Kwa lugha na mienendo ya viongozi wa sasa, bwawa la umeme lisingejengwa

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Maradhi na ukame vilikuwepo tangu enzi za mababu zetu tena magonjwa makali sana kuliko haya.

Hizi kejeli za kukosoa mradi wa bwawa la umeme kwa kisingizio cha kuharibu mazingira zikome kabisa

Rais Samia Hassan amesema kuna maradhi ambayo hayakuwepo siku za nyuma lakini yanajitokeza siku za karibuni kwa kuwa uharibifu wa misitu unasababisha Viumbe wa Msituni wasambae kwa Wanadamu

Amesema “Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi, ametoka ziara Mikoa ya Kusini (Lindi), ameniambia ameona maradhi mapya yameingia. Watu wanatokwa na damu za pua na wanadondoka chini”

Rais anaongeza "Hatujui ni kitu gani, Wanasayansi wamehamia huko kwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni Watu wengi wanaougua kwa mfululuzo, na yote ni kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule walikowekwa na Mungu. Tunawasogeza kwetu wanatuletea maradhi”

Rais Samia amezungumza hayo leo, Julai 12, 2022 katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika Mashariki (#AMECEA)
 
WATU waache kulakula vitu visivyojulikana! ... mara chamaki'nchanga, mara chamaki'uchiku(popo) ... 'ata huyo ngichi pia mchile! 😅😎😅
 
Hilo Bwawa Mzee si alikaa miaka 6 na alifikia wapi? Reli miaka 6 kafikia asilimia 46%. Kama tu hizi flyover na barabara za mwendokasi hakumaliza kwa wakati na hali yakuwa fedha zake zilishatengwa tangu yeye akiwa Waziri mpaka anakuwa Rais miaka 6 amekamilisha mbili tu. Hilo bwawa la Tril 16 angemaliza baada ya miaka 15 ( baada ya kujiongezea).

Kukopa kakopa sana miaka mitano kawazidi miaka 30 awamu ya pili mpaka ya nne na hakuna kilichofanyika pamoja na kuvunja rekodi za makusanyo ya mapato. Alisimamisha ajira, mishahara na madaraja akadai anajenga miradi na kaondoka miaka 6 hakuna nusu mradi uliokamilika

Lazima tugawe fedha za bajeti, miradi na fedha za maendeleo. Lazima watu waajiriwe, wapandishwe madaraja, walipwe posho zao n.k pia kuna miradi mingi elimu, maji n.k maendeleo ya vitu na ya watu pia .

Haiwezekani familia watembee uchi na viraka, peku , washinde njaa eti kwa sababu baba anajenga nyumba nzuri
 
Rais Samia hata hapo Dar ilipo ikulu yalikuwa makazi ya wanyama ila walikimbia ndio ikajengwa ikulu. Poli lolote ni makazi ya wanyama, kwa maendeleo yoyote hupatikana kwa wengine kupitia magumu.
Mfano ujenzi wa barabara kuna makazi ya watu yatavunjwa n.k
Nalog off Z
 
Yule jamaa hakupaswakuwa rais hata kwa siku moja au basi ni sawa kama ilivyotokea

Miaka 6 unatengeneza bomu la vijana wenye Msongo wa mawazo kwa kuwanyima ajira

Wafanyakazi kutoongezewa mishahara wala kupandishwa madaraja ya mishahara tena ya kisheria eti unatengeneza nchi kwa miradi isiyokwisha

Miaka 6 unakopa mikopo isiyoeleweka, masharti ya kibiashara, uliona wapi huo ujinga

Miaka 6 ya kuharibu diplomasia yetu, mpaka watu wakakosa soka la korosho na mbaazi kwa mifano

Miaka 6 ya kufunga kila mtu mdono, alafu unauliza ni wapi aliiba? Tungejuaje ikiwa vyombo vyote vya habar vilifungwa mdomo, na kila aliyethubutu kufungua mdomo kusema kweli alipotezwa au kutekwa na kuumizwa au kupewa kesi za money laundering

Yaan angeendelea kutawala, yanayotokea Sirilanka leo, yangekuja kutokea hapa bila ubishi wowote

Unadhan, baada ya kuchuka fedha za wafanyabiashara kwa nguvu kumalizika, angechukua tena fedha wapi?

Makundi kama Alshabab yangepata mtelezo wa kuchukua vijana wasio na ajira na kuwapa ajira, mtu alitengeneza Taifa la wamachinga, mpaka wafanyabiashara wa size ya kati nao wakaamua kuwa machinga?

Asante sana Mungu
 
Kukopa kakopa sana miaka mitano kawazidi miaka 30 awamu ya pili mpaka ya nne na hakuna kilichofanyika pamoja na kuvunja makusanyo ya mapato. Alisimamisha ajira, mishahara na madaraja akadai anajenga miradi na kaondoka miaka 6 hakuna nusu mradi uliokamilika
Jambo zuri hili. Weka namba mkuu tujikumbushe, tulinganishe na mihela ya sasa, kisha kupitia hizo data, tuongee nani kafanya nini.

Kuna vidaraja vinatumika sasa, vilishakamilishwa ile miaka 6, zile zahanati 400 pia zilikamilika nadhani, kila siku watu wanadandia mi-dreamliner kwenda kuzurula, natumai ni ile midege ya hiyo miaka 6, nasikia nyingine zilipelekwa nyumbani, ni miaka hiyo 6 sio? Hayo ma SGR, Bwawa, kusomesha watu bure n.k inawezekana ni miradi isiyokamilika kweli, tulinganishe ili kama KUMHUKUMU mtu tumhukumu kwa FACTS sio mapenzi na ubinafsi katika ulafi.

Nakumbuka kuna kama $2.29bn zimeingizwa miezi ile 8 ya kwanza, achilia mbali 600bn za Accacia, 512b za mazingira, Tozo n.k , weka tangible things so far kwa hiyo mifwedha na jinsi tulivyoweza ku-stimulate uchumi wetu kwa hivyo vimikopo kiduchu kama mnavyoona.
 
Kama Taifa hatuna priorities, ni wakati sasa tuwe na committee of national experts, tuwe na central thinking kama nchi, hii kutegemea mihemko ya mtu mmoja mmoja hamnakitu
 
Back
Top Bottom