Kwa Kuzingatia KATIBA ya Chama Na -MAADILI ya Uanachama Na Uongozi Wa Chama-Zitto Na

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
423
Kwa waliosoma vizuri mkakati Wa siri (conspiracy) Wa Zitto na wenzake Samson Mwigamba, Kitila Mkumbo na 'M' watakubaliana nami -pasi shaka yeyote kuwa huu ni mkakati wa Uhaini ndani ya chama. Huu mkakati ulikuwa Na lengo la -kuanzisha uasi ndani ya chama. Ushahidi wote pamoja na wa kimazingira unaonyesha kuwa -muasisi wake na mhusika mkuu wa haya mapinduzi ni Zitto. Ni mjinga tu awezaye kuamini mapinduzi yanaweza kupangwa bila mhusika Mkuu kufahamu.

Utetezi wa Zitto kusema hahusiki Na Mipango ya usaliti, ambayo ingeishia kwenye mapinduzi, -wakati ye ndiye mhusika mkuu ni -dharau kubwa kwa viongozi wa Chadema, wanachama na wananchi wote wa Tanzania wanaopenda haki na kutaka mabadiliko ya kweli -kwa ajili ya maendeleo.

Zitto ameonyesha dharau kubwa kwa kufikiria kwamba yeye ni mwelevu na viongozi wote wa chadema, wanachama -na watanzania wote ni vilaza na hawawezi kuelewa kwamba siku zote kinara wa mapinduzi hufichwa kama alivyofichwa yeye ingawa sasa keshabainika.

Kwa ufupi huu mkakati -ni mkakati wa siri (conspiracy) -unaopanga njama za kuondosha viongozi wote Wa chama katika ngazi zote kuanzia ngazi za Chini hadi taifa na kuweka viongozi wenye ufuasi -kwa mtu mmoja-yaani Zitto Kambwe.-Huu ni mpango wa siri ambao umekiuka taratibu zote za kidemokrasia.

Huu ni mkakati wa Uhaini ndani ya chama na si mkakati wa kidemokrasia au kukuza demokrasia ndani ya chama kama inavyodaiwa na wahusika. Huu ni mkakati unaokiuka misingi yote na taratibu zote za kidemokrasia. Ni mkakati unaoua demokrasia Na kuanzisha mfumo wa kidikteta unaofuata maelekezo ya mtu mmoja-Zitto ambaye ndiye angekuwa amewaweka hao vibaraka anaowataka katika ngazi mbali mbali-hii si demokrasia.

Kibaya zaidi ni unapoona mashabiki wa huu mkakati asilimia zaidi ya 99 ni wana CCM na watu ambao wamefukuzwa Chadema kwa kosa la usaliti.

Utetezi wa zitto na wahaini wenzake kwamba lengo lao lilikuwa kutumia demokrasia ndani ya chama ni kejeli kwa mana Chadema Kwani -Demokrasia haianzi Na uwepo wa mwenyekiti ambaye tayari amekwishajichagua na anatumia uchaguzi kujihalalisha. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia ambayo Zitto mwenyewe anadai kuipigania ndani ya chama.

Yumkini kabisa hata ushawishi wa wafuasi ambao Zitto angeshawishi wamfuate ungekuwa ni kwa kutumia hila na pesa. Ingawa hili halijaelezwa -moja kwa moja kwenye waraka lakini ni dhahiri Kwani hata wale viongozi wake Wa kitaifa wanaahidiwa kupewa milioni2 kila mmoja ili waanzishe miradi Na wajitosheleze kifamilia (ingawa siamini pesa halisi ambazo wangepewa ili wajitegemee ingalikuwa milioni hizo 2). Pia huu mkakati unatoa jukumu la 'kutafuta' Pesa ili kufanikisha njama. 'Kutafuta' ni neno lililotumika makusudi kwani hii njama tayari ina wafadhili na ukitaka kuwajuwa wafadhili angalia 'wanaoomboleza' kwa kulia sana wakati hawana undugu hata wa chembe.

Mkakati -huu umeandikwa kwa mafumbo sana na 'cleverly' umekwepa kuonyesha kwamba hiki kikundi tayari kina pesa nyingi Au kimeahidiwa kupewa pesa kwa ajili ya mapinduzi haya. Pia 'cleverly' waandishi Wa mkakati huu wa uhaini wamekwepa kwa makusudi kuonyesha kuwa Zitto ndiye 'mastermind' Wa mapinduzi haya in case mpango wa usaliti ungevuja Au kunaswa. Mkakati wa Mapinduzi usingeweza kuanzishwa bila mawasiliano ya awali Na makubaliano ( yaani 'Memorandum of Understanding') kati ya mhusika mkuu ambaye ni Zitto Kabwe -kina 'M'.

Hitimisho langu ni kwamba Zitto na viongozi wengine na hata wanachama ambao ni wasaliti lazima wafukuzwe wote na kunyang'anywa uanachama. Hakuna katiba inayoruhusu usaliti ndani ya chama Na vile vile hakuna maadili ya chama chochote yanayoruhusu usaliti au Uhaini ndani ya chama.

Zitto akifukuzwa uanachama sasa hivi chama kitapata madhara lakini kwa kiasi kidogo sana kwani mabomu yaliyoandaliwa na Zitto kuua Chadema -yatalipuka kabla ya kutegwa (prematurely) na hivyo kutokuwa na madhara makubwa. Hii sababu ndio inafanya wafadhili wa huu mpango kulia kuliko 'wafiwa'

Chadema ikisubiri kumfukuza baadae Au asipofukuzwa madhara yatakuwa makubwa zaidi. Atakuwa ameshawishi viongozi wengi zaidi na wanachama wengi zaidi kwa kutumia platform hii hii ya CHADEMA. Wakati huo chama hakitakuwa na muda wa kuwaeleza wanachama ukweli.-

Ataendelea kuvuruga chama na hasa kwenye chaguzi za chama. chaguzi za serikali za mitaa na kwenye uchaguzi mkuu.

Hivyo chama -kina uchaguzi; kuwafukuza kabisa sasa hivi Zitto pamoja na wasaliti wote ili kupoteza -kidogo Au kumwacha Zitto na wasaliti waendelee kuwa ndani ya chama ili-hatima yake iwe ni madhara makubwa kwa chama hapo baadae.-

Napenda nitahadhalishe viongozi wa Chadema, wanachama Na wapenzi wote Wa Chadema kwamba mhaini au msaliti yeyote anapothibitika moja kwa moja au kwa ushahidi wa mazingira hana tena utetezi. Kilichobaki ni kufuata taratibu za kikatiba na kuwaondosha wasaliti wote bila kujali nyadhifa zao ndani ya chama.

Na Kama Zitto ameweza kusaliti chama chake anachodai kimemlea tangu akiwa na miaka 16 hadi sasa amekuwa mwanasiasa anayefahamika nini kitamzuia kuuza nchi Kama atapata nafasi ya kuongoza nchi? Kwa sababu hii kiongozi yeyote Anayeweza kujiingiza kwenye Mipango ya usaliti na mapinduzi hafai kuaminiwa Na jamii yoyote.-

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema.
 
Hivi demokrasia gani ya kijichagu kuwa mwenyekiti. Na huyo anaye jiita dr. Mkumbo anafundisha chuo che hadhi?
Nakubaliana sana na mwandishi. Ukitaka kujuausaliti unaona wanao watetea hao waasi hawana tofauti na M23.
Ili chama kifanye vizuri lazima kiwatimue vibaraka wote
 
chadema mpango wa MUNGU haiwezekani leo hukawa mpango wa Zito .
 
Tumechoshwa na kelele Zenu si mwafukuze sasa mbona kelele nyingi.
 
Hivi demokrasia gani ya kijichagu kuwa mwenyekiti. Na huyo anaye jiita dr. Mkumbo anafundisha chuo che hadhi?
Nakubaliana sana na mwandishi. Ukitaka kujuausaliti unaona wanao watetea hao waasi hawana tofauti na M23.
Ili chama kifanye vizuri lazima kiwatimue vibaraka wote

Kweli kabisa Mkuu lazima vibaraka wote wang'olewe Na sisi wanachama wote tuunge mkono kwa hatua wanazochukua viongozi za kusafisha Masalia
 
Kwa waliosoma vizuri mkakati Wa siri (conspiracy) ...................ameweza kusaliti chama chake anachodai kimemlea tangu akiwa na miaka 16 hadi sasa amekuwa mwanasiasa anayefahamika nini kitamzuia kuuza nchi Kama atapata nafasi ya kuongoza nchi? .......
.
Hapa ndipo kwa sie tuanotizama UTAIFA uwa nasikia kama NIPASUKE ila naamini msemo huu wa kukopa toka jumba la cimea Marikani kuwa SHARK ARE BORN SWIM,ndio hivyo tena ITAKUWA NGUMU.
 
kamanda , kwa sasa hakuna namna yoyote ya zitto kuendelea kuwa mwanachama .

Ni kweli kabisa Mkuu, ila ni vizuri wanachama Na baadhi ya viongozi wasioelewa au ambao bado wanarubunika sababu za Zito kufukuzwa nao waelewe ili tuwe pamoja
 
naunga mkono hoja 100%

Uamuzi wa kumtimua Zitto uongozi na uanachama umechelewa sana. Ulipaswa uamuzi huo uwe umetekelezwa kabla ya Septemba mwaka huu. Yote niliyosoma, pamoja na zile hoja za Zitto, zinanifanya nihitimishe kuwa yeye ni msaliti tu. Sijashawishika vinginevyo.
 
Uamuzi wa kumtimua Zitto uongozi na uanachama umechelewa sana. Ulipaswa uamuzi huo uwe umetekelezwa kabla ya Septemba mwaka huu. Yote niliyosoma, pamoja na zile hoja za Zitto, zinanifanya nihitimishe kuwa yeye ni msaliti tu. Sijashawishika vinginevyo.

Zitto ni mjanja sana amejitahidi sana kutoacha ushahidi kwenye usaliti lakini this time amepatikana!
 
Zito ni msaliti tu full stop!!!
Sitaki kuamini kwamb zito ambaye ni mwelewa sana wa mambo ya democrasia na anayedai demokrasia ndani ya chama awe ndo mwandaaji mkuu wa mapinduzi kwa uongozi uliopo na bila kufuata taratibu zinazotakiwa et ndio demokrasia!
Sitaki kusikia zito akidai hahusiki wakti wenzake wamekiri kuwa yeye ndio mhusika mkuu ambaye anaandaliwa at the same time wanamkinga et hajui km yeye ndiye anayeandaliwa, haihitaji kuingia darasani kwa kweli!
Kama ataachiwa uanachama lazima akiri kuwa ni upendeleo wa pekee ambao asingestahili kabisa!
 
Zito ni msaliti tu full stop!!!
Sitaki kuamini kwamb zito ambaye ni mwelewa sana wa mambo ya democrasia na anayedai demokrasia ndani ya chama awe ndo mwandaaji mkuu wa mapinduzi kwa uongozi uliopo na bila kufuata taratibu zinazotakiwa et ndio demokrasia!
Sitaki kusikia zito akidai hahusiki wakti wenzake wamekiri kuwa yeye ndio mhusika mkuu ambaye anaandaliwa at the same time wanamkinga et hajui km yeye ndiye anayeandaliwa, haihitaji kuingia darasani kwa kweli!
Kama ataachiwa uanachama lazima akiri kuwa ni upendeleo wa pekee ambao asingestahili kabisa!

Mkuu uko sahihi kabisa Na Zitto hastahiki hata kubaki kuwa mwanachama tu Wa Chadema. Huyu ni msaliti Mkuu aondoke arudi kwa wanaomtuma
 
ULINZi wa kwanza wa MTU ni Akili

Niliona lile andishi, na nimerudia tena na tena kulisoma . HIYO TAASISI kingepasuka vipande vipande kama viongozi wasingeunasa Na K UCHUKUA HATUA
 

Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom