Kwa Kweli Watu Wanapendezwa Sana na Mwisho wa Dunia

Wamjengoni

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
265
250
Je, una wasiwasi kuhusu wakati ujao? Ikiwa ndivyo, kuna watu wengi wanaohisi kama wewe. Tangu zamani za kale, watu wamekuwa wakikisia kuhusu wakati ujao wa ulimwengu huu, na wengi wamekata kauli kwamba hakuna tumaini. Kwa maelfu ya miaka, watu wametaka sana kujua jinsi mwisho wa dunia utakavyokuwa.

Kwa mfano, fikiria hadithi za kubuniwa za hivi karibuni. Vitabu vya katuni, televisheni, mamia ya sinema, na maelfu ya vitabu vinasimulia jinsi ambavyo ulimwengu huu utaangamizwa. Hadithi hizo zinasimulia jinsi ambavyo wanadamu watavamiwa na kuangamizwa na vitu fulani vyenye nguvu sana kama vile, roboti zenye kuua, majitu ya kila aina, viumbe kutoka sayari nyingine, madubwana, mizimu, majoka, sokwe, ndege, panya wenye umbo lisilo la kawaida, na nyigu wakubwa sana. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kuamini hadithi hizo!

Lakini kuna hadithi na nadharia nyingine ambazo huwaogopesha watu fulani. Baadhi ya nadharia hizo zinasemekana kuwa za kisayansi. Nadharia moja inasema kwamba tabaka lote la juu la dunia litasonga ghafula na hilo litasababisha (tsunami) zenye nguvu, matetemeko ya nchi, na volkano. Nyingine inadai kwamba sayari zote zitajipanga katika mstari mmoja na hilo litasababisha kuongezeka kwa upepo kutoka kwenye jua ambao utaleta uharibifu mkubwa duniani. Na bado nadharia nyingine inasema kwamba ncha za dunia zenye nguvu za sumaku zitajigeuza ghafula kuelekea upande mwingine na kusababisha mnururisho kutoka kwenye jua utuue sisi sote. Huenda usiwe na hofu. Hata hivyo, matukio hayo ya kuwaziwa bado yanawavutia watu wengi.

Namna gani vitabu vingi na Tovuti kuhusu mwisho wa dunia vilitabiri kwamba ulimwengu ungeisha Desemba 21 mwaka 2000? Chanzo kimoja kinadai kwamba sayari ya kuwaziwa inayoitwa Nibiru (au Sayari X) iko mwendoni kuja kugongana na dunia na itafika hapa Desemba 2050.

Watu fulani ambao wameamini matabiri kama hayo ya maangamizi, tayari wamejenga mahali pa kujificha nje ya nyumba zao au wamelipa pesa nyingi ili kujihifadhia vyumba katika mahandaki ya umma. Wengine wamehamia milimani mahali ambapo hakuna huduma za umma kama vile maji, vifaa vya kupasha nyumba joto, au umeme.

Lakini pia bila shaka, kuna watu ambao hawaamini hadithi na nadharia hizo. Wanapuuza wazo la kwamba mwisho wa dunia unakaribia. Kwa mfano, wanasayansi katika shirika la NASA wanasema hivi: “Dunia haitapatwa na madhara yoyote katika mwaka wa 2050. Kwa zaidi ya miaka bilioni 4 hakuna jambo lolote baya limeipata sayari yetu, na wanasayansi wenye kutumainika ulimwenguni pote hawana habari zozote kuhusu tisho linalohusianishwa na mwaka wa 2050.”

Hata hivyo, ni kosa kukata kauli kwamba hakuna hatari yoyote inayowakabili wanadamu au kwamba ni watu wanaodanganyika kwa urahisi ndio huamini kwamba mwisho wa dunia ni jambo hakika.

Je, kweli mwisho wa dunia utafika?

Ikiwa ndivyo, utafika lini na jinsi gani?
 

Kitikiti

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
353
250
Ukifa, ndio mwisho wako wa dunia. Simple.
Usipo mpokea YESU kama Bwana na Mwokozi wako ndio hautaokoka. Hii imeandikwa kwenye Biblia zetu na zenu. Ni mstari ambao hata mapadere na biongoze vengini wa dene wanapinga huku wakiiamini Biblia walioibeba.

Wengine usema huwezi kuishi bila dhambi au ki Utakatifu hapa duniani kama Mbinguni. Na hapohapo wanaijua na kuomba kwa kusema "Baba yetu uliye Mbinguni .....Ufalme wako uje hapa Duniani kama ilivyo Mbinguni". Yaani, wanaomba wasicho amini.
 

Lwasu

JF-Expert Member
May 31, 2015
744
1,000
Kama ilishindikana mwaka 2000 basi dunia haitakua na mwisho ss tutakufa na kuiacha dunia yetu!!!
 

elineema William

JF-Expert Member
May 2, 2015
577
500
Mmmh ifike tu coz kila nafsi itaonja mauti ......hal ya saiv hela hakuna n sawa na mwsho wa dunia coz mizunguko mingi ya hela hakuna
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom