Kwa Kuzingatia AFYA: HIVI TANZANIA baada ya miaka kumi (10) itakuwa na vichaa wangapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Kuzingatia AFYA: HIVI TANZANIA baada ya miaka kumi (10) itakuwa na vichaa wangapi?

Discussion in 'JF Doctor' started by james mangu, Jun 1, 2012.

 1. j

  james mangu New Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tujiulize kitu hiki.. Hivi Baada ya miaka Kumi Tanzania itakuwa na Vichaa wangapi? na Wagonjwa wangapi wa Kansa ya mapafu or magonjwa elfu 4000 yanayosababishwa na Uvutaji wa Sigara na madawa ya Kulevya. Kila leo wimbo ni ule ule Vijana wanadhidi teketea ? Serikali hipo kweli? au imelala na Kama hipo why inashindwa kudhibiti hili wimbi ambalo linakuja kwa Kasi ... Tanzania ya kesho isipotee inabidi tufanye zoezi la kutunza Maadili yetu lakini kama Tukiweza ruhusu hii hali naamini kabisa hata hiyo miaka kumi ni mingi.. Mungu ametupatia Umri wa Kuishi ni miaka sabini (70) na tukiwa na Nguvu miaka themanini (80) hii mingine unayokuwa nayo ni kwa neema tu, But kwa hili wimbi tunadhidi kupunguza siku zetu za kuishi ata wimbi la kuongezeka Magonjwa ya kutisha kama UKIMWI na magonjwa mengine ya ZINAA yanaletwa na utumiaji wa Sigara na Madawa ya Kulevya.
  Basi Hatuna budi serikari yetu ifanye haya:-
  1) Iandae sehemu ambazo wavutaji awatahathiri viumbe wengine(binadamu) kama ni kuweka vibanda vya wavutaji.. ili mtu akijisikia kuvuta basi aende kwa maeneo or vibanda vilivyowekwa..
  2) Serikari ipinge vita kabisa kuhusu uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya kwa nguvu zote
  3) Serikari na hasa hasa Jeshi la Polisi liwe wazi kwa jamii husika wakati linapokamata madawa ya kulevya na linapotaka kuteketeza maana utasikia tu wamekamata Heroin lakini utasikia kamwe Heroin ilipoteketezwa ... " Labda ndio hizi zinazokuwa mabarabarani vijana wanatumia"
  4) Serikali pamoja na Halmashauri za Mji na Majiji zisiweke Mabango ya Kuhamasisha Uvutaji wa Sigara yasiwepo Kabisa
  5) Serikali itoe nasaha lakini na kuwaamuru hawa watengenezaji wasiweke picha ya haina yoyote katika pakiti za sigara . " Yaani Pakiti ziwe PLAIN tu" Zisiwe na michoro yoyote kusaidia wimbi la watu lakini hasahasa vijana Kutengeneza Hatima zao za Kesho..

  Ni haya machache tu
  Asanteni
   
Loading...