GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,865
Nianze kwa kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Watanzania wote Kuanzia kwa Serikali na hasa hasa TFF kwa kuiandaa vyema kabisa Timu yetu ya Taifa kiasi kwamba ‘ Maandalizi ‘ yake ya awali tu yamekuwa ni mazuri, yanatia matumaini kuliko hata Timu za Taifa za Majirani wetu Kenya na Uganda.
Wakati ‘ Maandalizi ‘ mazuri ya Taifa Stars yakiwa Boko na Uwanja wa Taifa huku Wachezaji wake muda mwingi tukipishana nao Mitaani na Vijiweni hadi maeneo ya Kula ‘ Bata ‘ wenzao wasiojua mpira na wabovu Timu ya Taifa ya Kenya ( Harambee Stars ) wao wapo Kambini sasa nchini Ufaransa huku Timu ya Taifa ya Uganda ( Uganda Cranes ) wao wakiwa Kambini huko Falme za Kiarabu.
Nichukue tu nafasi hii kuwaomba Watanzania wote tujiandae Kuipokea Timu yetu ya Taifa Stars pale itakaporudi na Kombe la AFCON 2019 huku tukiwa tumejazana Barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kwani siyo Siri kwa ' Maandalizi ' haya mazuri na ya Kisayansi kabisa huku Wachezaji Wetu muda mwingi wakipiga ' Story ' Vyumbani na Koridoni pale White Sand Hotel na Mabinti wa Mjini kubadilishana Kuingia Vyumbani mwao ni hakika kama kuna mwaka ambao Tanzania kupitia Taifa Stars yetu tunaenda Kufurahi basi ni huu.
Hongereni sana Taifa Stars, Benchi la Ufundi na Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF )
Nawasilisha.