Kwa kuwakodia ndege Wabunge; Barrick imetoa rushwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kuwakodia ndege Wabunge; Barrick imetoa rushwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 9, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,
  Maliasili na Mazingira.James Lembeli

  Barrick yawakodia wabunge ndege kwenda Nyamongo

  HATUA ya uongozi wa mgodi wa North Mara Barrick uliopo Nyamongo, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara kukodi ndege tatu ndogo kwa ajili ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwenda mgodini hapo, imezua malalamiko huku baadhi ya wananchi wakidai kwamba kitendo hicho huenda kikashawishi mtizamo wa kamati hiyo.

  Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli jana ilifanya ziara ya siku moja mgodini Nyamongo ikitokea mjini Dodoma, ziara ambayo kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo yake iliyoyatoa mwaka jana kuhusu athari za mazingira zilizosababisha baadhi ya wakazi wanaouzunguka kupata athari za kiafya.

  Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alikuwa amealikwa kuambatana na kamati hiyo, lakini safari yake iliishia Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma baada ya kubaini kwamba ndege husika zilikuwa zimekodiwa na kampuni ya Barrick. "Kweli mimi nipo Dodoma, nimerudia pale Airport (Uwanja wa Ndege), siwezi kwenda kuwasaliti wananchi wangu wa Tarime, maana kama tunakwenda kuwakagua Barrick halafu tupande ndege za Barrick sidhani kama tutatenda haki," alisema Nyangwine alipozungumza na gazeti hili kwa simu na kuongeza:

  "Barrick ndiyo (kampuni) inayotuhumiwa na wapiga kura wangu kwa kuwanyanyasa kwa kutowalipa baadhi yao fidia za mali zao hadi sasa mbali na kuhamishwa maeneo yao, kumekuwa na madhara makubwa kwa wananchi kutokana na matumizi ya maji yenye kemikali za sumu kutoka mgodini na maji hayo yanaingia Mto Tigite na kuleta madhara pia kwa wanyama, halafu nipande ndege yao! Haiwezekani."

  Msimamo wa Nyangwine unafanana na ule ambao umewahi kutolewa na Lembeli katika moja ya vikao vya Bunge mwaka 2009, akisema kwamba amekataa kupanda ndege za kampuni hiyo kwani huweka gharama za safari hizo kama sehemu ya huduma inazotoa kwa jamii. Lakini jana, Lembeli aliwaongoza wabunge wenzake kupanda ndege za Barrick ambazo zilitua Dodoma majira ya asubuhi na ujumbe wa baadhi ya wakuu wa kampuni hiyo, walioongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Deo Mwanyika kisha kuruka kuelekea Nyamongo.

  "Kilichonishtua ni kumwona yule bwana Mwanyika na hapo nilimwuliza Mwenyekiti (Lembeli) kwamba hii siyo rushwa? Lakini yeye akanijibu kwamba siyo rushwa kwa sababu ni jambo ambalo limefanyika kwa uwazi, lakini mimi nikaona kwamba siwezi kwenda na kamati hiyo kwa sababu hapo hakuna uhuru wa kufanya kazi," alisema Nyangwine. Alisema wananchi wake wasingemwelewa iwapo wangeshuhudia akishuka kutoka kwenye ndege ya Barrick wakati ni siku chache tu zilizopita alilalamika bungeni kuhusu madhara na unyanyasaji unaofanywa na kampuni hiyo dhidi ya wananchi.

  "Serikali hii ina uwezo wa kuwasafirisha wabunge wa kamati yoyote ile kama kuna suala lenye mgogoro au utata ili kubaini ukweli, sasa hii ya kuchukuliwa kwa ndege ya watuhumiwa haki haitatendeka ndiyo maana nimeona nisipande ndege hiyo ningelijua mapema ningekwenda huko jimboni kwangu wangenikuta hukohuko," alisema Nyangwine.

  Ofisi ya Bunge
  Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema jana kwamba ziara ya kamati hiyo ilipata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kampuni ya Barrick iligharamia kila kitu katika ziara hiyo. Hata hivyo, alisema hakuwa akifahamu idadi ya wabunge waliokwenda lakini taarifa ambazo Mwananchi lilizipata zilisema kuwa walikuwa zaidi ya 20, wakiwamo, Lembeli, Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkader Shah na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa.

  Wengine ni Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo na Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Buchosa (CCM), Dk Charles Tizeba, Mbunge wa Kikwajuni (CCM), Hamad Yusuff Masauni na Mbunge wa Longido (CCM), Mike Lekule Laizer. Joel alisema Spika aliridhia ziara hiyo kugharamiwa na Barrick na kwamba suala la wabunge kukubali au kutokubali kushawishiwa katika uendaji wao litategemea msimamo wao wenyewe kama kamati.

  "Kwa kawaida ziara za wabunge na Kamati za Bunge hugharamiwa na Ofisi ya Bunge, lakini ni kwa zile tu ambazo zipo kwenye kalenda na ratiba ya mwaka, sasa hii ya kwenda Nyamongo haipo kwenye utaratibu huo hivyo haikuwa rahisi kugharamiwa na Ofisi za Bunge, ndiyo maana waliomba kwa Spika ili Barrick wagharamie naye aliwaruhusu," alisema Joel.

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Barrick, Teweli Teweli alisema ilikuwa ni lazima kwa Barrick kugharamia ziara ya Kamati hiyo ya Bunge kutokana na asili ya kazi waliyokuwa wamekwenda kuifanya mgodini hapo. Teweli alisema kwa kuwa Barrick walikuwa wakituhumiwa kwa uharibifu wa mazingira, taratibu za kisheria zinawalazimisha kugharamia mchakato mzima wa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na taasisi mbalimbali za Serikali na Bunge na kwamba ziara ya jana inaangukia chini ya utaratibu huo.

  Mgodini Nyamongo
  Katika Mgodi wa Nyamongo, wenyeviti wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo wa Nyamongo, jana walizuiwa kuingia ndani ya mgodi huo walipokuwa wakitaka kwenda kushiriki katika mazungumzo baina ya uongozi wa Barrick na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge. Miongoni mwa waliofungiwa nje ya lango kuu la kuingia mgodini hapo ni Elisha Nyamhanga wa Kijiji cha Nyangoto, Omtanzania Omtima wa Kijiji cha Kewanja na Daudi Itembe wa Kijiji cha Matongo.

  Februari, mwaka jana kamati hiyo chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Job Ndugai ilifanya uchunguzi wa taarifa za athari za sumu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mgodi huo na kutoa taarifa inayoweka wazi kwamba kulikuwa na udhaifu katika ufuatiliaji wa sakata hilo. Kamati hiyo katika maazimo yake iliiagiza Serikali ichukue hatua za haraka kulichunguza suala hilo na kutoa malipo ya fidia kwa waathirika, huku baadhi ya wabunge waliochangia taarifa hiyo wakitaka kuwekwa kwa taratibu za kisheria za kukagua migodi.

  Mwananchi
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kamati za bunge zinapotembelea maeneo na taasisi mbalimbali na hata makampuni hulipiwa na serikali kutoka matumizi ya shughuli za bunge. Hawa Barrick wanajulikana kwa kashfa za kuwarubuni viongozi mbalimbali wa serikali kama inavyofahamika. Iweje sasa Bunge lisafirishwe kwenda Tarime kwa ndege za Barrik? Hii siyo rushwa?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,492
  Trophy Points: 280
  Wabunge hawa hawa baadhi yao walipokea rushwa toka Madini na Nishati ili kuhakikisha wanaipitisha bajeti ya Wizara hiyo, hadi hii leo si Kikwete, Pinda wala Makinda waliotoa kauli yoyote kuhusu rushwa ile, hivyo inaelekea Wabunge wameachiwa mlango wazi wa kupokea rushwa iwe toka Wizarani au Mwekezaji.
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nyambari Nyangwine asitudanganye! Yeye alishapigiwa marufuku na wananyamongo kwenda kwenye maeneo yao. Sasa asivunge kwa kisingizio cha ndege ya kampuni ya Barrick! Yeye Tarime hatambuliki kama mbungu. Kwa nini hajarudi Tarime tena tangia wamtimue kwa mawe ktk tukio la juzi la Nyamongo? Aache unafiki!
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ni kosa kubwa sana kimkakati kwa wabunge wa CDM kupanda ndege za hawa mabaradhuli. Kwa nini wenyeviti wa vijiji walizuiliwa kuhudhuria? Katika hili uamuzi wa Nyangwine ulikuwa sahihi.
   
 6. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi ni kweli kwamba wabunge hawajawahi kwenda Nyamongo kuchunguza hili sakata? Au mim mdiye niliyesahau,maana kuna wakati fulani wabunge walienda kuchunguza madhara ya mto Tigite au ndiyo ile ya UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA HUKU WANACHI WAKIPATA TAABU.
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nchii hii usanii kila kona....
   
 8. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tanzania x2 nakupenda kwa moyo wote...
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  bongo inaitwa takrima...
   
 10. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kupanda ndege za Barrick kwenda Nyamongo ni rushwa, kama Spika ndiye aliyebariki hili ameingia choo cha WANAUME, atawezaje kuwawajibisha wabunge waliopokea BAHASHA ya Jairo na wale waliokamatwa na Kafulila wakiomba rushwa wakati yeye amehongwa na Barrick kwa usafiri wa ndege kwa kamati ya Bunge?. Hii ni njia ya kupotezea uchunguzi wa Jairo & Wabunge wa CCM wanaoomba rushwa pamoja na wale wanao ghushi sahihi za viongozi. - Ngoja tuone matokeo ya ripoti ya hiyo kamati.
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hapa hakuna kitu, nimeshangaa hata wabunge wa CDM wamekubali kupanda hilo pipa.
  Hope watakuja na statement tofauti na ile ya kimagamba magamba.
  Na kwa nini Barrick wamewazuia wawakilishi wa wananchi? kuna kitu wanaficha? au kuna mgao huko ndani.
   
 12. p

  politiki JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kama chama makini hakitakiwi kufanya mambo kama haya, kitendo cha wabunge wa chadema kupanda ndege za Barrick ni kosa baya sana.

  Kama tunawalaumu CCM basi lazima tuwe tayari kuwakosoa CDM wanapokosea kwa sababu ya conflict of interest kwani hauwezi kufanya uchunguzi huru wakati mmoja anayechunguzwa ndiye analipia gharama za kuchunguzwa hakuna fairness kabisa kwa wananchi wa nyamongo by the way nimemwandikia email kiongozi wao James Lembeli kupinga kitendo hicho.

  Wabunge wa CHADEMA inabidi muwe makini sana kwani CCM wamefika hapo walipo kwa sababu ya mambokama haya hawajui pa kutokea. Kuonyesha kujirudi wapande usafiri wao kwa gharama zao na kukiri kutorudia tena makosa kama haya.

  Slaa/mbowe tunaomba maelezo ya swala hili kwani hatukutegemea mambo
  kama haya kutoka CHADEMA. Binafsi, I am very disappointed with CHADEMA ktk hili.

  Kwa hili bogus Nyangwine was right kukataa usafiri ule.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Bunge letu limeoza sana.
   
 14. Imany John

  Imany John Verified User

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  "You'r not supposed to be blind with patriotism that you can't face reality.wrong is wrong,no matter who say it''

  By

  Malcom little X.
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  ni mbunge gani wa chadema aliyepanda ndege ya hao maharamia wa barric?

  kama hilo ni kweli, chadema wamekosea.

  naunga mkono hoja.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sasa wewe nikikutukana nitaonekana mkorofi. Hujasoma habari unakurupuka kuchangia tu. Kwani siunyamaze tu. Siolazima uchangie, unatuongezea urefu wa thread bure.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tujiulize yafuatayo:

  Ofisi ya Bunge
  Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel amesema kwamba ziara ya kamati hiyo ilipata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kampuni ya Barrick iligharamia kila kitu katika ziara hiyo hata hivyo, hakuwa akifahamu idadi ya wabunge waliokwenda.
  ------kama yeye hajui idadi nani anahusika na ruhusa ya ziara kama hizo za kibunge.

  Lembeli
  Katika moja ya vikao vya Bunge mwaka 2009, Lembeli alikataa kupanda ndege za kampuni hiyo kwa madai kwamba huweka gharama za safari hizo kama sehemu ya huduma inazotoa kwa jamii, lakini Lembeli huyo huyo safari hii aliwaongoza wabunge wenzake kupanda ndege hizo za Barrick.

  -------Lembeli my friend try to be consistent

  Wabunge wa upinzani
  Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo pia walikuwa kwenye msafara.
  -------Chonde chonde muwe waangalifu wapinzani wenu huwa wanatafuta weak point kama hizi jifunzeni kwa Mnyika alivyostukia dili la bahasha ya kamati.

  Nyangwine
  Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alikuwa amealikwa kuambatana na kamati hiyo, lakini safari yake iliishia Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma baada ya kubaini kwamba ndege husika zilikuwa zimekodiwa na kampuni ya Barrick.
  --------kwa hili nampongeza Nyangwine ungepanda hiyo ndege wapiga kura wako wasingekuelewa.

  But All in all kweli hakuna dalili ya takrima hapa? ---- Nasikia harufu ya rushwa.
   
 18. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana JF hebu nielewesheni nimesoma katika gazeti moja jana kwamba kuna wabunge waliokwenda kuikagua kampuni ya barrick kama imetekeleza maelekezo iliyopewa awali kuhusu utunzaji wa mazingira pamoja na mambo mengine.

  Kilichonishitua ni kusikia kuwa kampuni au mgodi wenyewe ndiyo uliokodisha ndege zilizowachukua waheshimiwa wabunge kuwapeleka na kuwarudisha huko mgodini.

  Kama habari hii ni ya kweli sitashangaa kuwa wameandaliwa pia chakula cha mchana, vinywaji na bahasha. Najiuliza, katika hali hii waheshimika wabunge hawa walikwenda kukagua kweli au walikwenda kuvinjari na kujazwa mapesa?

  Je, wabunge wetu kweli wako makini? sio kweli kweli kwamba wameshatuona watanganyika hatuna hata yale mawazo ya kufikiria jambo? Nilisikia pia kuna mheshimiwa mbunge mmoja alikataa kupanda hivyo vipipa vyao. Naona huyu kama ni kweli anafikiria kwa kutumia kichwa.

  Naomba kuwasilisha
   
 19. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Iringa Bw .Mgaya akiwa angani na ndege huku akiwa amekosa amani kiasi cha kutamani kuruka kwa madai kuwa usafiri huo ni mgeni kwake,mgaya ambaye alipanda ndege hiyo kutoka mjini Njombe baada ya kuomba msaada wa kusafiri na usafiri huo kutoka kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ambaye alikuwa akiwai mjini Dodoma kwa ajili ya vikao baada ya kumaliza ziara yake na naibu waziri wa uchukuzi Dkt Athuman Mfutakamba hata hivyo katibu huyo alishukia katika uwanja wa Ndege wa Nduli Iringa huku akiwa amejishika kifua chake na kutoamini kabisa kama yaliyomkuta kwa kupanda ndege hiyo huku akijuta kuwa angejua kama usafiri huo ni hatari kuliko ule wa boti majini basi . Chanzo cha habari hapa   
 20. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  mmmhhhh!!
   
Loading...