Kwa kumsafisha Chenge, Kiongozi wa TAKUKURU ajiuzulu.

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
PCCB Chombo kilichoundwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa kimekosa rasmi uhalali mbele ya macho ya watanzania kwa kuwapamba wala rushwa. Kwa mara ya kwanza PCCB iliwasafisha Richmond kuwa mkataba wao wa kuzalisha umeme haukuwa na matatizo yoyote. Muda mfupi baadaye uchunguzi wa bunge ukagundua kuwa makataba kati ya serikali na Richmond ulikuwa umegubikwa na rushwa. Kama hiyo haitoshi kampuni hiyo ya Richmond ilifahamika rasmi kuwa ni feki na wala haikuwa imesajiliwa Marekani. Hilo likawa kosa kubwa la kwanza kwa TAKUKURU na wananchi wakaanza kupoteza imani na chombo hicho.

Sasa wiki hii PCCB ikatoa taarifa kuwa uchunguzi wa TAKUKURU na SFO umethibitisha bila shaka kwamba Chenge hana hatia ya rushwa. Cha kushangaza Uingereza kwa haraka haraka imekana kwa barua ya kiofisi kuwa si kweli kuwa Chenge amesafishwa na SFO kwa kuhusika kwake na rushwa ya ununuzi wa RADA. PCCB sasa imegeuka kuwa chombo cha kusafisha wala rushwa tena wakubwa, wala rushwa papa badala ya kupambana nao. Watanzania tunajiuliza kuna umuhimu gani kwa taasisi kama hii kuwepo?. Mafunzo wanayopata ya kupambana na rushwa yanawasaidia nini kama wanaendeleza kupoteza pesa za walipa kodi kwa kuipamba rushwa?. Kwa nini watanzania tuendelee kulipa kodi kuhudumia taasisi inayopamba rushwa badala ya kupambana na rushwa? Bunge la mwaka huu nina imani watakimulika chombo hiki na kuandaa utaratibu wa kukivunja kwa manufaa ya umma.
 
Takukuru osiha kaka umshikwa maskio? Unajidhalilisha mjomba achia tu ngazi umeingia kwenye historia mbaya kunatofouti gani kati ya wewe na watemi waliouza vijana wao kwa waarabu? Osea osea unazeeka vibaya
 
Takukuru osiha kaka umshikwa maskio? Unajidhalilisha mjomba achia tu ngazi umeingia kwenye historia mbaya kunatofouti gani kati ya wewe na watemi waliouza vijana wao kwa waarabu? Osea osea unazeeka vibaya

Weee kwa katiba hii mbaya tuliyonayo haaachi mtu ngazi. Cheki Kenya kiongozi anakashfa anakaa pembeni mpaka suala lake liishe, Tanzania bado. Hii sio taasisi ya kuzuia Rushwa bali ni taasisi ya kupamba na kukuza rushwa. So do not expect any mirracles from Hosea and Co.
 
Weee kwa katiba hii mbaya tuliyonayo haaachi mtu ngazi. Cheki Kenya kiongozi anakashfa anakaa pembeni mpaka suala lake liishe, Tanzania bado. Hii sio taasisi ya kuzuia Rushwa bali ni taasisi ya kupamba na kukuza rushwa. So do not expect any mirracles from Hosea and Co.
Kibaya zaidi inagharimiwa na kodi zetu WOTE wakati inafanya kazi za mabwana wao CCM. Inakera sana! Mi sioni tija ya hili LIHOSEA (I mean TAKUKURU) linatuongea gharama tu lingefutwa ili hiyo akina Hosea na wenzake watie akili.
 
Mh rais alitakiwa kuotesha kibarua cha mtu mara moja.

Sorry nimesahau kwamba Yeye ni Fisadi namba 1 :first:

Haya ndiyo mambo yanayotufanya tupende kuwa ma SNIPER.
Unafinyatua moja tu yenye kiwambo hadithi inafungwa pale pale.

Mijitu kama hii inafaida gani?
Kabla uongo wa kwanza haujapoa inadanganya kwa mara nyingine.
 
Waheshimiwa Wabunge, nawaomba mpitishe muswada wa kuivunja TUKUKURU na kuwastaafisha maafisa wake watendaji kwa manufaaa ya umma, haraka inavyowezekana.
 

Inashangaza sana kusikia kuwa HOSEA hadi sasa hivi bado yuko ofisini. Takukuru ni mzigo usiobebeka kwa watanzania, kumbuka kuwa wana ofisi kila wilaya wakilipwa mishahara, na gharama kubwa wanazotumia kusafisha watendaji wabovu wa serikali ya ccm, kwa kodi za wananchi. Kweli Takukuru inatia kinyaa.
 
DGeneral.JPG

Edward Hosea.

Takukuru is just a group of very lazy-thugs and irresponsible-vandals occupying the GOVERNMENT office, and wasting our resources in the name of finances!
Mfumo wa kifisadi ni mbaya jamani...JK anaona haya yote lakini hawezi kutamka neno, maana ana'cling kwenye mfumo huo, ambao unamcontrol pia. Zaid atasema kuwa wazungu ni wanafiki etc!...this is seriously shameful to JK!
 
Kama kuna asasi zimelitia taifa hasara na kulihaini ni asasi mbili; nazo ni Usalama wa Taifa (TISS) ambao mara kadhaa wametumika kuficha hila za kuliangamiza taifa badala ya kuliokoa! Nashindwa kuelewa ni vipi uhalifu mkubwa kama wa mitakaba hatari kwa maisha ya watanzania kama ya EPA, Richmond, IPTL, Meremeta, Buzwagi , Kagoda na mingine lukuki yenye madhara makubwa kwa taifa letu ifanikiwe bila ya kuchukuliwa hatua na Intelligence organ hiyo. Ninavyofahamu intelligence and security work inahusisha viashirio vya maafa kwa taifa hata kama si ya kutumia silaha. TISS wamejikita kwenye kuwalinda viongozi hata wanapolihaini taifa kwa kufanya vitendo ambavyo ni potentially catastrophic kama vya kuingia mikataba mibovu, kuiba kura, kuruhusu magari na vitendea vyao kutumika kwa shughuli zisizo rasmi na tija kwa taifa kama hivi karibuni ilivyoshuhudiwa magari yao na ya ikulu kubandikwa namba za kiraia na kutumika na familia ya mgombea urais mmoja.
Na kuhusu TAKUKURU ndiyo kabisaa; yaelekea shughuli wanayoifahamu vyema ni kuwa - flag na kuwasafisha wala rushwa wakubwa na si kuzuia. Uhalifu uliofanywa na taasisi hii katika uchunguzi wa Richmond na sasa hii ya "kumsafisha" Chenge ni vielelezo wazi katika hili. Taifa limeingia katika aibu nyingine kubwa kutokana na kitendo cha asasi hii kukurupuka na kujaribu kumsafisha Chenge, na muda mfupi baadae Ubalozi wa Uingereza kukanusha jambo hilo hilo! Ni kutokana na nchi yetu kukosa utamaduni wa kuwajibika, vinginevyo kwa mara nyingine tena Mkuu wa taasisi hiyo alipaswa kuwajibika kwa kuachia ngazi kwa asasi yake kuliaibisha taifa kiasi hicho.

Kwa mitaji hii TISS na PCCB zimepoteza moral authority mbele ya macho ya watanzania na wanaonekana kama part of the existing problems. Njia pekee ya kurudisha imani kwa wananchi ni kumpata kiongozi atakayekuwa na guts za kuvunja vyombo hivi na kuviunda upya.
 
Mimi nina wasiwasi na usafi wa mtukufu,huyu jamaa anapamba rushwa badala ya kupambana nayo,na yeye yuko pale anamuona,kweli kama hana uchafu kwanini asimuondoe?au ni hii tabia ya viongozi wetu kutudharau?
 
Nimesikia magazeti asubuhi ya leo Uingereza wamegoma na wanadai Takukuru hawasemi kweli more info please
 
Nijinsi gani chombo kama pccb kinaweza kukumbatia mafisadi!wakati kipo kwa ajili ya wananchi kinachoonekana nikwamba kesi nyingi zinazokihusisha chombo hicho zina walakini kwa sababu kipo kwa maslahi ya watu wachache inasikitisha na zaidi ina mshushia heshima Rais kwani chombo hicho kipo chini ya ofisi ya rais Aibu gani kwa serikali ya Tanzania!!Namshauri Kikwete Ampangie kazi nyingine E.Hosea labda kama yeye mwenyewe alilidhia kumsafisha Chenge!Bila hivyo amemtia doa kwenye serikali ya wingereza na (EU)na kimataifa!
 
Nilishasema TAKUKURU ni chafu. Niliwahi kuwemo nikatoka, najua kilichomo. Jamani kwa wenye jamaa, marafiki na ndugu wanaofanya kazi TAKUKURU hamuoni wanavipato ambavyo vinamashaka? Wale jamaa si wapambanaji na rushwa ni kweli wapamba rushwa, wanakula rushwa wale!
Angalia sasa wanavyouumbuliwa! Kasfa Rada na Richmond zinaonyesha TAKUKURU ni wahuni na wahaini. Kwa kuwa ni Tz, watazidi kuendelea na uchafu wao bila woga.
 
Kweli nimeamini ule msemo kuwa Watanzania waliowengi hasa wa bara ni Wadanyanyika na mbumbumbu. Katika nchi za wenzetu mkate ukipanda bei tuu sekeseke lake usiombe,sisi hapa mambo ya msingi kama PCCB kutoa tarifa za kumbeba mtu ambaye ananuka rushwa Wadanganyika tunakenua meno na kubaki kulalamika. Nahisi aliyetuloga amefunga akili zetu na funguo kishaakazitupa baharini. Mungu tunakuomba uingilie kati Wadanganyika wataisha. Inaniumaaaaaaaaa sanaaaaa.
 
It's another group of thieves, robbers, law-brokers and the list goes on, it's real sad and i feel like crying, laughing all at the same time. But we're going somewhere coz all their(TAKUKURU,CCM) dirty works, incompetence are now to the public judgment. I hate their deeds deeply, they need to be purged from the public offices (Dr Hosea and his crew) and CCM as the party at large, coz they have ears and they can't hear, they have eyes and they can't see are dead walking corpses
 
It's another group of thieves, robbers, law-brokers and the list goes on, it's real sad and i feel like crying, laughing all at the same time. But we're going somewhere coz all their(TAKUKURU,CCM) dirty works, incompetence are now to the public judgment. I hate their deeds deeply, they need to be purged from the public offices (Dr Hosea and his crew) and CCM as the party at large, coz they have ears and they can't hear, they have eyes and they can't see are dead walking corpses

.........And citizens who have the power to vote them out, they vote them in instead.
 
TAKUKURU ilitoa taarifa ya kumsafisha Chenge kuhusu kashfa ya Rada wakati taarifa yake imepingwa na Ubalozi wa Uingereza.Hii waliifanya tena wakati wa sakata la Richmond, je sasa si wakati wa Kiongozi wa TAKUKURU kujiuzulu na taasisi hiyo kuvunjwa na kuundwa upya na kudhibitishwa na Bunge?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom