahv 2020 bado mbali
 
Kwa maoni yangu mimi ningemshauri akae kimya tu. Akiendelea na mwendo huu anaokwenda nao, mimi nahisi atajivunjia tu heshima yake na hatimaye atapotea kabisa.
Ni kweli anatakiwa Awatumikie wana Mtama, hiyo mipasho yake aache kama alivyoacha Mzee Yusuph.
 
Back
Top Bottom