Kwa kutumia dhana ya " product life cycle" kwenye siasa CCM na Chadema ziko katika hatua gani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,900
141,836
Naomba wataalamu wa masoko mnisaidie maana hivi vyama vya siasa vinajiuza kwa kunadi sera zao nasi tunanunua sera hizo kupitia mfumo wa ruzuku.

Mimi siyo market researcher lakini nimeona graph moja ikielezea stages katika product life cycle kama R&D, Introduction, Growth, Maturity na Decline.

Kwa kufikiri kwangu nikaona kama ACT wazalendo wako hatua ya 3 yaani Growth
Nikaiona CCM ikiwa stage ya 4 yaani Maturity
Na " nikadhani" Chadema wako stage ya 5 yaani Decline.

Naomba wataalam wa Marketing mje hapa kunielimisha tafadhali ili nisiteseke na chama changu pendwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa hali niliyoiona kwa macho yangu Leo Kule Mabibo Mwisho NIT, CCM wakae vizuri....CHADEMA bado ina watu wengi sana na wako fearless and determined!
 
CHADEMA ipo kwenye Obsolete Stage..hakuna jipya, watu wameichoka..inachungulia shimo la NCCR Mageuzi.

CCM ipo kwenye Rejuvenation Stage...true phase of "Kujivua Gamba", new hope of the nation..
 
CHADEMA ipo kwenye Obsolete Stage..hakuna jipya, watu wameichoka..inachungulia shimo la NCCR Mageuzi.
CCM ipo kwenye Rejuvenation Stage...true phase of "Kujivua Gamba", new hope of the nation..
Duh......ahsante kwa misamiati ya kimasoko!
 
CHADEMA ipo kwenye Obsolete Stage..hakuna jipya, watu wameichoka..inachungulia shimo la NCCR Mageuzi.
CCM ipo kwenye Rejuvenation Stage...true phase of "Kujivua Gamba", new hope of the nation..

Ccm sio chama cha siasa bali ni taasisi ya dola iliyojivika koti la chama cha siasa. Chama kina zaidi ya miaka 40 lakini bado kinategeme mbeleko ya dola kufanya siasa, hicho ni chama au kikundi cha kijeshi kinachofanya siasa?

Hiyo CHADEMA inayohujumiwa kupitia madaraka ya rais, hairuhusiwi kufanya siasa na wapambe wanajidanganya imekufa, lakini ikipewa nafasi hata ndogo tu ya kufanya siasa nyomi kama lote.
 
Mrudishen dr Slaa na apewe uenyekiti Chadema izaliwe upya

Hakuna mzee anaweza kuleta mabadiliko, ukiona watu wanategemea kuletewa mabadiliko na watu walioko 70+ basi ujue hiyo jamii imekufa.
 
Back
Top Bottom