Elections 2010 Kwa kuwa na ina Ilani mbili za uchaguzi kumbe CCM ina ajenda za siri......

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Utafiti wangu wa kina umebaini yakuwa CCM ina ajenda za siri ambazo utekelezaji wake utazua mgawanyiko mkubwa wa utaifa wetu na ndiyo maana hawapo tayari kuzizungumzia hadharani wakati huu wa uchaguzi na hili linathibitishwa na kuwepo Ilani mbili za uchaguzi.........

1) Ilani ya kwanza ni ile iliyopo mezani ambayo ina mambo ya kawaida ambayo CCM inakusudia kuyafanya kama uimarishaji wa miundo mbinu, kilimo kwanza na uboreshaji wa huduma za jamii kama elimu, afya n.k. Ilani hii JK na CCM yake ndiyo wanaipigia debe majukwaani kwa nguvu na utashi wote lakini siyo watakayoipa uzito wakipata ridhaa yetu ya kuiongoza nchi.

2) Ilani ya pili na ile ambayo ipo chini ya meza yenye lengo la kuendeleza matakwa binafsi ya JK ambayo hata yeye mwenye anafahamu fika yatakuza nyufa za utaifa wetu. Baadhi ya makusudio hayo ni uanzishwaji wa mahakama ya kadhi, kujiunga na OIC na kuvishughulikia vyombo vya habari ambavyo CCM wanavilaumu kuwa ndiyo chimbuko la wao kuchukiwa na wapigakura. La jabu CCM hawataki kuona mapungufu yao ya utendaji mbovu usiomjali raia na maendeleo yake.

Kwa unafiki mzito kabisa Naibu Mwenyekiti wa CCM Bw. Pius Msekwa alisema Kamati Kuu ya CCM walinyofoa kwenye Ilani ya uchaguzi wake lengo la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa sababu siyo sera ya CCM lakini JK kumbe huku amewahakikishia Sura ya Maimamu inayoongozwa na Sheikh mmoja machachari wa msikiti wa Mwembechai ambao una mazoea ya kughubikwa na vurugu nyingi kuwa hizo ni geresha za uchaguzi tu. Na ya kuwa baada ya uchaguzi hoja hiyo itarejeshwa kinyemela kwa kupeleka muswada bungeni ili uwe sheria. Matarajio ya JK yalikuwa "it wa business as usual" na ya kuwa watanzania bado wataendelea kujitweka zigo la kuibeba CCM hata kama utendaji wao ni wakusuasua tu.

Lakini upepo unavyovuma sasa hivi hiyo dhana yaelekea kutokuwa na mafanikio kwani JK na wagombea wenziwe wa Ubunge huenda wakapoteza Ikulu na miliki ya taasisi nyeti ya Bunge na hivyo kushindwa kuendelea na hoja hizi za usiri.


Kutokana na Bw. Membe kuliweka wazi hilo mbele ya maaskofu ni dhahiri kuwa ajenda ya siri ya uanzishwaji wa mahakama za kadhi na OIC sasa siyo siri tena.

Swali ambalo tunapaswa kujiuliza hivi kwa nini CCM na JK wake wanatuzunguka wananchi na kufanya mambo kiusirisiri? Tutawaaminije wakati hawaweki mambo yao yote mezani ili tuyajadili na kupima mantiki zake kama zipo? Kwa nini wanapenda kuendesha nchi kwa udikteta hivyo.......au kwa vile Jk ni mwanajeshi basi anaweza kuongoza nchi hii kwa misingi ya kijeshi?

Ilani yao ya siri ya uchaguzi vile vile imepania kushughulikia vyombo vya habari ikiwa na kuanzisha sheria kali zitakazowabana wale wote kwenye fani hii ambao hawapo tayari kutekeleza CCM inayoyataka. Katika hili wanataka kupeleka muswada bungeni wa kushinikiza wahariri wote wawe wamejiandikisha katika taasisi ya umma ambayo wao serikali ya CCM watakuwa wanaisimamia na kuitumia kufuta leseni za wahariri ambao ni wakosoaji wa serikali ya CCM na JK wake. Katika mkutano wa CCM uliompitisha JK hapo Dodoma Jk alionyesha dhahiri kukerwa na wahisani na baadhi ya vyombo vya habari vinavyowaunga mkono na JK alitoa tishio ya kuwa watashughulika nao baada ya uchaguzi

Swali hapa ni wapi kwenye Ilani ya uchaguzi CCM imeahidi kudhoofisha utawala bora? Hili linanithibitishia ya kuwa kumbe JK na CCM yake wanazo ajenda za siri kwenye Ilani ya chaguzi wanayoijua wao wenyewe ambayo hawako tayari kuiweka mezani kwa wapigakura kwa kuelewa tutaikataa...............This is scurrilous dishonesty, pure and simple......

Pili wataanzisha sheria za kukuza fidia ya malipo kwa vyombo vya habari vitakavyokuwa vimeshindwa kwenye kesi za "libel" au za madai ya kuchafuliwa jina.

Tatu, wataendelea kuteua majaji na wasajili wa mahakama ambao watahakikisha azma yao hiyo ya kuvifunza vyombo vya habari adabu kwa kuvifilisi kutokana na madai hayo makubwa ya fidia ambazo watashindwa wamiliki wa vyombo hivyo kulipa na hivyo kuvifilisi kwa kutumia sheria.

Nne, ni kuwashughulikia wote ambao waliwaunga mkono wapinzani kwenye chaguzi huu ikiwa kwa wafanyabiashara kufuatiliwa ulipaji wao wa kodi kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha hawapati zabuni za serikali. Kwa watumishi wa serikalini kuwateremsha vyeo au kufuta ajira zao katika mazingira ya kutatanisha kabisa ya kulipiza visasi.

Hizi ni baadhi ya changamoto ambazo utatuzi wake ni sote kujituma na kutoipigia CCM kura hapo J2 ijayo na kumaliza hatamu yake ya kiimla ambayo sasa imekuwa ni zigo zito kwa raia wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom