Kwa kuua pundamilia jela miaka 20, kwa kuua binadamu hakuna cha jela wala nini!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Nasikitikia kweli matukio ya mauaji ya wananchi yanayofanywa na dola kwa kuwatumia polisi yanazidi kushika kasi na mara nyingi hakuna wanaowajibishwa. Hata hivyo lililonishtua na kunisikitisha zaidi ni kitendo wananchi watatu kupelekwa jela miaka 20 kila moja kwa hatia kuua pundamilia wakitafuta kitoweo. Kwa habari zaidi soma hapa;

 
. Hata hivyo lililonishtua na kunisikitisha zaidi ni kitendo wananchi watatu kupelekwa jela miaka 20 kila moja kwa hatia kuua pundamilia wakitafuta kitoweo.

Sijui kutorosha wanyama hai 132 kutoka Tanzania kwenda nje, kutia ndani twiga watatu na tembo wanne, itakuwa jela miaka mingapi!
 
Watanzania hatuna budi kuelewa kwamba kutojua sheria mbalimbali za nchi ikiwemo ya wanyamapori sio kinga ya kutoshitakiwa pindi tukikutikana na kosa.Hii ni changamoto kwa Serikali na jamii nzima kwa ujumla.Serikali ije na mkakati wa kuongeza uelewa juu ya sheria mbalimbali za nchi kwa wananchi wake ,vinginevyo kila siku tutaishia kupewa adhabu ambazo pengine zingeweza kuepukika kama watu wangekuwa 'well informed'
 
Yule Mheshimiwa aliyeua wale wadada wawili (ndani ya Bajaji) kwa Kuwagonga na VX lake alilipishwa laki 7 tu.
Duu, hata kama sheria iko hivi lakini this is too much Bwana!!!
 
Sheria hufanya kazi kwa maskini kwa wenye nazo wala hawajui sheria ni nini
 
Kama sio 100% ya waliofungwa ni muhanga wa matajiri na masikin wasio na uwezo basi ni 99%

Hukumu kwa asiye na pesa huyo hukutwa na makosa na kufungwa miaka kadhaa ahapa Tanzania.

Hukumu ni kwa asiye na ndugu mwenye mamalaka serikalini hata kama kauwa makusudi kama UKIWAONA DITOPILE MZUZURI alitoka nje bila shaka shaka wala aibu yoyote.

Hukumu huwa na mkosaji kwa maskini lakini kwa matajiri na wenye mamlaka huwa wanagongwa, ni bahati mbaya nk. ndo hayo ya mzee chenge na mauwaji

Kwa Tanzania hukumu hazifuati sheria bali zinahukumu asiyenacho ndiye mkosaji, zaid ya 75%. Kwa matajiri na wenye mamlaka hakuna makosa ni kuaachiwa huru tu kwa vifungu hivyo hivyo na na double standard kwa tafsiri touafuti kati ya makundi hayo mawili, simmeona ya Lema kule arusha?

KWA TANZANIA HAKUNA HAKI< BALI UWEZO WAKO NDIO UTAKUPATIA HAKI HATAKAMA HUKUSTAHIKI
 
Back
Top Bottom