Kwa kutumia madaraka vibaya, Dr. Magufuli aachie ngazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kutumia madaraka vibaya, Dr. Magufuli aachie ngazi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MANGUNGO, Aug 22, 2012.

 1. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mara kadhaa tumekua tukishuhudia viongozi wa serikali kama mawaziri na marais wastaafu kupanda katika mujukwaa ya siasa katika chaguzi ndogo za ubunge hata udiwani ili kusaka kusaka kura kwa chama chao hasa kwa njia chafu kama vtisho kwa wananchi, kama alivyotishia MAGUFULI kunyima huduma ya ujenzi wa daraja wananchi wa Igunga endapo hawata ichagua CCM.

  Hilo limeonekana pia Arumeru Mashariki baada ya MARY NAGU kuendeleza tabia hii ya kuwatishia wananchi kuwa wasipo chagua CCM basi jimbo litaenda likizo kimaendeleo.

  Binafsi MAGUFULI simuoni kama kiongozi bora, kwani kiongozi hawezi fanya UPUMBAVU alioufanya Magufuli kwa walipa kodi wa nchi hii. Kwa haeshima na taadhima inabidi Magufuli ajiuzulu kwani alichofanya ni ukiukwaji wa utawala bora na matumizi mabaya ya madaraka. Na ikiwezekana hata kushitakiwa mahakamani ashitakiwe, na liwe funzo kwa viongozi wa serikali kuwa unapokuwa mtumishi wa umma basi tambua mipaka ya majukumu yako.

  Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wote hawa ni watumishi wa umma kwa mujibu wa katiba. Kitendo cha Pinda kuhalalisha upuuzi na kusema hawa ni makada wa CCM na shughuli yao ni kuilinda CCM nalo ni kosa kubwa. Kwanini basi wasilipwe na ccm badala yake watumie kodi zetu kwa maslai ya ccm?

  Nchi hii siyo ile ya miaka ya 1970 kwamba unaweza wapeleka Watanzania kama unavyotaka,s asa tumeamka na tunajua lipi kimba na ipi keki; CCM na viongozi wake wasidhani haya wanayofanya leo huko mbele watakua salama wananchi uvumilivu utatushinda baada ya kuona viongozi wa serekali wakilipwa posho na mishahara kwa kazi za kushadadia CCM ktk chaguzi ndogo.

  MAGUFULI sio kiongozi bora tena, na sasa ni bora ajiuzulu. Kama Dr. Magufuli ulidhani unajenga tambua umebomoa na umejenga chuki miongoni mwa walipa kodi wa igunga.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ccm ilishapoteza mvuto muda tu wanachofanya sasa ni kulazimisha mambo.hilo liko wazi na wanalitambua wazi..
   
 3. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mbinu aliyotumia magufuli ndiyo mbinu pekee iliyobaki kwa ccm katika ulingo wa siasa.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  I second!!
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  ...Rais mtarajiwa toka Magamba 2015 inasemekana naye ni fisadi wa kutupa.
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Naona mmepata cha kuongea
   
 7. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mchwa akikaribia kufa, huota mbawa.
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Magufuli ni mwalibifu wa democrasia lakini pia ni mtu wa kwanza kwenda kinyume na sera pamoja na kanuni za utawala bora nchini;

  aliuza nyumba za serikali watu tukabaki kimya na yeye akajiona mjanja sasa anaamua kwa kutumia mabavu na cheo alichonacho kupanda jukwaani kuwatisha wananchi wasimchague kiongozi wanaomtaka;

  ni hatari tukiendelea na watu wa namna hii kwenye uongozi.
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ngonja wafu wajizike wenye
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi chadema wana bajeti ya kujenga madaraja, maana bajeti yao ilikuwa ni mapato 0 (kivuli).
   
 11. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hapana, ni wanachama wa CCM tu ndiyo wanalipa kodi.
   
 12. k

  kisimani JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ila Pinda nae si alisema ni kazi ya viongozi wa ccm kuhakikisha inashinda milele hata kama wanatumia kodi za wananchi kufanya hivyo? Sijaona PM mwenye upeo mdogo kiasi hichi jamani... Naomba aingizwe kwenye Geuness
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  naona huna neno isipokuwa kuwa mpole.
   
 14. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  System Sleeping At Work, serikali ndio inajenga madaraja sio chama cha kisiasa. Hapo ndio CCM hamjitambui na watu wamefunuka, itaendelea kula kwenu.
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wananchi ndio wanaojenga daraja kwa kutumia kodi yao na serikali ni kama msimamizi/mnyampala kwahiyo anapaswa kujitamba kwa ajili ya ujenzi wa daraja ni mwananchi/mtoa fedha na siyo mnyampala.
   
 16. M

  Mhamashiru Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hakuna Kipengele cha Kumburuza Mahakaman mtu kama Magufuli kwa kosa kama Hili?? Kwani ndo watajifunza na wengine,wataogopa!!! Otherwise 2015 ni Mbali mno
   
 17. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu upo?
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  namshangaa ''Maghufuli'' mpaka muda huu alitakiwa awe amejiuzulu.
   
 19. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  unamaanisha kwamba CDM wasichaguliwe kwa kuwa hawana bugjet?
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hahahaa Hamna jipya nyie
   
Loading...