Kwa kweli tuchukue tahadhari, huyu ni "malaika" asiye na huruma wala mzaha toka kitambo

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Huyu ni mtu mwenye kisasi na roho ngumu sana.Amekunywa damu ya mwana wa Saa8 na yule "SHIHATA" wa Kibiti.Hii imekuwa tabia yake,hajatosheka na kiwango cha bilauli za damu alizokwisha chota na kunywa.

Raha yake ilikuwa apate bilauli ya damu ya Lissu juu ya meza yake,ili anywe na kusuuzika roho,bahati mbaya damu ile imekuwa ngumu kuipata,ngamia amegoma kupiga goti ili achinjwe,sasa anataka kumchinja ngamia kwa shuruti,yupo radhi kunywa damu chungu ya ngamia inayotokana na ngamia kugoma kuchinjwa.Huyu ni mnywa damu,hajaanza jana wala juzi.Alianza na damu za familia,sasa amehamia kwenye damu za walio nje ya familia.

Mwaka 2005,Kaskazini Magharibi mwa Tanganyika,jimbo la Ziwa(LakeProvince),Mkoa wa Ziwa Magharibi (West-Lake Region)aligombea na kijana toka chama cha Upinzani.Aliona tishio la yeye kupata upinzani,yeye huwa hapendi kukosolewa wala kupigwa,ni mpenda sifa,hujiona kama malaika.Msifie utakuwa wake,mkosoe upasuliwe.Hii ni hulka yake iliyo ndani ya damu.

Hajaanza jana wala leo,2005 hakutaka tabu,alimtumia watu mgombea wa chama cha pili,akaagiza asafirishwe mpaka Makao Makuu ya Nyanza Province,pale akakatiwa tiketi ya Community Airline,wakati huo ipo juu ya ramani zaidi ya Kasuku aliyefurushwa kumpisha Twiga,breki ya kwanza ikawa bandari ya Salama,na moja kwa moja mpaka JB Belmond wakati huo.

Pale alihudumiwa kila kitu,kwa mpango kuwa aachie nafasi kupunguza ushindani,na hakika kwa zawadi ya kutunukiwa cheo kwa wakati ufaao.Huduma zote zilitoka kwa "Malaika",mkuu wa "watakatifu" na "wenyeheri" wasio na mawaa.Kipindi hicho makao ya "malaika" yalikuwa jengo moja na Kibubu cha Ushirika na Maendeleo Vijijini,mkabala na Mkaguzi na Kituo cha kujua lugha ya Hard-Talk ya Steve,pale kwenye jina la "God Made the World,The Dutch Made Holland".

Baada ya mchakato wa tume kupita,na "malaika" kuchukua ushindi wa team kutokufika uwanjani,walituma maafisa wa "kukodi" wa wakati huo Physics,Chemistry na Biology kabla ya kuongezewa C moja katikati,"Malaika" akamtengenezea mchezo mgombea kuwa anamuomba mlungula ili amuachie nafasi ya ukuu wa kitalu.

Hii ni baada ya kupita siku tatu,"malaika" anapigiwa simu bila kupokea maana alishamaliza kazi yake ya kupita bila kuwa na kizuizi cha ukuu wake.Kwa hiyo,huyu ni "malaika" ambaye hutumia mbinu zote ili kuhakikisha anadumisha ukuu wake,wakati akiwa bila majeshi ya mbingu na ardhi,alitumia nafasi na dinari,huyu hawezi kubadili hulka,iwe kwa fimbo au kwa rungu.

Ni aina ya "malaika" wasiotaka kugusika,ana sifa,kiburi na roho mbaya inayojificha katikati ya maneno ya uwongo na lugha za kutaka kuonekana ni wa watu wa chini.Ni hulka ya kisaikolojia mtu wa chini kuona anaambiwa anapendwa kuliko tajiri.Ni tabia za masikini wote duniani,masikini hupenda faraja tupu isiyo na mkakati,tajiri hupenda mkakati usio na faraja,ndio maana wale "interepirinuwaa" walikuja na msemo wakasema "An Interpreneur is a risk taker".

Ni kweli tulipenda kumpa ukuu wa himaya,na wengine hatukulala,usiku na mchana,maana tuliona ni ufadhali huyu kuliko yule mwenye unga kichwani.Tulijipa matumaini nankuchukua hatari kama kucheza bahati nasibu.Lakini,hapana,hakuna maendeleo bila amani na upendo,hakuna maendeleo yenye raha katikati ya chuki na visasi,maendeleo ndani ya zimwi la husuda na machozi ni sawa na nyumba nzuri yenye giza wakati wa mwanga.

Tunapokwenda ni mbali,sio tena salama kwa vizazi vyetu vijavyo.Mchonga alisurubu ndio,lakini hakufika huko,Mzee wa pwani alikuwa swala 5 sana,mengi alisema hewala,nitamaliza na kuondoka,Chinga mwanzo wake alikuwa muoga na kauli na jicho la mchonga,alipofukiwa Mchonga akakosa washauri,akaangukia kwa ambao mpaka kesho anawasikitikia.Handsome wetu hata wale wa mfumo walipomsaidia bila kumpa taarifa,aliwaambia waacheni hao,watasema watachok.Huyu "Malaika" anaagiza na kuomba kikombe na yeye aonje.Ni hatari sana.

Alipokumbwa na skendo ya kuuza mapango ya serikali kwa mipango ya kando na wadogoze,umalaika wake ukapungua nguvu,ikaonekana kuwa kumbe hata malaika wana tamaa kama biandamu.

Marehemu Gavana wa Makete na baadae Handeni akiwa mwandishi mkongwe wa gazeti moja pale Sinza Kijiweni aliandika mambo mengi ya kweli kumuhusu Malaika,kashfa nyingi ambazo mpaka leo zinaishi za malaika ziliwekwa peupe.

Malaika akaenda kituo cha polisi Mabatini,akafungua kesi kuwa marehemu anataka kumuuwa,kamtishia maisha,watu wakashangaa,malaika unatishiwaje kifo na binadamu??Binadamu akawekwa ndani baada ya polisi kurambishwa asalai ya nyika,siku kadhaa malaika haonekani kufuatilia kesi yake,lengo si kutishiwa bali kumnyamazisha binadamu asimseme malaika.

Hajaanza jana wala juzi,ndio maana wengi wanamuogopa,sababu hana mzaha.Ukibisha wewe kiongozi wa watunga sheria,anakuondoa kwa kutumia idadi ya vimalaika vipenda vyeo na pesa mle jengoni,na ili ulijue hilo,chini yako kakuwekea mtu ambaye kamteua kwa nguvu ya cheo chake cha umalaika mkuu.

Tunavunja misingi ya amani,tunavunja nguzoza upendo na amani.Tunaviziana,tunauwana,tunajeruhi na kutesa.Hatujaanza jana,roho hizi zina miaka mingi kati damu na jasho la watu.

Tunamtengeneza malaika mdogo,ili jae kulinda ya malaika mkuu,hata ile ya kusema natamani siku moja niwe kama malaika mkuu,na malaika mkuu kujibu kuwa ninapenda malaika mdogo siyo tu aje awe kama mimi,bali awe zaidi yangu,ni mpango mkakati wa malaika mkuuna malaika mdoo kuwaandaa watu kisaikilojia.

Tusikubali kugawanywa sababu ya udhaifu wa watu kulemewa na madaraka,hizi ni dalili kuwa kuna malaika tuliwapa madaraka bila wao kujiandaa,yamewazidi,hawana namna zaidi ya kutoa upanga wao alani na kucharanga bnadamu kama wanyama.Na hakika,kuna wakati wanatuaibisha,maana wanasema kazi hii ya umalaika mkuu,kwao ni mzigo,walikuwa wanabisha kwa kusabahi tu,lakini wamekaribishwa toka upenuni mpaka chumbani.Hawakutegemea!!

Amini,amini nawaambia...tunakwenda kubaya sana sana,fukuto la chuki na kisasi ni kubwa sana.Kanuni ya kimaumbile ya kumruhusu aliye na tumbo lenye gesi kupumua,ni kanuni hiyohiyo inaruhusu aliye na lake aseme na mwishowe atachoka au atapata ahueni .Kumziba mweye gesi kwa gunzi au kiwiko,ni kuruhusu gesi kupitia mahali pengine penye upenyo.

Nimepita huko na huko,nimeiona gesi ya chuki na malalamiko,si kwa sababu malaika hafanyi lolote,ila lolote analofanya linaweza kufunikwa na matendo yanayojenga sura ya ukatiri katikati ya watu.Ni sawa na dhana ya mashabiki kumshangilia na kumpa pole msakata kabumbu asiye na njumu dhidi ya yule emye njumu na ustadi wa mavazi uwanjani.Kanuni ya maisha ni huruma dhidi ya anaydhaniwa kuonewa.

Sisi wengine si malaika,lakini tunaona wapi malaika unaweza kuwa unakosea.Malaika anayehubiri upendo bila matendo,ni tafsiri ya malaika feki.Hata wafuasi wa malaika,kuna misingi iliyotukuza na kutulea tumeanza kuona inapotea na kumomonyoka.
 
Huyu mtu ni hatari sana!

Ni mtu popular kwa watu wenye sifa hizi:
1.Wenye uwezo mdogo wa kuona mbali
2.Wasiotazama mbali
3.Wenye uwezo mdogo wa kumsoma mtu
4.Wanaodanganyika na kupumbazwa na vitu vya kuonekana machoni
5.Wavivu wa kufikiri na wenye uwezo mdogo wa kupima kauli na matendo ya mtu.
6.Wanaoabudu watu kwa wadhifa au cheo na hawatazami matendo na dhamira ya muhisika.
7.Watu ambao sio wafuatiliaji wa mambo

Hawa watu wakuja kuelewa when it is already too late huku baadhi yao nao wakiwa teyari ni wahanga.
 
barafu nadhani una msongo wa mawazo! Unahitaji msaada
Mkubwa sana,hii siyo Mama Tanzania niliyokulia na kuishi.

Kuna mabadiliko makubwa sana ya kihisia katikati ya jamii na wanajamii.Kuna kakitu fulani ka chuki na tuhuma za chuki zinajengeka.

Kwa miaka mitatu niliyokuwa mbali,mabadiliko ni makubwa sana katikati ya watu wengi.

Usiishie kwenye gari binafsi,jipe muda na recorder yako,panda Mwendo Kasi ya jioni toka K'koo mpaka Kimara,rudi nayo Kkoo,panda kesho yake daladala za Kkoo-G'Mboto,tena panda Kkoo-Tandika...malizia na Kkoo Tegeta.Utapata hisia halisi ya Watanzani,kama una hulka ya utafiti,utarudi hapa na kusema bila unafiki.
 
Ha ha haaa...kitakachofanyika siku yakutua LISU ataokotwa Airport kukutanishwa na Joka lenye njaa....kitu watu tunatakiwa kujua waliomchagua huyu bwana na wapuuzi wanaomshangilia wanaboa hii Nch kumbuka hata ikitokea bahati mbaya akaondoka mamlakani atatuachia watu hatari sana!
Lakini mkuu barafu unadhani ngwe inayofuata yani 2020 timu hii itaruhusu mgombea wa chama kubwa la kinondoni agombe kitalu ambacho ni makazi yake?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uandishi wa makala unastahili 100% MARKS, ila kuhusu uhalisia wa ulichoongea sijui tukupe ngapi?.

Namaanisha tukiorodhesha madhambi ya maraisi wote watano waliotangulia kabla ya awamu hii madhambi yao kabla hawajawa Wakuu wa nchi hii, kiukweli wa sasa hivi anaweza kuwa MALAIKA kweli vinginevyo ujifanye hujui.

Kwenye zile mada zinazohusu mambo ya ndege na maswala ya anga ndo huwa unaongea ukweli tupu na kwa ile knowledge unayoonyeshaga hapa inaonekana wewe ni msafiri unayejua yanayoendelea ulimwenguni. Ulivyoelezea hapa leo ni as if Tanzania ya leo tupo Reo De Janeiro, Johannesburgh ,Columbia, California na miji mingine ambayo kwa siku ni kawaida wastani wa watu 6 hadi 8 hupigwa risasi au kupotea kila siku iendayo kwa Mungu.

JPM sio Mungu ana madhaifu yake ila hali halisi na hali mnayojaribu kuonyesha kwenye mitandao ni vitu viwili tofauti. Watu wanaendelea na maisha yao mitaani kama kawaida huku mitandaoni mkijitahidi kuelezea kama vile mnakufa usiku huu huu. Hakuna mtu anayepotea tu bila sababu, hata uswahilini watu wanapotea kwa kupotezana baada ya kudhulumiana pesa, kufumaniana au sababu zipo nyingi. Wengine waweza kuwa wanapotezwa na system kama unavyosema ila narudia hakuna mtu anapotea tu, lazima kuna kitu kakifanya.. Wewe mbona hujapotea upo hapa unabwabwaja maneno kibao ukiwa huru?, ni kwasababu umelelewa kwa nidhamu na unajua mipaka yako ndo maana hata kwenye huu uzi wako pamoja na maelezo yote bado umezingatia nidhamu,hujamtukana kiongozi yoyote wala kumkwaza mtu, ila upo hapa unatetea walopokaji hovyo huku ukieleza maelezo kibaoo eti hatupo salama???...

Ni kama yule jamaa yenu jana alikuwa BBC.. ana akili nyingi za darasani lakini kuna elimu inaitwa ELIMU DUNIA, kichwani mwake ni 00% ndo maana dunia inamfundisha ukubwani.Atazunguka duniani koote mwisho wa siku atarudi nyumbani na atajiona mjinga tu.Ila kanuni za kidunia zipo na zinafanya kazi. Na kuna kitu anaendelea kukitafuta muda sio mrefu atakipata iwe nchini au hukohuko aliko.

Nimalize kwa kukwambia TANZANIA bado ni mahali salama sana,tena zamu hii hata zile bunduki ndogo kwa kubwa ndugu zetu walikuwa wakionyeshwa ili watoe hata laki 2 mapema kweupe kwenye mabanda ya tigopesa siku hizi zimepotezwa kabisa, hadi wale wanasiasa waongo waongo wapo bize majimboni.

Endeleeni kuimba nyimbo za uongo ila TUKUTANE 2020 ndo utajua kama JPM anapendwa na wananchi wake au LA.

Mkuu BARAFU hizi CHEAP(politics) propaganda waachie akina SALARY SLP & CO.LTD,. wewe uelewa wako ni mpana zaidi ya hapo.Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom