Kwa kutumia madaraka vibaya, Dr. Magufuli aachie ngazi!

Jamani hakuna Kipengele cha Kumburuza Mahakaman mtu kama Magufuli kwa kosa kama Hili?? Kwani ndo watajifunza na wengine,wataogopa!!! Otherwise 2015 ni Mbali mno

Mbona MARY NAGU hamtaji jina lake au kwakuwa mlishinda kule Arumeru..!!? Naye anastahili kuburuzwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka.
 
Utamaduni wa uwajibikaji haupo kwa viongozi wa CCM,hivyo suala la Magufuli kujiuzulu ni ndoto.
 
nawashangaa sana wanaomkubali magufuli, eti rais,
wakati ameshindwa hata jimbo lake wanahaha umeme na barabara hakuna.
 
Mukama nae alisema nin??????
kipindi cha kampeni Igunga, Mukama alisema (aliropoka) CDM wameleta makomando toka Misri, Libya na USA ili kuvuruga uchaguzi Igunga, mahakama imeomba athibitishe akaingia mitini
 
Magufuli siku zote anajifanya yuko juu ya sheria kwanza alitakiwa kujiuzulu kwani ameshasababisha hasara mbali mbali kwa serikali kama kubomoa kituo cha mafuta Mwanza baadae ikabainika kilibomolewa kimakosa na serikali kulipa fidia, kuuza nyumba za serikali na baadae kusababisha walioteuliwa kuishi mahotelini na serikali kuingia gharama kubwa, kuendesha bomoa bomoa bila kujali wanaobomolewa baadhi walipata hizo sehemu kihalali.

Ni mtu anayejua kucheza na vyombo vya habari lakini ukimfatilia kwa undani ni mtu mdhaifu aliongeza nauli za vivuko na wakanunua mashine lakini mpaka leo hazitumiki
 
Mbona MARY NAGU hamtaji jina lake au kwakuwa mlishinda kule Arumeru..!!? Naye anastahili kuburuzwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Hapa CCM ndo ambao wanatakiwa waweke pingamizi!Hoja kuu iwe uchaguzi haukuwa huru na wa haki kwa kuwa waziri wa serikali alitoa maneno ya kuipendelea CCM ishinde.Kauli yake ikaathiri matokeo kwa kuchochea chuki kwa wananchi na wakaamua kupiga kura ya hasira dhidi ya CCM.Kwa hiyo ni simple tu,ccm waweke pingamizi huku wakimshtaki Nagu na hivyo uchaguzi haukuwa huru na haki!
 
Magufuli ni mtu wa visasi kweli,katika jimbo lake la Chato wakati wa uchaguzi wa 2005 kata za Kachwamba na Kasenga walimnyima kula ikabidi wakati wa mradi wa umeme uliokuwa upite katika kata hizo kutokea biharamulo nguzo akazipitisha porini mbali kabisa na makazi ya watu pamoja na kwamba wananchi walikuwa tayari kupitishiwa katika maeneo yao.aliwaambia wazi kabisa kwamba alifanya hivyo kwa sababu hiyo.
 
Hivi huko Chato hakunaga watu makini wa kumtoa huyu jamaa, hebu jipangeni bana come 2015 tafuteni vijana wa CDM
ambao ni makini.
 
Bila shaka alikuwa anatimiza wajibu wake ingawa hakujua kuwa nguvu ya umma haihitaji ahadi za majaliwa ya muda mfupi vile
 
Hivi huko Chato hakunaga watu makini wa kumtoa huyu jamaa, hebu jipangeni bana come 2015 tafuteni vijana wa CDM
ambao ni makini.
Mbona nasikia hilo tayari! M4C ishafanya kazi yake. Hawa watu wamejisahau sana, na hivi walikuwa wanaona Mahakama ni kama jumuia ya CCM hivyo hawakuwa na hofu yeyote. Thanks to Tundu Lissu kwa kuizindua mahakama na wao kuanza kujitazama maana sasa ukitoa maamuzi ya ovyo kila mtu atakutazama na utaanza kuchunguzwa ulipataje nafasi hiyo.
 
Taasisi za nchi hii zisizo weka wazi separation of power,responsibilities and checks and balance nitatizo kubwa na mambo ambayo yamefanya kila kiongozi ajione kama mungu wa duniani.
 
Back
Top Bottom