Kwa kusulubiwa Lowassa, CCM ilipona! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kusulubiwa Lowassa, CCM ilipona!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Dec 24, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Siku zote huwa Najiuliza ni kwa nini Kamati ya Mwakyembe iliyoundwa kufatilia sakata la Richmond haikuwahi kumhoji Laig'wanani Edward Ngoyayi Lowasa?

  1. Je Kamati iligopa Majibu ya Lowasa?
  2. Je Spika aliyeshindwa kutetea kiti chake Mh Sita aliamua kuitumia Kamati Kummaliza Laig'wanani Lowasa na Mbio zake za Urais 2015?
  3. Je kitu gani ambacho akina Mwakyembe walikificha ili Kuisitiri CCM na Serikali yake? Je hicho kitu si kwamba kilikuwa kimuumbue Mkuu wa Kaya lakini Laig'wanani Lowasa akaamua Kufa kwa ajili ya Mkulu?
  4. Je Watanzania tuna Haki ya kudai kile kilichofichwa na Kamati ya Mwakyembe kiwekwe wazi maana hawa jamaa walitumia Kodi zetu kwenda Mpaka Marekani kufuatilia Richmond

  Je Ni Kweli Kwamba Laig'wanani aliamua kusulubiwa ili CCM Isianguke?

  Nawasilisha
   
 2. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naiunga mkono namba 4.
   
 3. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ile kamati ilikuwa ina agenda moja kuu, kummaliza Lowassa, we jiulize kwa nn haikumpa nafasi ya kujitetea, na mpaka Leo akijaribu kujisafisha Mwakyemba na Sitta wanakuja juu!
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Walichoficha ni ule ushahidi wa maandishi wa Lowasa kumshinikiza Msabaha afanye kila awezalo ili richmond wapewe tenda japo hawakuwa na uwezo.
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  LOWASSA hakuchafuliwa na Kamati ya Mwakyembe,kwa sababu tayari alikuwa mchafu,akiwa na utajiri usioelezeka!
  Lakini,wakina Mwakyembe hawakumtendea haki Lowassa kwa kutomhoji,hivyo kuonekana wanasiliba matope kwenye
  nguo chafu za Lowassa!
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi Great Thinker kwa Akili yako akina Mwakyembe wangekuwa na Ushahidi wa Kimaandishi wa Kuimplicate Laig'wanani Lowasa wangeacha Kuutoa Hadharani kweli? Hebu kifikirishe kichwa chako

  Naamini kabisa akina Mwakyembe kuna kitu walikuwa hawataki kukisikia kutoka kwa Laig'wanana Lowasa. Je kitu hicho nini?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je Unafikiri walikuwa hawajui kwamba walitakiwa Kumhoji Laig'wanani Lowasa?
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa China, Sitta na Mwakyembe wangekuwa wameshanyongwa.
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Najua Hizi Nondo Madhabiki wa Sitta lazima Wanyai
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na ingekuwa Saudi Arabia Lowassa na mijizi myenzake na walamba viatu wake Kama wewe mngekuwa mmeshakatwa mikono na kuuawa kwa mawe.

  Kwa ujinga wenu mnadhani mnaweza kurudisha gurudumu na kujiondoa kwenye kongwa hili mlilojivika? Huwezi kuwa na keki na wakati huo huo unataka kuila. Lowassa ni muoga na anajua alivyookoa Ainu yake kwa kukimbilia kujiuzulu ili kuua noma maana alijua kwamba ule ulikuwa ni wizi alioubuni na kuuratibu.

  Lakini tujiulize tena. Kwa nini mke wake Lowassa alikwenda kupiga magoti kwa Mwakyembe ili asifichue siri zaidi? Hivi Lowassa alikuwa na haraka gani mpaka asisubiri mjadala wa hoja na yeye ajitetee na kumwaga anayoyajua kuhusu sakata hili. Kwa nini alikosa ujasiri Rais huyu mtarajiwa? Hivi mnayemfanya badge hapa nani? Kwa taarifa yenu JF silo maliwato ya kusafisha wafu wa kimaadili Kama Lowassa!
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tayari umejipambanua kwamba kumbe wewe ni shabiki wa Lowassa aliyesukumwa na ushabiki badala ya utashi na uzito wa hoja. You can take this to the bank: Lowassa ni mzigo wa mavi ambao haubebeki na hata ukibebeka haupokeleki. Mnaweza kuchagua kutwanga maji kwenye kinu lakini watanzania wamesham-delete. Labda mpindue nchi.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mtatukana dini za watu ni mtu mmoja tu alisulubiwa kwa imani....yesu kristo acha matusi ya kumfananisha Yesu na Lowassa
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Lowassa alijimaliza mwenyewe kwa kukaa kimya muda mrefu hakuna anayehitaji kumsikiliza sasa wakati tulimuomba sana atueleze anachojua kuhusu kashfa ilimwondolea Uwaziri Mkuu
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  JK hukumbeleka mahakamani lowassa watetezi na wafuasi wake wanaleta dhihaka dhidi yako
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wafuasi wa Lowassa wana roho ya paka hawakati tamaa kumpigania kawapa nini hadi mnataka kumfia?
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,175
  Trophy Points: 280
  Mbopo hata kama hukubaliani na Lowassa, hivi kweli kuna ulazima wa kutumia neno hili? "Lowassa ni mzigo wa mavi ambao haubebeki"!.

  Just imagine kama kila asiyemkubali JK naye angepost " ... ni mzigo wa mavi ambao haubebeki"! How does it sound?.

  Pamoja na tofauti zetu na viongozi wetu, tunapaswa kutumia lugha za staha hata kwa tusiowapenda au kuwakubali!

  What goes around, comes around!, Nape alipomshutumu Lowassa, UV CCM walimtimua na aliokolewa na huruma ya JK, baada ya Nape kupata cheo, UV CCM wamenywea, ila Nape sasa ndio akautumia mwanya huo kupuliza vuvuzela za kuvuana magamba ili kummaliza kabisa Lowassa!. Hebu subiria uchaguzi wa 2012 kama hutashuhudia Nape akitafuta pa kutokea!.

  Kumbuka lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu linawezekana!

  " Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"!

  Wewe Mbopo wewe, utageuka mzigo wa mavi ambao haubebeki!.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,175
  Trophy Points: 280
  Gagnija, hakuna ubishi Lowassa alishinikiza kwa all sorts of vimemo etc, etc, ila jee unajua aliyafanya yote haya kwa niaba ya fulani?.
  Concetration ni kwenye action (vimemo), na end result (richmond kupata tenda), lakini ni wachache wanatazama the motive behind vile vimemo, the underlying factors ambazo ndizo causative agents!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,175
  Trophy Points: 280
  Kuna sheria kuu kuliko zote inaitwa Law of the "Karma", ambayo inasisitiza malipo ni hapa hapa duniani!
   
 19. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanapakula kwa kupakatwa wanajulikana kwa hoja zao.
  Wanajulikana.mavuvuzela nao wanajulikana tu kwa hoja zao. Wewe pasco ni pork.mean hoja zako.
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hivi kusulubiwa ndio kule? Mbona hana jeraha? Pilato pamoja na kugwaya mbele ya Yesu, alisulubiwa. Mbona nec iligwaya mbele ya lowassa na akafanikiwa kuchoropoka?
   
Loading...