Kwa Kuzingatia KATIBA ya Chama Na -MAADILI ya Uanachama Na Uongozi Wa Chama-Zitto Na

wewe nimekuzoea, hata madaraka uliandika hatuwezi kumvua na kamati kuu ikamvua sauti ya wengi ni sauti ya mungu na hata uanachama tutamfuta, poor zzk

Sipendi mnapomtaja Mungu kwa kufurahia udharimu. Jipambeni muwezavyo lakini msimtaje Mungu kama dhihaka, Mungu ana heshima ya pekee.
 
ZITO -Rudi nyuma Shetani weee maana huyawazi yaliyo mapenzi ya Mungu.UNAHONGEKA KIRAHISI HIVYO WAKATI HATA SUTI YA KWANZA KUIVAA IMETOKA CHADEMA KWA HUYO UNAYEMWONA HAFAI SASA;Kwa kosa hili hakika unastahili kufukuzwa haraka sana. UBAHATI UNGEKUKUWA CHINA UNGENYONGWA MCHANA KWEUPE.
 
Toka avuliwe madaraka ndani ya chama mh ZITTO, kwa tuhuma ambazo kimsingi ilibidi avuliwe uanachama, hali imekuwa tete sana.

Chadema lazima wajue kwamba athari za kumvua Mh zito madaraka yake yote ndani ya chama na kumuacha kuendelea kuwa mwanachama ni kama kukaa na TIME BOMB ndani ya nyumba yako.

Kwanza, Muhusika ameonyesha kupinga maamuzi ya kikao halali kilicho muadhibu hivyo anajenga tension kwa wanachama na pia malumbano ndani ya chama yasiyo na tija. Hali hii inadhoofisha chama kiasi cha kusikitisha. Huwezi kupanga mikakati yeyote kama una makundi yasiyokubaliana tena kwa makusudi. Lakini kama ZITTO angetimuliwa chadema wanachama wangebaki na choice mbili tu. Either kumfuata zitto kokote atakapoenda or kubaki chadema na kuendeleza gurudumu la maendeleo.

Pili, Ma ccm pia wamepata nafasi ya kutumia mapandikizi kukidhoofisha na kukihujumu chama, Wanahonga watu kuigiza kuwa ni wana chadema ili watoe matamko feki, watukane viongozi, waharibu mali za chama, na ku organise maandamano feki kabisa. Kama nilivyosema awali kwa makosa ya Zitto , hastahili kuendelea hata kuwa mshabiki wa chadema sii tu mwanachama. kuendelea kwake kubaki CHADEMA ndo kunatoa nafasi hii kwa ndugu zake maCCM, na hili ni ushindi kwake na wapambe zake (WAASI). Lakini kama zitto angetimuliwa mara moja maCCM wasingepata nafasii hii ya kuweka mapandikizi. Labda wangekuwa wanashangilia kujiunga kwa zitto ccm, nna Chadema ingeendelea na mipango yake kama kawaida

Mwisho, si kweli kwamba vijana wengi walio chadema walivutwa na Zitto, Naamini vijana walio chadema ni wasomi na si lahisi kumfuata mtu bali "POLICY" safi za CDM. Lakini as far as Zito bado yupo ndani ya chama katika wakati huu, anapotosha ukweli wa mambo na kuwafanya wanasiasa wachanga hasa wale wanaotaka kuingia katika vyama kuwa katika Dilemma. Na pia kukosa imani na misingi ya chama hasa ukizingatia kuwa zitto anadanganya kuwa vijana waliingia katika chama kumfuata yeye binafsi.

Ili kuepusha hujuma, migongano ya kupandikiza, na taharuki hata kwa wanachama safi, Zitto na wenzie wavuliwe uana chama ndani ya CHADEMA immediately ili anayemtaka zitto ajiondoe mapema na kuwaacha wanachadema SAFI tukijenga chama na kijiandaa kuchukua nchi. Kumuacha zitto ndani ya chama kwa kipindi hiki ni hatari hata kuliko athari za walaka wa uasi walio uandaa na ni ushindi kwa wabaya wa chama kwani wanapata muda wa kukihujumu chama.

ASANTENI

Hoja safi sana Mkuu, kwa kosa la usaliti kwa kweli hawa wasaliti hawakustahili kupata hata muda Wa kujitetea.

Walistahili summary dismissal
 
Wachagga wanavyopenda pesa, hawawezi kumfukuza huyo, waikose ruzuku ya jimbo lake?

Ingekuwa kumfukuza wangemfukuza Shibuda anaewapakia waziwazi.

Naona wewe ukabila umekujaa Na chuki dhidi ya wachaga imekujaa rohoni mwako. Naona nyie huko CCM wachaga Na Watu wote Wa kaskazini hatimaye mtawafukuza wote
 
Kwanini haya yanatokea kila tunapokaribia uchaguzi mkuu?jana wangwe,leo zito kesho nani?

Kwa hiyo ulitaka waachwe tu kisa uchaguzi umekaribia? kumbuka waraka wao unataka kupanga mikakati ya kupanga safu kwa kuwanunua watu kwa msaada wa maccm kinyume cha kanuni za CDM.utaratibu wa matumizi ya fedha kupanga safu za uongozi na wa magamba na kamwe CDM haiwezi kuruhusu upumbafu kama huu.napendekeza zitto afukuzwe tena haraka pamoja na mamluki wenzie.CDM 4 LIFE
 
Kwa hiyo ulitaka waachwe tu kisa uchaguzi umekaribia? kumbuka waraka wao unataka kupanga mikakati ya kupanga safu kwa kuwanunua watu kwa msaada wa maccm kinyume cha kanuni za CDM.utaratibu wa matumizi ya fedha kupanga safu za uongozi na wa magamba na kamwe CDM haiwezi kuruhusu upumbafu kama huu.napendekeza zitto afukuzwe tena haraka pamoja na mamluki wenzie.CDM 4 LIFE

Sawa kabisa kamanda, kwa uhai Na afya njema ya chama lazima wasaliti wote wafukuzwe bila kujali nyadhifa zao
 
Kuna siku nilimrudisha kwao ghafla house girl wangu, matokeo yake ni kwamba asubuhi nilishangaa jirani yangu analia huku akiongea maneno ambayo kama vile yananihusu. Nilivyokuja kuchunguza, niligundua kwamba kuondoka kwa yule house girl kulitibua mipango mibaya juu yangu iliyokuwa inafanywa na yule jirani akimtumia house girl yule, na mbaya zaidi yule house girl alikuwa amekopeshwa hela na huyo jirani. Usishangae wanaolalamika kuvuliwa madaraka ya huyu mheshimiwa ni maCCM pamoja na wale madogo waliofukuzwa CHADEMA. Mipango imevurugika, hela imetumika lakini ilikuwa bado haijarudisha return
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom