Kwa maamuzi ya JPM Mwanza na Shinyanga, tumerejea kwenye safari yetu ya Mapinduzi

Landson Tz

JF-Expert Member
May 8, 2011
295
221
Mapinduzi ya hiari ni process inayopaswa kuendelae kila siku katika jamii iliyo hai. Mapinduzi yapo ya aina mbili: Mapinduzi chanya na Mapinduzi hasi. Mapinduzi chanya ni yale yenye manufaa kwa jamii kwa ujumla, Mapinduzi hasi ni yale yenye manufaa kwa mtu au kikundi cha watu.

Kwa nchi yetu, Mapinduzi ya kwanza yalifanyika wakati wa kupigania uhuru na hatimaye tukapata uhuru 1961. Mapinduzi ya pili yalifanyika 1967 kwa Azimio la Arusha, mapinduzi ya tatu yalifanyika 1977 kwa kuanzisha chama cha mapinduzi, Mapinduzi ya nne yalifanyika 1991 kwa azimio la Zanzibar na mapinduzi ya tano yalifanyika 1992 kwa kuanzisha vyama vingi.

Na sasa tunahitaji mapinduzi ya sita ya amani, mapinduzi ya uchumi. Mapinduzi ya kuwawezesha wanyonge kutoka katika ukoloni wa unyonge na umaskini wa kutupwa. Hii kazi JPM hawezi kuiepuka, ameisha ianza, namuomba aiwekee muongozo ili jamii nzima ya Watanzania ishiriki.


Tangu mwaka 1991 baada ya azimio la Zanzibar, kumejengwa ukuta mkubwa miongoni mwa jamii, ukuta unaotenganisha walio nacho na wasionacho. Ukuta huu umejengwa muda mrefu (kuanzia miaka ya 1990 hadi sasa). Kundi la wasionacho ni kubwa sana na ndilo kundi la wanyonge. Hawa wanapatikana mjini na vijijini. kilimo duni kimegeuka kuwa mateso kwa wakulima/wajamaa wa nchi hii. Kazi zingine kama madini, biashara ndondogo nazenyewe zimekuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa wanyonge.

Mwisho nashauri jamii ya kitanzania kupaza sauti zao kwa mambo ya msingi na kuchangia kwa uzalendo mada hii. Tuwe wepesi wa kuboresha kulipo kukosoa, maana watoa mada ni binadamu si wakamilifu na hilo hawajalidai.

Kama watanzania wangelijua sera za fedha na uchumi, mifumo ya fedha na mabenki ya kilibelari, sababu za umaskini wetu, ulibelari uliotamalaki nchini, hata kesho tungeshuhudia mapinduzi.
 
mi nahitaj tu mabadiliko ya kisiasa kwan siamin hawa waliotawala kwa miaka zaidi ya hamsin na kujihusisha na maovu kibao ikiwemo ufisadi na rushwa wanaweza kuisaidia nchi kusonga mbele kwa kasi inayoendana na rasilimali tulizonazo..............
 
Back
Top Bottom