Kwa kuwa Wizara ya Fedha si Swala la Muungano, Hizi RUZUKU hulipwa vipi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kuwa Wizara ya Fedha si Swala la Muungano, Hizi RUZUKU hulipwa vipi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Dec 23, 2010.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mpango wa serikali kuvipa vyama vya siasa RUZUKU ni sawa kabisa kwa kuwa ni vyama vyetu sisi wenyewe. Lakini, maswali yote yatakua yamejibiwa juu ya zoezi hili ipasavyo??

  Labda nanze kwa kuuliza kwamba je, hizi fedha za RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA zitatolewa na Serikali gani ukizingatia ukweli kwamba WIZARA YA FEDHA si swala la Muungano. Hebu tuwekane sawa hapa.

  Naona CUF ina wabunge wengi Visiwani, chini ya Serikali ya Zanzibar ambayo ina Wizara yake ya Fedha, kuliko hali halisi ilivyo huku bara. Nayo CCM ina Wabunge wengi zaidi Bara, ambako nako kuna Wizara yake ya Fedha, kuliko hali halisi ilivyo kule visiwani. Sasa ulipaji wa ruzuku hizi zitakuekoje hapo??


  HOJA YANGU:


  Wenye habari zaidi tujuzeni kama Mkaguzi Mkuu wa Fedha na Matumizi ya Serikali Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Msajili wa Vyama Mzee John Tendwa na wenyeviti wenyewe wa Vyama Tanzania wamekwishaliona UTATA huu.


  Kusije kukatokea vyama fulani KULA DABO Bara na Visiwani au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuubeba mzigo wote wa kulipa vyama vya siasa ruzuku kwa kujumuisha na wabunge wa Bara ambao hawana faida kwao visiwani.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tendwa atusaidie kwa hili!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Maana ulipaji kodi na uwakilishi lazima ziendane. Kusije kukatokea mlipakodi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akawa anawalipa Ruzuku vyama ambavyo wajumbe wake ni wa bara.

  Endapo hili halijaangaliwa uzuri, kuna JAMBO ZITO chini ya bahari katika hili.
  :bump:
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mmh, ''Kusije kukatokea mlipakodi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akawa anawalipa Ruzuku vyama ambavyo wajumbe wake ni wa bara".

  Tafiti vizuri! The contrary could be true

   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huu ni mfano wa mtafaruku wa Muungano wetu! Wizara ya Fedha ni ya Muungano kwani Zanzibar haina sarafu yake binafsi na wala haina Benki kuu binafsi. Haya yaoneni wenyewe jinsi mlivyo chetu changu changu changu!
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Unataka kusema ile Wizara ya Fedha Zanzibar wala si mali-kitu kwani?? Au wewe mwenyewe haujawahi kusikia kila upande wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Wizara yake ya Fedha??

  Mimi naona kuwa na sarafu moja yenye kuchangiwa picha na historia zetu si tatizo isipokua kwenye kulipana ruzuku kwa vyama hapa tena kwa kuzingatia IDADI YA WABUNGE ambao chama husika kimebahatika kuwapata katika chaguzi.

  Tuelewesha vema hapa jaama.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hii haijakaa vizuri inahitaji ufafanuzi. Mfumo wa serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar kuna impact. Nijuavyo mie mataifa mengine yenye mfumo wa serikali zaidi ya moja na kisha kuwa na serikali kuu ya shirikisho inayotokana na serikali mbalimbali, kuna bajeti ya kila serikali na kuna bajeti ya serikali ya shirikisho.
  Tatizo tanzania tuna serikali ya zanzibar, hakuna serikali ya tanganyika na kuna serikali ya Shirikisho yaani ya jamhuri. Sasa mpangilio wa bajeti kama serikali ya Jamhuri kama ndiyo inayolipa ruzuku kwa maana nyingine watanganyika tunanyonywa na wazanzibari kwa vile wana serikali mbili na sisi tuna serikali moja ambayo tunashiriki na wazanzibari.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Wadau,

  Kama hili nalo ni kero ya muungano basi lisukumeni kwa tume/kamati ya kero za muungano.

  Pia Tendwa anaweza kutupatia maelezo kidogo, sidhani kama maelezo yake yatajitosheleza. Katika Tanzania yetu, hakuna jibu kwa kila kitu. Kwa hiyo tutaliundia jopo,kamati kumshauri rais kuhusu hili na yeye ataelekeza nini kifanyike!!!
  Tanzania yetu!!
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  mkuu,
  unafikiri tunaihitaji serikali ya Tanganyika? kwa sababu gani?
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,809
  Likes Received: 5,119
  Trophy Points: 280
  ..lakini vyama si lazima viwe vina sura ya muungano?

  ..labda..labda hiyo ndiyo inayosababisha ruzuku itoke serikali ya muungano.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  RUZUKU KWA VYAMA VYA SIASA NA ULIPAJIWA KATI YA SERIKALI MBILI TANZANIA

  Nadhani kama vile kila Mbunge atokaye Bara ni Mbunge wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini ukigeuza shingo lako upande wa pili, bila shaka si kila Mbunge wa Tanzania Visiwani ni Mbunge wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Na kwa mantiki hii, inamaana ya kwamba Mbunge huyu atokaye Pemba na au Unguja na uchaguzi wake uliinuiwa uwe ni ulu wa baraza la wawakilishi kule Zanzibar, hapashwi kuchovya tonge kwenye kibakuli chenye kitoweo kwa ajili ya wabunge wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hata kama Chama cha siasa kilichomfadhili kupata ubunge wake kwenye baraza hilo la wawakilishi ni kile kile kilichofadhili wabunge wengine toka huko huko Tanzania Visiwani LAKINI kwa kusudio la kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Dodoma.

  Chini ya hoja yangu hii ni kwamba napendekeza yafuatayo kuzingatiwa na washikadau wote wa suala hili:

  1. Mahesabu ya Chama gani cha Siasa kipate Ruzuku kiasi gani KIZINGATIE IDADI YA WABUNGE WAKE Katika Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) tuu na hundi kuandikwa na Wizara ya Fedha ya SJMT na kupitishwa na Spika wa Bunge la SJMT kwamba idadi hiyo ya wabunge kweli ni sahihi na kwamba KATIBA ya SJMT hakika inawaruhusu watu hao wanaoitwa Wabunge wa SJMT kufanya kazi zao za ubunge pale Dodoma.

  Hao maafisa wetu wakishafanya hivyo ndipo hundi hiyo iende ofisi ya Tendwa kabla hajaikabidhi kwa VIONGOZI HALALI wa chama kilichowafadhili wabunge tajwa katika Bunge la SJMT.

  2. Naomba ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa mahesabu za Serikali atoe ripoti ya wazi kabisa inayoainisha kwamba ni chama gani kimewahi kupewa RUZUKU kwa kuzingatia idadi ya wabunge katika bunge la SJMT tangu mfumo wa vyama vingi uanze nchini.

  Na endapo itabainika ya kwamba kuna chama chochote ambacho kimewahi KUCHOTEWA FEDHA ZA WALIPA KODI tuseme kwa mgongo wa idadi ya wabunge wa SJMT wakati idadi hiyo inapingana na WAPI mbunge anakofanya kazi (Baraza la Mapinduzi Zanzibar au Bunge la SJMT Dodoma) na KUSUDIO LILILOKWEPO wakati wa kuchaguliwa kwa mbunge huyo basi ijulikane wazi kwamba ama SMZ au SJMT au zote kwa pamoja ZILIKUA ZIKIIBIWA kinyume na KATIBA ya SMZ na ile ya SJMT zinavyotamka juu ya Wabunge na Ubunge wao.

  3. Kwenye kuzingatia masuala ya utawala bora wa masuala ya mapato na matumizi ya fedha za na kwa serikali hizi mbili na kutilia sana mkazo masuala ya Checks and Balance, walipakodi tutapenda kuona ama SMZ au SJMT zikirejesheana malipo ya RUZUKU kwa vyama vya siasa ambavyo kwanza hayakupashwa hata kidogo kuvuka meza kwenda upande wa pili.

  4. Na vyama vya siasa ambavyo vilidiriki KUPOKEA MALIPO KAMA HAYA KAMA RUZUKU ama kutoka kwa SMZ au SJMT kwa mgongo wa wabunge ambao itabainika malipo ya RUZUKU tajwa haya kupashwa kutoka huko na basi moja kwa moja chama husika ama kirejeshe RUZUKU HIZO KWA THAMANI YA SASA, yakila shilingi walioipata na Interest ya muda chama hicho kiliamua 'Kutukopa' sisi walipakodi kwa ajili ya matumizi binafsi ya chama husika nje kabisa ya tamko kwenye KATIBA, ambazo hazikua stahili zao kwa mujibu wa KATIBA ya SMZ au SJMT ambazo vyama hivyo vya siasa vinafahamu fika kwamba VILIKUA NA WAJIBU WA KUVISOMA NA KUVIELEWA fika juu ya swala zima la Mbunge na Ubunge wake kule SMZ au hapa SJMT.

  Vile vile, njia mbadala inaweza ikawa ni kwamba hiyo thamani halisi ya hizo shilingi zilizoazimwa na chama toka kwa walipakodi ZINAWEZA ZIKAPIGIWA MAHESABU NA KUANZA KUKATWA KWA ASILIMIA 50% kila wakati chama husika kinapopata kulipwa RUZUKU yake na kurejeshwa kwenye hazina yetu kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama vile KUTUNISHA MFUKO WA MKOPO KWA AJILI YA WANAFUNZI VYUO VIKUU NCHINI ambao kwa sasa zoezi la mkopo limekua ni kitendawili kigumu mno.

  5. Vyombo vya habari nchini vipewe ushirikiano wa hali ya juu sana katika kufuatilia hichi KITENDAWILI CHA ULIPAJI RUZUKU kwa vyama vya siasa kwa mgongo wa idadi wa wabunge, mahala wanakofanyia kazi zao, kusudio ilivyokua wakati wa kuchaguliwa kwake na MAREJESHO AMBAYO WALIPAKODI TUNAPASHWA KUDAI ama kwa upande wa SMZ au SJMT au kushoto kulia hapa. Wakaguzi binafsi wa mahesabu nao wapewe nafasi ya kufanya kazi hiyo.

  Ikumbukwe kwamba haya yote ninayoyazungumza NINAYAZUNGUMZIA KAMA MLIPA KODI MAKINI ambaye napenda nijue kodi yangu inatumikeje, kwa maslahi gani na KATIBA ya sasa yenyewe inasema nini juu ya hilo. Ni vema wahusika wakuu ambao ni Wizara za Fedha, Ofisi za Bunge, Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini wakafanya hima juu ya jambo hili, wakatoa taarifa sahihi na ukweli mtupu ndani ya muda ambao ni sahihi kutendeka utoaji ripoti juu ya jambo kama hili lenye umuhimu mkubwa kwa taifa. Ukiuliza kwamba nilifikake kwenye kuchimbua haya yote, jibu langu ni rahisi tu; NCHI YAKO INAPOPORWA KUSHOTO KULIA, MTU UNAFIKA MAHALI UNACHAPWA KISAWASAWA NA MIJELEDI YA MAFISADI HAO NA KUANZA KUFIKIRI kiundani zaidi tena bila uzembe wowote ule.

  Kwa kumalizia tu, naamini Wa-Tanzania walipakodi wenzangu kamwe hawatochelewa KUJITULIZA VICHWA VILIVYOJAWA NA MIHANGAIKO ISIOFANIKIWA KILA KUKICHA na kutafakari juu haya ninayoyasema.

  Ndugu Wa-Tanzania walipa kodi, Wana-JF Great Thinkers, Wageni wetu mnaotembelea jukwaa letu hili na hata wadau mnaoguswa na HOJA HII YA MBUNGE, UBUNGE WAKE NA USTAHILI WA MALIPO YA RUZUKU KWA CHAMA CHAKE chini ya maelekezo ya KATIBA zinazohusika SMZ na SJMT, nawashilisha sehemu ya pili ya hoja na mjadala uendelee.
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani saa zengine tunatakiwa tuwe at least kidogo Great thinkers na sio Great Stinkers. Unapohoji kuwa kwanini CUF inapewa ruzuku pamoja na Chadema na CCM jiulizeni na maswala haya vilevile:-
  a. Je zanzibar haipo katika mipaka ya Tanzania?
  b. Wale wanaochagulia visiwani zanzibar ni wabunge (wanatambulika na sheria za bunge) au wapambe tu.
  c. Vp wale wabunge wa ukerewe au mafia nao tuanze kuwahoji kwa vile tu wako visiwani?
  d. Je tutafika?

  Kujadili hoja kama hii ni dhaifu kwasababu madhali wao ni wabunge waliochaguliwa na wananchi na chama kinawagharimia kuleta maendeleo ya majimbo yao sasa kwanini tunahoji wanapopewa ruzuku??? Au ndio mnataka ruzuku yote iende chadema chama kinachopendwa humu JF!!! Hoja zengine!!!!
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hivi una maana kuwa CCM na CUF wanapata rudhuku mara mbili ama?? Yaani wanapata za ZNZ then za serikali ya muungano?? Kutokana na katiba yetu hii inawezekana kabisa iwapo ZNZ kama nchi wakaamua kuvilipa vyama kutokana na wawakilishi wake kwenye balaza la wawakilishi na selrikali ya muungano ikawalipa pia kutokana na wabunge wao kwenye jamuhuri.

  Hayo ndiyo yatakuwa ni mapungufu ya katiba. Unless ZNZ kama hawatoi rudhuku.
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Sijaona popote ktk katiba ambako imeandikwa a nation/country of z'bar. Z'bar ni kijieneo cha nchi ya Tanzania,ivo kama wabunge watatoka sehemu yoyote Tanzania ruzuku yake italipwa kwa chama na katiba ya sasa yenye viraka kama kaptula ya Babu inasema Chama cha siasa haitaandikishwa kama kina sura ya udini,ukabila,sehemu moja ya Tanzania nk. Ina maana kama jamhuri italipa ruzuku italipa kwa cuf ,ccm,tlp au cdm kufuatana na uwakilishi wao katika bunge la Nchi iyo. Hapa wataalam elezea zaidi ili kodi yetu iliwe kihalali.
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu hakuna chama kinachopata ruzuku mara mbili kwani hakuna wabunge wawili wawili. Mie niliwahi kumuuliza Professa mmoja kuhusu hili jambo akanifahamisha kwamba Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania na ili kutofautisha wakaweka kuwa zanzibar kuna wawakilishi ambao wanaingia katika baraza la wawakilishi. Kutokana na hilo basi wao wanaingia katika muhimili wa Zanzibar kama nchi iliyo na serikali yake, jeshi lake na baraza lake. Hivyo basi lazima ili waweze kutunga sheria lazima wawe na wawakilishi wa kila jimbo kuweza kusimamia na kutunga sheria.

  When it comes to muungano kwakuwa muungano wa nchi ni baina ya SMZ na Serikali ya Tanzania basi kunahitajika wabunge ndani ya bunge la muungano wa Tanzania. Hivyo wabunge wanaochaguliwa ni wabunge sahihi wa muungano sasa sijui hoja ya kulipwa mara mbili mnaitoa wapi. Mie nadhani watu wangelianza kwa kuhoji serikali yetu ya tanganyika imefia wapi???
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu kasome katiba mpya ya zanzibar utapata jibu lako. Ilikuwapo hicho kipengele Nyerere akaja kukiondoa baadae ila juzi juzi kabla ya uchaguzi wazanzibar walikirudisha kipengele hicho.
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,809
  Likes Received: 5,119
  Trophy Points: 280
  Uwezo Tunao,

  ..mbona hiyo ruzuku ya vyama na malipo ya wabunge ni cha mtoto tu??

  ..wakati mwingine hata mishahara ya watumishi wa SMZ inalipwa na wa-Tanganyika.

  ..umeme tunawapa bure, na hata wakilipa wanalipa kwa bei ya chini kuliko wa-Tanganyika.

  ..it is about time wa-Zenj wajitegemee. mbona Rwandi,Burundi,Comoro,wanaweza?

  ..huu muungano una madubwana mengi tu ya hovyohovyo, it is much easier uvunjwe, na badala yake tushirikiane kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Asante kwa maelezo mkuu. Ila nafikiri hujanijibu swali langu la msingi. Selikari ya ZNZ haitoi rudhuku kwa vyama kupitia idadi ya wawakilishi??
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UFAFANUZI ZAIDI HOJA YA SERIKALI YA UBIA & ULIPAJI RUZUKU

  Ndugu usipate taabu sana katika hili la wabunge, ubunge wao na ulipaji RUZUKU kwa vyama. Mwana-JF mmoja, Ndg Ng'wanangwa alishatutahadharisha juu ya KUPIGANA NA FIKRA ila kupingana nalo ni ruksa kabisa.

  Bora ugombane na mtu lakini usigombane na HOJA maana kama lipo, lipo tu na litajisimamia na kujieleza lenyewe tu bila kupendezeshwa na watu. Nitatoa mfano rahisi tu kutufanya kuliona hili jambo uzuri sana hapa chini.

  1. a) Hebu chukulia kwamba SMZ inayo jumla ya Wa-Tanzania wanaitwa wabunge 100.

  b) Na kwamba kati ya hao wabunge 100, kati yao 80 ni wa Bunge la wawakilishi Z'br.

  c) Na kwamba wabunge wengine 20 ndio wa kwenda Bunge la SJMT Dodoma.

  d) Itambulike wazi kwamba wakati KATIBA ya SJMT inaelekeza kwamba vyama vyote vya siasa nchini ni lazima viwe ni vyenye sura ya KIMUUNGANO (yaani ujumla maeneo yote ya iliokua Tanganyika, Pemba na Unguja) hivyo kupata haki ya KU-SHARE sehemu ya ile idadi ya wabunge 100 (ikiwa na maana kwamba kwa siasa za ushindani, kila chama kitawania idadi fula kati ya wa 80 kwenye bunge la Wawakilishi Zanzibar na hivyo hivyo kati ya wa 20 kwenye bunge la SJMT kule Dodoma).

  LAKINI katiba hiyo hiyo inatoa baraka ya uwepo na uhalali wa SMZ kule na SJMT huku bila kuingiliana kiutendaji ila tuu katika yale MAENEO YA KI-MUUNGANO tu.

  Basi dira inayotolewa na KATIBA SJMT inabaini kwamba kwa kujitegemea kule kule, SMZ itawafurahia haki yake ya kujitegemea katika maeneo husika na vile vile KUWAJIBIKA KUGHARAMIA haki hizo, na SJMT nayo hivo hivo.

  Hii inaleta maana kwamba kati ya wabunge 100 SMZ italazimika kwa mujibu wa KATIBA ya SJMT kulipa RUZUKUZOTE zitokanazo na wale wabunge 80 ambao lengo la kuchaguliwa kwao na pia eneo lao la kazi ni katika ofisi inayoitwa Bunge la Wawakilishi kule visiwani. Wajibu huu unatakiwa kutekelezwa SMZ vyama vya siasa ambavyo vimefanikiwa kupata wabunge kule.

  Sasa tuiweke hivi, kati ya wabunge 80 wale wanaotumikia kule Visiwani tu na wala si katika Bunge na maswala ya Muungano Dodoma, tuseme:


  CCM kimefanikiwa kujinyakulia wabunge 33,
  CUF wabunge ................................ 32,
  CHADEMA wabunge .........................10,
  TLP wabunge ................................. 03
  TPP Maendeleo, Mbunge ................... 01
  NCCR-Mageuzi, Mbunge .................... 01
  Jumla ya Wabunge SMZ ............ 80


  Gharama ya Wabunge hawa 80 zilipwe, siku zote na SMZ kama ambavyo KATIBA ya SJMT inavyotambua uwepo wa serikali hii na kwa kuzingatia ukweli kwamba serikali hii inafurahia huduma za hawa waheshimiwa wabunge kule Visiwani kwa mambo ambayo si ya Ki-Muungano, ukiachilia mbali tofauti za kiitikadi za kisiasa na vyama vyao wabunge hawa.

  Kwa upande wa pili, miongoni mwa wale Wabunge 20 kutoka kule Tanzania visiwani kuja kwa ajili ya kazi waliochaguliwa kwa mujibu wa KATIBA ya SJMT kule Bungeni Dodoma na kwamba KWA UHAKIKA SJMT inaendelea kufurahia haki ya kupata huduma toka kwa waheshimiwa wabunge hawa pale Dodoma na basi SJMT nayo inawajibika moja kwa moja kugharamia ulipaji RUZUKU kwa vyama vya siasa vile vile na kwa misingi ile ile ya idadi ya wabunge ambao kila chama kitakua kimejinyakulia kati ya wale 20.

  Labda nayo tukaiweke hivi:


  IDADI YA WABUNGE NA WANAKOWAJIBIKA

  WABUNGE: VISIWANI BARA JUMLA

  CCM kimefanikiwa kujinyakulia wabunge .... 08, ............ 220 ...................... 228
  CUF wabunge ................................ ......06, .............. 21 ...................... 27
  CHADEMA wabunge ............................... 02, ............. 50 ....................... 52
  TLP wabunge ....................................... 01 .............. 08 ....................... 09
  TPP Maendeleo, Mbunge ......................... 01 .............. 02 ........................ 03
  NCCR-Mageuzi, Mbunge .......................... 02 .............. 10 ....................... 12
  Jumla ya Wabunge SJMT ........... 20 ............ 311 ...................... 331

  Sasa ndugu zangu Wa-Tanzania walipa kodi, Wana-JF tunaojadiliana, na Wageni wetu mnaotutembelea hapa jamvini, HOJA HAPA NI KWAMBA kwa kuwa SERIKALI YA MUUNGANO NI SERIKALI YA KI-UBIA, KATI YA Serikali mbili ambayo mbia mwingine (Tanganyika) ama alikufa au kapumzika bado usingizini, na basi walipakodi Tanzania wakafurahie ubia huu na haki zake zote na vile vile tukubali kuwajibika kugharamia furaha zetu hizo tunazozinuna kutoka kwenye ubia wenyewe hadi pale ambapo MKATABA WETU WA UBIA unavyotuelekeza.

  Hii ina maana ya kwamba kwa msingi wa mfano wa kinadharia hapo juu, walipakodi upande wa Tanganyika wanaelekezwa na KATIBA ya SJMT wakagharamie kwa peke yao kulipa vyama vya siasa RUZUKU kutoka Wizara ya Fedha ya Tanganyika hadi idadi ya wabunge 311.

  Na kwa upande mwingine Wabia wengine wa SJMT yaani walipa kodi Zanzibar nao wakagharamie kwa peke yao kulipa vyama vya siasa nchini RUZUKU kutoka Wizara ya Fedha ya Zanzibar hadi kwenye idadi ya wabunge 80.

  Na kwamba kwa msingi huo, SJMT ambayo sasa ndio sura halisi ya SERIKALI YA KI-UBIA uliko nayo pia ifurahie haki ya utumishi na huduma za wabunge wa MUUNGANO kwa kuomba walipakodi wa pande mbili za SERIKALI YA KI-UBIA na kulipa vyama vya siasa kama RUZUKU mpaka idadi ya wabunge wa Muungano unakokomea.

  Hii inatuelekeza kwamba wale wabungu 20 toka Zanzibar kwenda Bunge la Muungano ni kwa gharama ya kushirikiana ambayo SJMT lazima ilipe. Hii ina maana kwamba Walipa kodi wa mbia anayeitwa Tanganyika nao ni SHARTI WAKATUWEKEE MEZANI NA TUJUE WABUNGE WAO WA MUUNGANO ni akina nani, na wako wangapi ili nao gharama zao zikaingizwa kila mara kwenye hundi inayoandikwa na na SJMT.

  Na kama wabunge wa muungano kwa upande wa Tanganyika hawapo basi ni juu ya huyu mbia MZEMBE na wala hilo halimuondolei wajibu wa kuendelea kuwalipa wabunge waliopo kwa jina la SJMT wale 20 toka Zanzibar.

  Sasa, hapo awali niliomba maafisa wetu mbali mbali kuitikia hoja ya mlipa kodi mimi kwa kukagua taratibu za ulipaji ruzuku kwa vyama vya siasa nchini kwa msingi wa wabunge na ubunge wao kama ambavyo KATIBA zetu zinavyotuelekeza na waone kama kuna mlipaji RUZUKU fulani au vyama vinavyolipwa ruzuku hizo kama kweli mambo yote yanakwenda kwa USTAHILI WA UBIA WETU??? Lakini hata Mwana-JF alio na taarifa katika hili akatuwekee hapa jamvini.

  Sasa, wewe mwana-JF mwenzangu uliekua na waswali kifuani ambayo kidogo yalionekana kutopatiwa majibu basi endelea kuwauliza wanajamvini na kama TUNAO UWEZO wa kulijibu basi tutajitahidi. Karibu sana.
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  mkuu,

  Hapo kwenye red, huyo profesa kama umemkariri kama alivyosema basi alikudanganya, urudi kwake akuekee sawa hilo suala.
   
Loading...