Kwa mafanikio haya, Magufuli kuchukua kura zote Mkoani Shinyanga

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Na Baraka Mina.

Waingereza wanasema “Seeing is believing” yaani “kuona ni kuamini”. Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari John Pombe Joseph Magufuli siku ya leo (03/09/2020) majira ya tano asubuhi kwenda saa sita mchana atakuwa anawasili katika viwanja vya Kambarage mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuendelea na kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kipindi cha pili kwa mwaka 2020 – 2025.

Nimefika mkoani Shinyanga na kuona mafanikio mengi, yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yatakayochochea ushindi wa kishindo na kumfanya JPM achukue kura zote hapa mkoani Shinyanga.

  • Ukarabati wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga: Ukarabati wa hospitali hii umepanua wigo wa utoaji wa huduma bora na za kisasa za afya katika mkoa huu. Katika hili wanaShinyanga hawataacha kumpa kura JPM.
  • Kuweka taa za umeme wa jua katika barabara za halmashauri za Shinyanga: Usalama wa watumiaji wa barabara umeimilika, usiku umekua mchana pale Shinyanga. Nani atapiga kura kwa wapinzani?
  • Ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 35,000 katika mkoa wa Shinyanga: Ni jambo la kujivunia na kushukuru, wakulima wanasema katika hili wameipa tano serikali ya awamu ya tano na wataichagua tena kwa miaka mitano ijayo.
  • Kuboresha makazi ya wazee kwa kukarabati na kujenga miundombinu mipya katika makazi ya wazee ya Kolandoto: Wazee hawajasahaulika, wanaishi katika makazi bora. Bado kura zitaenda kwa JPM, hawataweza kumuacha.
  • Kuimarisha barabara zenye kwa kiwango cha lami katika manispaa ya Shinyanga: Barabara pale manispaa zina lami safi na imara, unasafiri bila shida huku ukikumbuka idadi ya ng’ombe ulizonazo. Hapa wapinzani wameshapigwa.
  • Kurejeshwa kwa mali za vyama vya ushirika zilizokuwa zimeuzwa kiholela na nyingine kuporwa zikiwemo nyumba za makazi, maghala, viwanda na viwanja: Chama Kikuu cha Ushirika SHIRECU Ltd pale Shinyanga kinashuhudia bila kupepesa macho, hata kampeni zikiwa miaka miwili nawahakikishieni wanaushirika watampa kura JPM.
  • Kuhamasisha ufugaji wa samaki katika mkoa wa Shinyanga ambapo mabwawa 103 yamejimbwa na kujengwa: Wafugaji wa samaki wao wanasema JPM anatosha, leo wanaenda kusikiliza sera thabiti kwa miaka mitano ijayo. Hawa wana mapenzi ya dhati na JPM hawataweza kumsaliti.
  • Kuboresha huduma za machinjio kwa kujenga machinjio ya kisasa katika halmashauri ya Shinyanga: Niliwasikiliza kwa makini na utulivu wafanyabiashara pale machijioni, walilisisitiza waziwazi kura zao kwa JPM. Sioni kama kuna mgombea urais atawabadilisha akili.
  • Kutengwa kwa maeneo rasmi kwa ajili ya wajasiriamali wakiwemo mama lishe na wauza mbogamboga kufanyia biashara: Mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa ambayo maeneo yametengwa, hawa nao wana mapenzi yaliyoshiba na yakashibana na JPM, wapinzani wajipange mikoa mingine pale Shinyanga wataaibika wakiwa na miwani ya mbao.
  • Ujenzi wa mabwawa umeanza kutekelezwa, ikiwemo bwawa la Seke Ididi: Mradi huu wa mabwawa ni kwa ajili ya kutatua kero ya maji. Je unahisi JPM atatoswa na wanaShinyanga jibu ni moja HAPANA.
  • Kuanzishwa kwa vituo vya huduma ya mkono kwa mkono (One stop centres) ili kulinda haki za wanawake katika mkoa wa Shinyanga: Vituo hivi ni mfumo wa kuweka na kuimarisha haki kwa wanawake, kupitia hili kinamama watampa kura JPM.

JPM atashinda kwa kura zote pale Shinyanga, tuombe Mwenyezi Mungu atujalie uzima tushuhudie ushindi huu wa kishindo pale Shinyanga.

Nitarejea baadae ngoja niendelee kumsikiliza JPM kupitia matangazo ya moja kwa moja. Mungu atubariki sote.

Wako Baraka Mina.
Email: barakamina20@gmail.com
 
Tuko pamoja Baraka Mina, tutaendelea kushare maandiko yako.
 
Back
Top Bottom