Kwa lugha ya kiswahili haya maneno yapo sahihi

qaxemvule

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
230
117
Kwani kuna makabila fulani yanapenda sana kutamka kwenye Maneno yanayoanzia na herufi :"m" wao huweka herufi : "N" sasa sijui wao ndio wapo sahihi au laa
Kwamfano Maneno haya
Mkate: nkate
MTO: nto
Mchele: nchele
Mkeka: nkeka
Mchinje: nchinje
Mke: nke
Mkojo: nkojo
Mlete: nlete
Na n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayapo sahihi. Hayo maneno yalikuwa yanatumika zamani kabla ya kiswahili hakijapitia kwenye michakato mbali mbali km undondoshaji, uyeyushaji, ukakaishaiji n.k na pia usanifishaji.
Ukakaishaji.
Kyai-chai. Kwahiyo kyai halitumiki
Udondoshaji
mutu-mtu
maneno km hayo nke, nto, nchele hayatumiki ktk lugha ya kiswahili.
Kwenye usanifishaji tulipata maneno km Ng'e, mbwa n.k kwahiyo Lugha ya kiswahili imepitia michakato mingi sana mpaka kuwa hapa ndiyo maana ktk kiswahili tuna lugha sanifu na fasaha.
Sanifu. Crazy love ameenda kunya
Fasaha: crazy love ameenda kujisaidia
Hitimisho.
Hayo maneno hayatumiki ktk lugha ya kiswahili ni sawa na kiingereza viwakikishi km Thou, thee, thy hayatumiki
lkn yanaweza kutumika km misimu au rejesta lkn siyo kiswahili fasaha wala sanifu
 
Hayapo sahihi na hutokana na athari za matamshi kama mambo yanayoharibu lugha japo kupitia lafudhi zao huweza kumtambua mzungumzaji kijiografia Mfano, Niliendaga badala ya Nilienda(Hapa mzungumzaji ni Msukuma ambao wao hupenda kuongeza kitamkwa "ga" katika kitenzi), Nunua huyo mabati badala ya Nunua hayo mabati(Mjaluo), Kura tumekura pa kurara sasa(Mkurya), Ntonto nchanga(Mtwara)
 
Hayapo sahihi. Hayo maneno yalikuwa yanatumika zamani kabla ya kiswahili hakijapitia kwenye michakato mbali mbali km undondoshaji, uyeyushaji, ukakaishaiji n.k na pia usanifishaji.
Ukakaishaji.
Kyai-chai. Kwahiyo kyai halitumiki
Udondoshaji
mutu-mtu
maneno km hayo nke, nto, nchele hayatumiki ktk lugha ya kiswahili.
Kwenye usanifishaji tulipata maneno km Ng'e, mbwa n.k kwahiyo Lugha ya kiswahili imepitia michakato mingi sana mpaka kuwa hapa ndiyo maana ktk kiswahili tuna lugha sanifu na fasaha.
Sanifu. Crazy love ameenda kunya
Fasaha: crazy love ameenda kujisaidia
Hitimisho.
Hayo maneno hayatumiki ktk lugha ya kiswahili ni sawa na kiingereza viwakikishi km Thou, thee, thy hayatumiki
lkn yanaweza kutumika km misimu au rejesta lkn siyo kiswahili fasaha wala sanifu
Ndugu yagu wapo mpaka kesho tena tunao humuhumu miji mikuu tena dar wameyaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yagu wapo mpaka kesho tena tunao humuhumu miji mikuu tena dar wameyaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno kutumika haimaniishi ni maneno sahihi ya lugha husika, ndiyo maana tuna misimu na rejesta. Hayo maneno siyo sahihi japo yanatumika lkn siyo maneno sahihi ya Kiswahili fasaha au sanifu.
Maneno kama ntu, chacha, thatha, , nto, nke n.k ni maneno yanatokana na athari ya lugha mama. Msukuma, mjita, mpare, mkurya, makonde, mzinza na wengine wakiongea kiswahili kuna athari ya lugha mama itajitokeza katika maandishi, na lafudhi. Msukuma hawezi kuandika mtu, ataandika mutu (neno mutu alitumiki kwa sasa sbb hili neno limepitia undondoshaji. U- imedondoshwa kwa hiyo neno Mtu ndiyo sahihi na mutu siyo sahihi.
HITIMISHO
Hayo maneno nke, nto n.k ni maneno yanatokana na athari ya lugha mama. Ndiyo maana watumiaji wa maneno hayo wanajulikana ni watu wa kabila gani na wanatoka wapi. Kutumika kwa maneno haimaniishi ndiyo maneno sahihi ya lugha ya kiswahili. Watu hutumia lugha kuwasiliana kwa hiyo hakuna mipaka itakayomzuia mtu yoyote kutumia neno au kuanzisha neno. Ww hapo unaweza kuanzisha neno lolote lile na likatumika katika jamii ila tunapokuja katika lugha ya kiswahili fasaha na sanifu ndiyo hapo utakutana na mipaka na kusema neno nto siyo neno sahihi ktk lugha kiswahili japo utaendelea kutumia. Na ukienda jamii nyingine ukatumia hayo maneno watakucheka.
 
Kwani kuna makabila fulani yanapenda sana kutamka kwenye Maneno yanayoanzia na herufi :"m" wao huweka herufi : "N" sasa sijui wao ndio wapo sahihi au laa
Kwamfano Maneno haya
Mkate: nkate
MTO: nto
Mchele: nchele
Mkeka: nkeka
Mchinje: nchinje
Mke: nke
Mkojo: nkojo
Mlete: nlete
Na n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mikoa ya kusini lini na Mtwara ndo wanaongeaga hv
 
Hayapo sahihi. Hayo maneno yalikuwa yanatumika zamani kabla ya kiswahili hakijapitia kwenye michakato mbali mbali km undondoshaji, uyeyushaji, ukakaishaiji n.k na pia usanifishaji.
Ukakaishaji.
Kyai-chai. Kwahiyo kyai halitumiki
Udondoshaji
mutu-mtu
maneno km hayo nke, nto, nchele hayatumiki ktk lugha ya kiswahili.
Kwenye usanifishaji tulipata maneno km Ng'e, mbwa n.k kwahiyo Lugha ya kiswahili imepitia michakato mingi sana mpaka kuwa hapa ndiyo maana ktk kiswahili tuna lugha sanifu na fasaha.
Sanifu. Crazy love ameenda kunya
Fasaha: crazy love ameenda kujisaidia
Hitimisho.
Hayo maneno hayatumiki ktk lugha ya kiswahili ni sawa na kiingereza viwakikishi km Thou, thee, thy hayatumiki
lkn yanaweza kutumika km misimu au rejesta lkn siyo kiswahili fasaha wala sanifu
Kongole, umenikumbusha MICHAKATO YA KIUSILIMISHO & ISIYO YA KIUSILIMISHO.
 
Kwani kuna makabila fulani yanapenda sana kutamka kwenye Maneno yanayoanzia na herufi :"m" wao huweka herufi : "N" sasa sijui wao ndio wapo sahihi au laa
Kwamfano Maneno haya
Mkate: nkate
MTO: nto
Mchele: nchele
Mkeka: nkeka
Mchinje: nchinje
Mke: nke
Mkojo: nkojo
Mlete: nlete
Na n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kiswahili siyo sawa ila kwa kichewa na kimakonde cha msumbiji ni sawa ila inategemea ntu na ntu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom