Kwa kumuapisha Shein Wamevunja Katiba ya Muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kumuapisha Shein Wamevunja Katiba ya Muungano?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 5, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa vile Katiba ya Muungano inasema kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakoma kuwa Makamu kati ya sababu nyingi ni hii:

  Kwa maana hiyo kwa vile hadi sasa Rais mpya na makamu wake hawajaapishwa na kwa vile sote tunakubaliana kisheria kuwa bado Kikwete ni Rais halali (kwani naye Urais wake wa miaka mitano unakoma pale atakapoapishwa kwa miaka mingine mitano) hivyo Dr. Mohammed Shein bado ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano - kwani namna nyingine zote za kuuondoa Umakamu kwa Mujibu wa Katiba hazihusiki


  Na kuwa Katiba ya Muungano inatangulia kusema kuwa:


  Sijui inawezekana kuwa sasahivi:

  JMT - haina makamu wa Rais kwa vile aliyekuwa Makamu wa Rais ni Rais wa Zanzibar? Kama ni kweli, amepoteza umakamu wake vipi wakati Rais mpya na Makamu wake hawajaapishwa bado?

  Kulikuwa na haraka gani ya kumuapisha Rais wa Zanzibar wakati bado ni makamu wa Jamhuri ya Muungano? Labda ninausingizi kuna kitu kimenipitia, naomba msaada.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hahaa sheria za bongo utaziweza? Yaani ni shaghala bin baghala
   
 3. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The loophole is the 'huo huo' part.

  I do agree though, CCM shouldn't be allowed to govern either territory.
   
 4. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu MM, ukiwabana sana watakuambia alishajiuzulu kwani kifungu cha 50: (2c) cha Katiba ya JMT kinaruhusu nafasi ya Makamu wa Rais kufikia ukomo kwa kujiuzulu.

  Kwa kuzingatia kuwa umeibua hoja hiyo kwa sasa inawezekana barua ya kujiuzulu inaandaliwa haraka ili iingizwe kwenye file.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mmh.. mbona hawakutuambia kajiuzulu maana baada ya kujiuzulu Kikwete alitakiwa ateua Makamu mwingine..ambaye angetakiwa apitishwe na Bunge. Fikiria kwa mfano, Mahakama isitishe kutangaza matokeo ya Urais ili kesi iweze kuangaliwa... itakuwaje? Au labda mimi nimekosea kuwa Kikwete sasa hivi siyo Rais?
   
 6. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watakuambia bado hajakiuka katiba kwani Kifungu cha 50:4 kinampa siku 14 kufanya uteuzi wa mtu mwingine. Kwa vyovyote kama wataandika barua ya kujiuzulu itakuwa siku moja ama mbili kabla ya kuapishwa kwake kuwa Rais wa ZNZ
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ndo tatizo la dhuruma wamemwapisha fasta fasta ili kufunika kombe mwanaharamu apite
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji. Heshima kwanza.

  Hivi uliona Post iliyokuwa na "Orodha ya Wabunge Vihiyo wa CCM"?

  Tuna aina ya viongozi ambao ni wakurupukaji na washauri ambao hawana shule.

  Safari ni fupi. Tutafika tu.
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sheria za katiba zina utaalamu wake. kmbuka hii si mara ya kwanza kuwa na situation kama hiyo.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mgombea Ubunge.. kuwa "si mara ya kwanza" haina maana ni halali.. labda unisaidie kwa kutumia utaalamu wa Katiba uliopo kuelezea kilichofanyika kinakubalika kwa misingi ipi. Nataka kujifunza.
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji mambo ya Tanzania wewe acha tu. Niliwahi kuuliza kuwa mgombea mwenza wa Kikwete, Dr. Gharib Bilal anatumia kifungu gani cha katiba kutoa maagizo kwa vyombo vyetu vya dola na Usalama. Nilijiuliza ni vifungu gani vya katiba vinamruhusu kupata protokali alizokuwa anapewa kwenye kampeni, sikupata jibu. Kwa Tanzania CCM ni dola na ukishakuwa kiongozi ndani ya CCM, unakuwa kiongozi wa serikali na ukiwa kiongozi wa serikali moja kwa moja unakuwa msemaji wa CCM. Ndio maana Makame, JWTZ na sasa Usalama wa taifa nao wametumbukia wanapigana vikumbo katika kuwajibia CCM. KATIBA ?
  Labda ya CCM na mafisadi.
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani viongozi wetu wa siasa hawaaminiani kabisa ndio maana wanavunja baadhi ya sheria, kanuni na taratibu kama ilivyofanywa hapo.

  Maana, si ajabu kulikuwa na hisia kuwa, endapo asipoapishwa mapema, wapinzani wangeweza kubadili msimamo na kudai kurudiwa kwa uchaguzi. Kwa kumuapisha mapema, wapinzani wanakosa uwezo huo kwakuwa Katiba zinazuia kumshitaki Rais.

  Ndio maana huwa nasema kila mara kuwa, Katiba yetu haiwezi kutusaidia kabisa. Inatakiwa mgombea yeyote wa kiti chohcote cha kisiasa kuachia madaraka aliyonayo kwenye serikali mara baada ya kutangazwa kuwa mgombea wa kiti anachotaka kugombea. Hii iwe kwa kiti cha u-Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na unaibu waziri. Rais awe na jukumu la kuunda serikali ndogo ya kumsaidia kumaliza kipindi chake hadi atakapoapishwa Rais mwingine.
   
 13. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jibu ni Yes, black & white:
  Kama umechakachua kura, ustarajie utakuwa na muda wa kuangalia katiba. Uchakachuaji wenyewe ni kuvunja katiba, sasa hapo, msaada gani tutakupatia Mwanakijiji. Majibu yako obvious!!
   
 14. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani wadau ni hapo tu ndio sheria inakiukwa,mbona ni kila mahali kwa kila kitu watawala wakitaka wao inakuwa tu.Mbona utawala wa sheria haupo,labda watatuletea sheria ya utawala na nina uhakika hiyo wataitii na kuiheshimu kwani itawasidia kwenye malengo yao ya kumdidimiza mwananchi.
   
 15. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa ni kwamba hatuna Mahakama ya Katiba, hivyo panapotokea uvunjifu wa katiba na viongozi wa serekali inakua kazi kubwa kushughulikia hilo swala, maana hata hiyo mahakama kuu bado haiko competent sana ukiangalia kesi ya Mtikila kuhusu mgombea binafsi.
   
 16. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  It is true, katiba imevunjwa, ila for a good faith.
   
 17. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, pole sana. Tanzania hakuna katiba. kama ingelikuwepo mambo mengi yangelikuwa sawa. Je wadhani kwa hali ilivokuwa Unguja wangelichelewesha masaa hata mawili pale? thubutuuu.... Punda afe mzigo wa bwana ufike.:thinking:
   
 18. F

  Ferds JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  tatizo sheria zetu zina clw bck clauses, yaani we ukisema katiba, kumbe kuna ka Act suppliment kanampa pawa mtu kama huyo, yaani tumepewa na mkono wa kulia halafu wanakupora kwa mkono wa kushoto., ngoja niperuzi hako ka supliment nikikapata nitakupostia mzee mwanakijiji
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,905
  Trophy Points: 280
  i like this one .napata matumaini
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Katiba ya JMT kwa masuala yanayoigusa Zanzibar imekuwa kama haipo vile. Wanaposema Zanzibar ni NCHI katiba ya JMT haisemi hivo. Walipompigia mizinga 21 Rais Karume kumuaga walikuwa na maana gani? Juzijuzi hapa tumeona Karume anawapa kamisheni wanajeshi wa vikosi vyake eti naye sasa Amiri Jeshi wa Vikosi vya Zanzibar! Makubwa zaidi yanakuja. Wewe subiri serikali mpya zianze kazi wiki ijayo.
   
Loading...