Kwa madereva hawa ajali hazitaisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa madereva hawa ajali hazitaisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Oct 19, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia hii picha ndo utajua kwa nini ajali Tanzania hazitaisha.
  [​IMG]
  Hii picha inaonyesha basi liki-overtake lori kwenye mlima na hapa ni maeneo ya karibu na chalinze ukitokea morogoro.
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kweli umenena. Ni mara nyingi nishakutana na hali kama hii wakati unapandisha kilima na unakutana na gari ina overtake! Hapo kuna mstari unaonyesha wazi wazi kuwa huwezi ku overtake, lakini huyu dereva wa minibus anahatarisha maisha ya abiria, pamoja na wale kwenye gari linalokuja usoni. Ni vizuri kama ikiwezekana kuchukua namba za magari hayo na madereva wake kuchukuliwa hatua kali. Vile vile ukaguzi wa leseni na mafunzo zaidi kwa madereva wa mabasi ni muhimu.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiyo siyo mini bus ni basi kubwa la aina ya super class andare la abiria 60.
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  hawasikii hata uwapigie tarumbeta.....sasa kinachomfanya afanye overtaking sehemu hii ni kipi? Na tena pamechorwa mstari ambao hauruhusu kufanya overtaking ... Anafaa achapwe viboko...
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kunifahamisha. Sikutazama vizuri!
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sheria sheria sheria sheria sheria pamoja na wasimazi sijui hawajui kuzisoma au ndo njaa,Ee Mwenyezi tusaidie hili tongotongo la akili litoke
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mie sipati picha hapa ina maana madereva wanakuwa hawajui sheria za barabarani au ni kiburi chao bila kujali maisha ya abaria
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Hicho ndo kinashangaza, lakini labda ni haraka na mara nyingi haraka haraka zina leta matatizo.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu nilikuwa nyanda za juu kusini takribani wiki moja iliyopita, na nilibahatika kushuhudia the same story - Hili basi linasafiri DAR - Mbeya/Songea linaitwa LULALWEDI. Nadhani SUMATRA inabidi walikague upya inawezekana lina chasis ya lori! Linakimbia kwelikweli - Nilipiga simu Polisi lakini sina uhakika kama kuna hatua zilichukuliwa/zitachukuliwa!
   
 10. M

  Msindima JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  FL1 sheria wanazijua sana tu wanapozivunja wanaelewa kabisa kwamba hapa nimevunja sheria,wengi wao ni vichwa ngumu sana,na wengine pia unakuta leseni zao ni zile za kufanyiwa mpango na ndugu hakupitia chuo chochote kujifunza sheria na unakuta anaingia barabarani na kuanza kubeba abiria,niliiona hiyo picha asubuhi kwenye site ya Ippmedia nikabaki na mshangao tu nikawaza kweli sijui tutaponea wapi na hawa madereva.

  Hebu pata hii picha jamaa alikua ni kondakta wa daladala mara unashangaa unamwona anaendesha gari tena amepakia abiria jiulize kwanza amepataje leseni kwa kipindi kifupi na pia je anazijua vizuri sheria za barabarani? Jumamosi kuna dala dala nilipanda na yule aliekuwa anaendesha niliwahi kumwona akiwa konda,nilipata maswali mengi sana,nikajiuliza huyu kweli atatufikisha huko tunakoenda? na kuna kituo tulifika trafiki akamsimamisha akamwambia kama leo ikiisha salama bila kukuweka Lock-up umshukuru Mungu,nikapata swali lingine ina maana huyu askari anamfahamu jamaa?

  Kingine nionacho ambacho kinasababisha tunakuwa na ma-driver wa ajabu ni hawa askari wanaotoa leseni kwa watu ambao hawaja-qualify kuwa ma-driver, sasa sielewi tutaponea wapi?
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sheria zetu za barabarani ni kali, ila utekelezaji ni sifuri kabisa. Leseni za kufoji ni tatizo kubwa sana na ndio chanzo cha ajali sio madereva wote wenye lesseni halali. Kwa hali hiyo akipelekwa mahakamani anakubali kosa anapigwa faini anafungiwa kuendesa miaka mitatu kesho yake ananenda kununua leseni nyingine ya kufoji na kuendelea kuuwa watu.Sio hiyo, wapelelezi wakubwa kaika kesi za traffic ni askari wa usalama barabarani, hawa muda wote wanaongoza magari na wakipumzika kidogo ni misafara ya viongozi mpaka muda wa mahakama unanapoisha, matokeo yake wahatokei mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi na mwishowe kesi hufutwa na madereva anatoka huru kuuwa watu wengine.Mwisho kabisa ni uroho wa hela kwa wanaotoa leseni zingine ni halali lakini zinavyotolewa duh, utata mtupu, zinauzwa kama njugu, unaweza kupewa leseni wakati hujui hata kushika usukani achilia mbali sheria za barabara. tutegemee nini???? ndio hiyo picha.WENGI WETU TUNAEZA KUYAFANYA MAGARI YAENDE WACHACHE SANA WANAJUA KUENDESHA
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 684
  Trophy Points: 280
  Hii mirungi wanayotafuna wakidhani matembele itatumaliza sana!!!
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Mkuu linaitwa 'LUTELWEDI'

  Hii nakubaliana na wewe!
  Kuna mabasi kadhaa ambayo nimeshuhudia madereva wakila mirungi. Hii i hatari sana kwwa usalama wa raia.
   
 14. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji Rais Fyatuuuuuuuu, Nakumbuka Thread ya Mwkjj
   
 15. F

  Fadhila Member

  #15
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila na sisi abiria tunaopenda kushabikia madereva wanaoendesha bila kuzingatia sheria vile vile tunatakiwa kujirekebisha. Mimi nilishawahi kupanda basi dereva alikuwa anaendesha kama mwehu na mimi peke yangu ndani ya basi ndio nilikuwa napiga kelele apunguze mwendo. Hakuna hata abiria mmoja aliyenisupport. Ikitokea ajali akalipindua basi ndio utasikia heee dereva alikuwa anakimbia sana!
   
Loading...