Kwa Kuzingatia KATIBA ya Chama Na -MAADILI ya Uanachama Na Uongozi Wa Chama-Zitto Na

Lissu kasema Waraka Original wa kina Mkumbo haujatoka wewe umeutoa wapi nasi tuusome then tu Comment?

Inawezekana wasaliti walikuwa Na nyaraka zaidi ya 1, tumeona waraka mmoja ambao uko humu kwenye mtandao. Na huo waraka ndio tunaoujadili. Ukisha usoma huo waraka ndio sasa usome huu Uzi utanielewa
 
CHADEMA watake wasitake Zitto ni mtu hatari sana katika uhai wa chama chao. Sisi wana CCM ambao tuko mbali na makao makuu ingelikuwa vyema mkatutambulisha kuwa huyu ni nani yetu chamani. Huku vijijini hata ukiwa kwenye vikao vya kahawa watu washamstukia zamani sana {hata CCM tunalijua hili}. Mimi ktk hili naogozwa na imani yangu ya kidini kuwa siwezi kusema kile nisichokiamini toka moyoni,ZITTO ni msaliti tena hatari sana hata tukimpokea CCM. Mimi ningependa sana vijana wa CCM tulioko humu Jf tuleteni hoja za kujenga chama chetu, ya CDM tuwaachieni wao {udini sijui ukabila mambo ambayo siyaamini kabisa}. Nawapa mfn; huku kanda ya ziwa hata kama uchaguzi mkuu ukiitishwa leo Lowassa ataibuka mshindi na si Magufuri,huku hatuendeshwi na ukabila,ukanda au udini. Nani asiyefaham kama Zitto amejikita kwenye ukanda,ukabila na udini? Halafu tuacheni kuhubiri udini hauna tija ktk taifa hili. Kauli za viongozi waandamizi ndani ya chama kuwa CDM ni ya wakristu zinaijenga CHADEMA na kutusononesha hata sisi wakristu tulioko CCM. Naomba sana wana CCM mliostaarabika tumuunge mkono mh. January Makamba kwani ni kijana mwenye muonekano tofauti sana na baadhi ya viongozi wakubwa serikalini,ni mgodi utembeao,hongereni wana Bumburi. January ana kauli za kuwaleta pamoja watanzania na si kuwatenganisha,namfananisha na rais msitaafu Mwinyi.

Hapa nakugongea 'LIKE' Mkuu. We ni CCM lakini Umesema ukweli kabisa
 
Tuko pamoja mkuu! The earlier the better, or never! Watimuliwe tukabiliani na changamoto hii ya muda mfupi lakini yenye kukijenga chama na kukiimarisha katika msingi wa haki,uadilifu na kujiamini katika kutoa maamuzi na kuyasimamia kwa maslahi ya nchi.Hayo ndio maandalizi ya kuingia IKULU! cdm forever!

Safi sana Mkuu; Pamoja Daima
 
Moja ya maandiko murua sana ndani ya jf,

Ninaiamini kamati kuu ina watu makini sana,

Kumwacha Zitto ndani ya chadema ni sawa na daktari kuacha mkasi tumboni mwa mgonjwa baada ya kumaliza oparesheni
 
Zitto ndo Mastermind wa Mkakati Mzima, hili halina ubishi, ingawa amejitahidi sana kutacha aushahidi katika kutekeleza kwake Mpango Haramu, lakini haihitaji Degree kulijua hili.
Zitto asipovuliwa uanachama wana CHADEMA wengi sana tutakuwa hatujateendewa haki
 
Moja ya maandiko murua sana ndani ya jf,

Ninaiamini kamati kuu ina watu makini sana,

Kumwacha Zitto ndani ya chadema ni sawa na daktari kuacha mkasi tumboni mwa mgonjwa baada ya kumaliza oparesheni

Asante sana Mkuu, Zitto ni mtu hatari sana, unfortunately si Kama jinsi anavyoonekana publicly
 
Lissu kasema Waraka Original wa kina Mkumbo haujatoka wewe umeutoa wapi nasi tuusome then tu Comment?

Huwezi kutajwa kuwa mhusika mkuu (mm) ktk mkakati ambao huujui. Zitto Kabwe anajua kila kitu ndiyo maana alikuwa akigawa zile fedha kwa wasaliti wenzake. Bahati mbaya sana kwake hakujua kama mpango wote ungejulikana kabla ya kutekelezwa. Shame on him. Mwingulu alimtetea Zitto akisema ni msomi, mchapa kazi na mwimarishaji wa cham. Mwingulu huyu huyu ndiye alisema Chadema ni adui yake namba 2 baada ya shetani. Sasa kwanini asimchukue Zitto ampeleke CCM ili Chadema isambaratike!? Kama kufukuzwa Zitto ni kuharibikiwa kwa Chadema, kwanini anahuzunika? Shame on him.
 
Mkuu blueray umenena kweli huyu aslelewe afukuzwe awafuate wafadhiri wake, apokelewe na Wasira, Mwigulu, Nape na Kinana!!
The failed Wasira projects versas CDM!!
 
Last edited by a moderator:
gambala nyoka umesahau hata wale waluofukuzwa kina Shonza, Mtela & CO walisema Boss wao alikuwa ni Zito!! It was a matter of time tuu!! CDM kuna Mungu amewekwa hadharani msaliti mkuu sasa anatapatapa!!
Zito By by salimia Mwigulu na Nape!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu blueray umenena kweli huyu aslelewe afukuzwe awafuate wafadhiri wake, apokelewe na Wasira, Mwigulu, Nape na Kinana!!
The failed Wasira projects versas CDM!!

Sasa hivi kina Nchemba, Wasira na Nape wamechanganyikiwa. Bomu Lao limewalipukia
 
Last edited by a moderator:
Kwa waliosoma vizuri mkakati Wa siri (conspiracy) Wa Zitto na wenzake Samson Mwigamba, Kitila Mkumbo na 'M' watakubaliana nami -pasi shaka yeyote kuwa huu ni mkakati wa Uhaini ndani ya chama. Huu mkakati ulikuwa Na lengo la -kuanzisha uasi ndani ya chama. Ushahidi wote pamoja na wa kimazingira unaonyesha kuwa -muasisi wake na mhusika mkuu wa haya mapinduzi ni Zitto. Ni mjinga tu awezaye kuamini mapinduzi yanaweza kupangwa bila mhusika Mkuu kufahamu.

Utetezi wa Zitto kusema hahusiki Na Mipango ya usaliti, ambayo ingeishia kwenye mapinduzi, -wakati ye ndiye mhusika mkuu ni -dharau kubwa kwa viongozi wa Chadema, wanachama na wananchi wote wa Tanzania wanaopenda haki na kutaka mabadiliko ya kweli -kwa ajili ya maendeleo.

Zitto ameonyesha dharau kubwa kwa kufikiria kwamba yeye ni mwelevu na viongozi wote wa chadema, wanachama -na watanzania wote ni vilaza na hawawezi kuelewa kwamba siku zote kinara wa mapinduzi hufichwa kama alivyofichwa yeye ingawa sasa keshabainika.

Kwa ufupi huu mkakati -ni mkakati wa siri (conspiracy) -unaopanga njama za kuondosha viongozi wote Wa chama katika ngazi zote kuanzia ngazi za Chini hadi taifa na kuweka viongozi wenye ufuasi -kwa mtu mmoja-yaani Zitto Kambwe.-Huu ni mpango wa siri ambao umekiuka taratibu zote za kidemokrasia.

Huu ni mkakati wa Uhaini ndani ya chama na si mkakati wa kidemokrasia au kukuza demokrasia ndani ya chama kama inavyodaiwa na wahusika. Huu ni mkakati unaokiuka misingi yote na taratibu zote za kidemokrasia. Ni mkakati unaoua demokrasia Na kuanzisha mfumo wa kidikteta unaofuata maelekezo ya mtu mmoja-Zitto ambaye ndiye angekuwa amewaweka hao vibaraka anaowataka katika ngazi mbali mbali-hii si demokrasia.

Kibaya zaidi ni unapoona mashabiki wa huu mkakati asilimia zaidi ya 99 ni wana CCM na watu ambao wamefukuzwa Chadema kwa kosa la usaliti.

Utetezi wa zitto na wahaini wenzake kwamba lengo lao lilikuwa kutumia demokrasia ndani ya chama ni kejeli kwa mana Chadema Kwani -Demokrasia haianzi Na uwepo wa mwenyekiti ambaye tayari amekwishajichagua na anatumia uchaguzi kujihalalisha. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia ambayo Zitto mwenyewe anadai kuipigania ndani ya chama.

Yumkini kabisa hata ushawishi wa wafuasi ambao Zitto angeshawishi wamfuate ungekuwa ni kwa kutumia hila na pesa. Ingawa hili halijaelezwa -moja kwa moja kwenye waraka lakini ni dhahiri Kwani hata wale viongozi wake Wa kitaifa wanaahidiwa kupewa milioni2 kila mmoja ili waanzishe miradi Na wajitosheleze kifamilia (ingawa siamini pesa halisi ambazo wangepewa ili wajitegemee ingalikuwa milioni hizo 2). Pia huu mkakati unatoa jukumu la 'kutafuta' Pesa ili kufanikisha njama. 'Kutafuta' ni neno lililotumika makusudi kwani hii njama tayari ina wafadhili na ukitaka kuwajuwa wafadhili angalia 'wanaoomboleza' kwa kulia sana wakati hawana undugu hata wa chembe.

Mkakati -huu umeandikwa kwa mafumbo sana na 'cleverly' umekwepa kuonyesha kwamba hiki kikundi tayari kina pesa nyingi Au kimeahidiwa kupewa pesa kwa ajili ya mapinduzi haya. Pia 'cleverly' waandishi Wa mkakati huu wa uhaini wamekwepa kwa makusudi kuonyesha kuwa Zitto ndiye 'mastermind' Wa mapinduzi haya in case mpango wa usaliti ungevuja Au kunaswa. Mkakati wa Mapinduzi usingeweza kuanzishwa bila mawasiliano ya awali Na makubaliano ( yaani 'Memorandum of Understanding') kati ya mhusika mkuu ambaye ni Zitto Kabwe -kina 'M'.

Hitimisho langu ni kwamba Zitto na viongozi wengine na hata wanachama ambao ni wasaliti lazima wafukuzwe wote na kunyang'anywa uanachama. Hakuna katiba inayoruhusu usaliti ndani ya chama Na vile vile hakuna maadili ya chama chochote yanayoruhusu usaliti au Uhaini ndani ya chama.

Zitto akifukuzwa uanachama sasa hivi chama kitapata madhara lakini kwa kiasi kidogo sana kwani mabomu yaliyoandaliwa na Zitto kuua Chadema -yatalipuka kabla ya kutegwa (prematurely) na hivyo kutokuwa na madhara makubwa. Hii sababu ndio inafanya wafadhili wa huu mpango kulia kuliko 'wafiwa'

Chadema ikisubiri kumfukuza baadae Au asipofukuzwa madhara yatakuwa makubwa zaidi. Atakuwa ameshawishi viongozi wengi zaidi na wanachama wengi zaidi kwa kutumia platform hii hii ya CHADEMA. Wakati huo chama hakitakuwa na muda wa kuwaeleza wanachama ukweli.-

Ataendelea kuvuruga chama na hasa kwenye chaguzi za chama. chaguzi za serikali za mitaa na kwenye uchaguzi mkuu.

Hivyo chama -kina uchaguzi; kuwafukuza kabisa sasa hivi Zitto pamoja na wasaliti wote ili kupoteza -kidogo Au kumwacha Zitto na wasaliti waendelee kuwa ndani ya chama ili-hatima yake iwe ni madhara makubwa kwa chama hapo baadae.-

Napenda nitahadhalishe viongozi wa Chadema, wanachama Na wapenzi wote Wa Chadema kwamba mhaini au msaliti yeyote anapothibitika moja kwa moja au kwa ushahidi wa mazingira hana tena utetezi. Kilichobaki ni kufuata taratibu za kikatiba na kuwaondosha wasaliti wote bila kujali nyadhifa zao ndani ya chama.

Na Kama Zitto ameweza kusaliti chama chake anachodai kimemlea tangu akiwa na miaka 16 hadi sasa amekuwa mwanasiasa anayefahamika nini kitamzuia kuuza nchi Kama atapata nafasi ya kuongoza nchi? Kwa sababu hii kiongozi yeyote Anayeweza kujiingiza kwenye Mipango ya usaliti na mapinduzi hafai kuaminiwa Na jamii yoyote.-

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema.

hivi hii mijadala katibu wetu mkuu si ameshaifunga??? au wale wa kumponda Zitto ndio ruhusa kuendelea ila wanaomuunga mkno zitto si ruhusa??? alafu na wewe si sehemu ya utekelezaji wa mkakati mwingine wa siri kuhakikisha mbowe anaendelea kuwa mwenyekiti wetu??? hivi nani asiyejua kuwa kuchafuliwa kwa zitto mitandaoni na ile ripoti ya siri ni sehemu ya mkakati mwingine???? kulikoni mambo haya mwayatazama kwa jicho moja tu na lenye kubeba sura ya ubaguzi?? tubadilike na tujenge chama chetu,,,tuache huu upuuzi,,,wa kuchafuana,,,coz mmeshagundua kuwa waraka haumtaji zitto kuhusika na wandaaji wamekana uhusika wa zitto sasa mnatumia nguvu kubwa kuhakikisha zitto anahusika..hivi kwanini mnatumia nguvu kubwa katika kutaka mbowe anaendelea kuwa mwenyekiti? kwanini tusiache wapiga kura waamue???
 
Zitto ndo Mastermind wa Mkakati Mzima, hili halina ubishi, ingawa amejitahidi sana kutacha aushahidi katika kutekeleza kwake Mpango Haramu, lakini haihitaji Degree kulijua hili.
Zitto asipovuliwa uanachama wana CHADEMA wengi sana tutakuwa hatujateendewa haki

huu nao ni mkakati mwingine...
 
Ni ushahidi gani wa kwamba Zitto anauhusika na ule waraka?.
Kitila na Mwigamba wametoa testimony kwamba Zitto hahusiki na ule waraka, ni jukumu la wale wanaodai anahusika walete ushahidi.

By the way tundu Lissu na Mnyika walisema ule waraka tuliousoma kwenye mtandao ni fake, SASA NI VIPI UMHUKUMU ZITTO KWA WARAKA FAKE, SI UNGESUBIRI UKAPEWA AMBAO NI GENUINE ILI UJENGE HOJA YAKO?.

BINAFSI NAONA ZAITTO HANA KOSA, BALI NI HOFU YA MBOWE TU KUPATA MSHINDANI CREDIBLE KATIKA UENYEKITI WA CHADEMA
DR. Kitila anatufanya watanzania wote ni wajinga kiasi cha kutojua hata logic zenye arguments
rahisi kiasi hicho- Mimi nafikiri hawa jamaa wote wameonyesha dharau mbaya sana kwa wana CHADEMA.
 
gambala nyoka umesahau hata wale waluofukuzwa kina Shonza, Mtela & CO walisema Boss wao alikuwa ni Zito!! It was a matter of time tuu!! CDM kuna Mungu amewekwa hadharani msaliti mkuu sasa anatapatapa!!
Zito By by salimia Mwigulu na Nape!!
Zitto kwisha habari yake!! Miaka miwili iliyobakia Ubunge wa mahakamani -- teh teh teh
 
Sikuwahi na sitamkubali ZZK ata siku moja ni mbinafsi saana briefly ZITTO SHOULD BE PERISHED AWAY.
 
Hivi mkuu FUSO siku 14 bado tu tumscan huyu kirusi malware?

Zitto kwisha habari yake!! Miaka miwili iliyobakia Ubunge wa mahakamani -- teh teh teh
 
Last edited by a moderator:
DR. Kitila anatufanya watanzania wote ni wajinga kiasi cha kutojua hata logic zenye arguments
rahisi kiasi hicho- Mimi nafikiri hawa jamaa wote wameonyesha dharau mbaya sana kwa wana CHADEMA.

Dr Kitila ametufanya wajinga kivipi?- TANGU LINI DHANA ISIYOBEBWA NA USHAHIDI IKASIMAMA KA USHAHIDI WENYEWE?
 
Usimshirikishe Mwenyezi kwenye mambo ya kijinga. Mpango wa Zitto unaweza pia ukawa ni wa Muumba kama ni wa haki. Mola anaangalia haki na hana upendeleo.

Mchukueni awe mwenyekiti kwenye chama chenu atekeleze hiyo mikakati huko. Kwanini mnang'ang'ania abaki Chadema wakati hatumtaki?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom