Kwa kusimamisha wagombea wawili wa urais, Je ccm imevunja katiba?

GodfreyTajiri

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
981
652
wana jf, kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja tumesikia madai ya ccm kwamba dr. slaa ni
mwanachama mwenye kadi (inayolipiwa) wa ccm. pamoja na mengi yanayozungumzwa
kuhusu hili lipo jambo ambalo naona wengi hawalizungumzii. nalo ni hili,

kwa kukiri hadharani kwamba dr. slaa ni mwanachama wa ccm, chama hiki tawala kinakiri
kwamba katika uchaguzi wa 2010 ccm ilisimamisha wagombea wawili wa urais ambao
ni wanachama wa chama hicho. binafsi hili naona ni tatizo kubwa ambalo tume ya uchaguzi
inabidi iingilie kati na kutangaza kwamba uchaguzi wa 2010 ulikuwa batili.

aidha kama ccm itadai dr. slaa si mwanachama wa ccm ila alikuwa analipia kadi yake tuu,
basi itabidi ccm ikiri kwamba ilikuwa inajipatia mapato isivyohalali kwa kupokea pesa za
kadi kutoka kwa raia ambaye si mwanachama wake. hapa itabidi warudishe pesa zote za malipo
ya ada ya "uanachama" wa dr. slaa.

tafadhali wataalamu wa katiba na sheria za uchaguzi tusaidieni katika hili.
 
Tulishasema kuendelea kujadili hili swala la kipuuzi ni upuuzi.ngoja na mimi niishie hapa nisijeitwa mpuuzi.
 
Pia muulize Padri muasi kwa nini alijificha kama ana kadi mpaka alipoumbuliwa na Nape? Kwa nini anaitunza na kulipia kadi kama yeye si mwana CCM, najua huna ubavu wa kumpinga mwenye ubavu huo ni Mmoja tu Naibu wake wengine nyie ni ndio mzee!
 
Mdau hapo juu anaongea kitu chenye maana kubwa, kama kweli dk. Slaa alikuwa mwanachama halali wa CCM tangu 2010 basi uchaguzi ule ni batili. Na vyama vyote vinatakiwa kuwajibishwa.
 
Mtu akikwambia jambo la kijinga,huku akijua kwamba anachokuambia ni cha kijinga nawe ukakubali basi atakudharau (Mwl.Nyerere:1995). Bila shaka Nape anawadharau sana mlioacha kujadili kuhusu mpango wa uranium,gesi na katiba mpya na hatimaye kuangukia kwenye kujadili watu binafsi bila shaka mnajidhalilisha.Kwa akili ya Nape ni sahihi kumjadili mtu sana kuliko wanyamapori wanaoporwa kila siku...Tanzania haina maslahi ya kudumu na Dr.Slaa ila na maliasili zake.Fungeni mjadala huu wa kipuuzi tuendelee kujadili misingi ya kuimarisha nchi miaka kwa mingi ijayo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
We better put an end to the discussion about this KADI thing
kweli hii takataka ingefungwa kwani inatukosesha amani humu JF aliyeianzisha hii thread amejitaja kuwa ni Makupa leo kaikamata Nape basi nchi nzima na hasa CDM hawalali au kuangalia kazi yao ya kuikosoa Sreikali na CCM wanazamia kwenye kadi tu,
Leteni mambo ya kuishtua Serikali km ipo usingizini au inapotea kuliko hii kadi kwani ni hal;ali yake Dr Slaa kuwa nayo
Mimi nina Kadi za vyama v3
 
Last edited by a moderator:
wana jf, kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja tumesikia madai ya ccm kwamba dr. slaa ni
mwanachama mwenye kadi (inayolipiwa) wa ccm. pamoja na mengi yanayozungumzwa
kuhusu hili lipo jambo ambalo naona wengi hawalizungumzii. nalo ni hili,

kwa kukiri hadharani kwamba dr. slaa ni mwanachama wa ccm, chama hiki tawala kinakiri
kwamba katika uchaguzi wa 2010 ccm ilisimamisha wagombea wawili wa urais ambao
ni wanachama wa chama hicho. binafsi hili naona ni tatizo kubwa ambalo tume ya uchaguzi
inabidi iingilie kati na kutangaza kwamba uchaguzi wa 2010 ulikuwa batili.

aidha kama ccm itadai dr. slaa si mwanachama wa ccm ila alikuwa analipia kadi yake tuu,
basi itabidi ccm ikiri kwamba ilikuwa inajipatia mapato isivyohalali kwa kupokea pesa za
kadi kutoka kwa raia ambaye si mwanachama wake. hapa itabidi warudishe pesa zote za malipo
ya ada ya "uanachama" wa dr. slaa.

tafadhali wataalamu wa katiba na sheria za uchaguzi tusaidieni katika hili.
tunajua chadema ni ccm b. that is clear. hakuna cha ajabu hapo, hivi huoni hata vyombo vya habari vivyoibeba kama ccm? huone mpaka usalama wa taifa unawatumikia pia? mwenye macho haambiwi tazama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom