Kwa maamuzi ya leo naamini wazee ni hazina. Hongera Sana mzee Msekwa

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Licha ya kuongea kwa kusisitiza uharamu wa Mdee na wenzake kutotambulika kama wabunge rasmi lakini kuna wengine waliona hayupo sahihi ikiwemo Spika Tulia. Mzee Msekwa katuonesha ni namna gani mtu anatakiwa kusimamia anachoamini.

Nami binafsi niliona Mdee na wenzake hawakustahili kuwepo pale lakini walistahili kusamehewa zaidi lakini kwa maamuzi yaliyofikiwa na mkutano mkuu wa CHADEMA ni budi yaheshimiwe na kukubaliwa hata kwa Spika Tulia.

Ninajua huu ni wakati mgumu kwa Spika Tulia ,ni wakati wa kula matapishi yake au ni wa kuweka uspika wake rehani. Mwenyekiti wa CCM ambaye Mara zote anaamini ushirikiano na vyama vingine vitaleta umoja wa kitaifa kwa hakika hawezi kutokubaliana na uamuzi wa CHADEMA wa kuwavua uanachama.

Swali:Je, msimamo wa Spika utabaki uleule?

Natamani nione Spika akisimama katika maimamo wake ili nione ukuu na mamlaka ya bunge lakini hiki ninachokitamani ni ndoto ya kutisha.

Mwisho, Kama Kuna sehemu tulishindwa kusikiliza ushauri wa wazee huu ni wakati sahihi wa kufanya hivyo. Kuna mengi wazee wetu wanayajua lakini wanaamua kukaa kukaa kimya kutojihusisha na siasa za kileo, tusiwaache wakae kimya waongee ili taifa lipate kuponywa. Wazee ni hazina, tuwatumie.

Hongereni CHADEMA kwa Sababu kilichofanywa leo kingefanywa na CCM na tofauti ni kwamba CCM wangewafukuza mapema zaidi.
 
Msekwa alikurupuka kutolea maamuzi kabla kesi haijaisha. Leo ndipo Mdee na wenzake wamekosa sifa, lakini Msekwa aliongea kwa hisia zake kufuate maneno ya mitaani tu bila kuwa na nyaraka zinazoonyesha kuwa Mdee na wenzake kweli hawana sifa.
 
Msekwa alikurupuka kutolea maamuzi kabla kesi haijaisha. Leo ndipo Mdee na wenzake wamekosa sifa, lakini Msekwa aliongea kwa hisia zake kufuate maneno ya mitaani tu bila kuwa na nyaraka zinazoonyesha kuwa Mdee na wenzake kweli hawana sifa.
Taratibu na kanuni za bunge hazikuanza kwa Mgogo au Tulia zipo toka kipindi hiko akiwa ni Spika hivyo anazifahamu vyema Sana. Mzee Msekwa hakukurupuka Kuna siri alikuwa anaijua ukiachana na hisia unazosema hivo leo ameonesha thamani ya kusikiliza wazee
 
Kabla ya wazee tayari kulikuwa na kanuni, mzee alipitia kwenye kanuni za bunge na kuongea so maudhui ya kutoa tamko yanatokana na kile mzee alichokuwa anakisimamia akiwa juu.
 
Back
Top Bottom