Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
PCCB Chombo kilichoundwa kwa ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa kimekosa rasmi uhalali mbele ya macho ya watanzania kwa kuwapamba wala rushwa. Kwa mara ya kwanza PCCB iliwasafisha Richmond kuwa mkataba wao wa kuzalisha umeme haukuwa na matatizo yoyote. Muda mfupi baadaye uchunguzi wa bunge ukagundua kuwa makataba kati ya serikali na Richmond ulikuwa umegubikwa na rushwa. Kama hiyo haitoshi kampuni hiyo ya Richmond ilifahamika rasmi kuwa ni feki na wala haikuwa imesajiliwa Marekani. Hilo likawa kosa kubwa la kwanza kwa TAKUKURU na wananchi wakaanza kupoteza imani na chombo hicho.
Sasa wiki hii PCCB ikatoa taarifa kuwa uchunguzi wa TAKUKURU na SFO umethibitisha bila shaka kwamba Chenge hana hatia ya rushwa. Cha kushangaza Uingereza kwa haraka haraka imekana kwa barua ya kiofisi kuwa si kweli kuwa Chenge amesafishwa na SFO kwa kuhusika kwake na rushwa ya ununuzi wa RADA. PCCB sasa imegeuka kuwa chombo cha kusafisha wala rushwa tena wakubwa, wala rushwa papa badala ya kupambana nao. Watanzania tunajiuliza kuna umuhimu gani kwa taasisi kama hii kuwepo?. Mafunzo wanayopata ya kupambana na rushwa yanawasaidia nini kama wanaendeleza kupoteza pesa za walipa kodi kwa kuipamba rushwa?. Kwa nini watanzania tuendelee kulipa kodi kuhudumia taasisi inayopamba rushwa badala ya kupambana na rushwa? Bunge la mwaka huu nina imani watakimulika chombo hiki na kuandaa utaratibu wa kukivunja kwa manufaa ya umma.