Kwa kumng'o Mubarak sawa ila kubaka Siwaungi Mkono hata kama ni Waislam wenzangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kumng'o Mubarak sawa ila kubaka Siwaungi Mkono hata kama ni Waislam wenzangu!

Discussion in 'International Forum' started by Arafat, Feb 16, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mwana-mama Lara Logan ambaye alikuwa aki-cover taarifa mbalimbali za Maandamano ya Wamisri katika kuukataa Utawala wa Mubaraka Alitekwa katika eneo la Tahrir square na Wanaume wapatao 200 na kumbaka pamoja na kumpa vipigo; Lara amefanya kazi nyingi za Habari Afghanistan, Iraq na Kosovo katika mazingira magumu wakati mwingine akifukuzwa kuwa labda ni Kachero wa Misri na huku akilaumiwa na kutengwa mara zote kwa kuwa si Muuislam, sasa ameishika katika kudharirishwa na hii Miislam yenzangu yenye Kichwa maji ambao wao kila siku jina la Kikristo uwatia kichefuchefu wakilisikia.

  Hata hivyo akiwa bado katika vipigo Lara alinusuliwa na kikundi cha wakina-mama na Askali Jeshi wapatao 20. Hivi sasa yupo Marekani kwa matibabu.

  Nalaani kitendo hicho kwa nguvu zangu zote na nina amini huo sio Uislam bali ni tabia na Ulka ya mtu binafsi, katika hili siungani na Waandamanaji waliomngÂ’oa Mubarak.

  Ugua Pole Dada yangu Lara, nakutakia upone haraka na kurudi kazini, hata hapa kwetu Kubena alimwagiwa Tindikali, ndio ukikubali kufanya kazi Mochwari husiogope maiti.
   
 2. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  maandamano ya misri yalikuwa ya wanamapinduzi toka dini zote mpaka na wale wasiokuwa na dini! sasa unaushahidi gani kama waliombaka huyo dada ni Waislamu? mbona Askari wa Serikali ya Mkapa waliowabaka akina Mama zetu huko Pemba na UNGUJA mwaka 2001 umewasahau? na unaemuona ni huyo Dada wa Kizungu tu?

  Yaani wewe unaguswa sana tendo la Mzungu kubakwa lakini kubakwa kwa Mama na dada zako wa Kitanzania unaona ni sawa sio? yaani ngozi nyeupe kubakwa ni haramu lakini nyeusi ni halali?
  tuache unafiki na tukemee machafu hapa kwetu kwanza kabla ya kurukia nchi zingine kwani hiyo ni tabia ya vimbelembele!!!!!!!
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Zubeda unao ushahidi kuwa maandamano yalikuwa na watu wa dini zote? au unatumia nguvu badala ya hoja! au unadhani dini yetu inafundisha uhalifu! la hasha sikubaliani nawe.

  Unaweza kutoa sababu yeyote ya maana kwanini laana ya ubakaji huo unakuudhi dada yangu? aliyekwambia nimelaani kwakuwa ni Mzungu ni nani? au wewe nimingoni wa hao waislam niliosema nawalaani? ebu fafanua!
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wabakaji washikwe na wapelekwe kwenye vyombo husika

  Uislamu hauhusiki na upuuzi..kwa hiyo araf usichanganye madawa.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Arafat,

  Nasikitika unatukosea adabu na wewe si muislamu kwani sidhani kama ungelikuwa muislamu ungeliandika haya. Vile vile kama ulivyojieleza katika thread zilizopita kuwa wewe ni msomi I am beginning to question your intellectual ability let me ask you a question umejuaje wale waliomshambulia huyu mama ni waislamu?? Pale Tahrir square kulikuwa na waislamu, wakristo, wapagani, wamatumbi sasa iweje ukawahukumu waislamu? Hebu soma taarifa hii:-  On 15 February 2011, CBS News released a statement revealing that Logan had "suffered a brutal and sustained sexual assault and beating" while covering the celebrations in Tahrir Square following the resignation of then President Hosni Mubarak some four days earlier.[19] CBS News indicated that she was overwhelmed by a mob, along with her camera crew and security staff: "It was a mob of more than 200 people whipped into frenzy. In the crush of the mob, she was separated from her crew. She was surrounded and suffered a brutal and sustained sexual assault and beating before being saved by a group of women and an estimated 20 Egyptian soldiers."[20][21] An unnamed source told the New York Post that she was "attacked for 20 to 30 minutes," during which the assailants were heard screaming, "Jew! Jew!"[22] Logan returned to her hotel after the assault and was flown out of the country within hours on a chartered network jet. She reportedly wasn't taken to a local hospital because the "network didn't trust local security there" and didn't report the assault to Egyptian authorities because they "couldn't trust them, either."[22] Upon returning to the United States, Logan was admitted into a hospital for recovery.[23]
  [24]


  Nampa pole huyu mama kwani sio kitu cha kufurahia ubakaji ila huwatendei haki waislamu na madai yako.
   
 6. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kubaka ni tabia mbaya na hulka za watu hicho kitendo nafkiri hakihusiani na dini yeyote na sidhani kama kuna dini yeyote duniani including islamic ambayo inaruhusu au kuhalalisha maovu kama hayo. Katika mkusanyiko wa watu takribani milion 3 kuna watu wa kila aina na tabia mbalimbali kwa hiyo katika huo mkusanyiko kulikuwa na wahuni na wabakaji ambao baadhi yao ndo waliofanya hicho kitendo na sio ulaumu uislam kam dini. Kama kuna umuhimu wa kulaumu laumu wazazi na viongozi wa dini ambao wameshindwa kuwafunda vijana wao ktk maadili au vijana wenyewe kwa kutoshika mafunzo so siku nyingine laumu watu binafsi na sio dini, dini kama dini haihusiki kabisa
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mdondoaji hapa tuna toa pole kwa Lara siyo kurushiana maneno, mi sija-husisha hili swala na Dini ila nyie wachangiaji ndio Mnatafsi zenu kila mmoja
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Topical kumtambua mhalifu kwa dini yake siyo kuhusisha uhalifu wake na Dini yake; Nadhani nyie ndio hamtaki kutoa pole badala yake mnalaumu, kwani pale Osterbay Polisi wahalifu huwa hawaulizwi Dini zao? Mi sijasema Dini imewatuma!
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ndugu Arafat, angalia haya maneno katika rangi nyekundu na haya au wewe nimingoni wa hao waislam niliosema nawalaani? uliyomwuliza Zubeda. Anyway, hapa tunazungumzia ubakaji ambao ni suala linalopaswa kulaaniwa kwa nguvu zote, bila ya kujali kama aliyetendewa ni Mzungu au Mwafrika, au aliyetenda ni muislamu au mpagani.
  Ninampa pole Lara na ninamwombea apone maumivu haraka, ingawaje taathira za kisaikolojia daima zitakuwa zinamwandama.
   
 10. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Lete ushahidi hapa kama dada na mama zako walibakwa huko Zenj !
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sawa kaka! ukitaka kuona Askari wa Mzee wako Mkapa kubaka dada na mama zangu huko Pemba soma hapa kama unaubavu: Ni ipi hatma ya demokrasia Tanzania baada ya

  Unaonekana wewe hujawahi kuishi Tanzania!!!
   
Loading...