Kwa kukubali yaishe seif amepoteza fursa kurejesha madaraka kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kukubali yaishe seif amepoteza fursa kurejesha madaraka kwa wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Nov 2, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kauli mbiu ya "mapinduzi daima," pamoja na mambo mengine inawakilisha dhana kwamba madaraka ya kuongoza nchi, milele na milele yatabakia mikononi mwa kundi dogo la Wazanzibari waliotwaa madaraka kufuatia mapinduzi ya tarehe 12/1/1964, na kizazi chao. Jambo hilo linadhihirishwa na uamuzi wa kuendelea kuiita serikali ya visiwa hivyo,"Serikali ya mapinduzi." Katika hali halisi, serikali iliyowekwa madarakani kwa ridhaa ya wananchi wenyewe kupitia kura zao, haiwezi kuitwa serikali ya mapinduzi.lakini kwa upande wa Zanzibar, wameendelea kutumia jina hilo, pamoja na ukweli kwamba tangu mwaka 1984 serikali ya Zanzibar imekuwa ikipatikana kupitia kwa kura za wananchi. Kwa wadadisi wa mambo, kuendelea kutumika kwa jina hilo la "Serikali ya Mapinduzi" kunahashiria jambo moja tu, nalo ni kwamba; mfumo wa demokrasia ya kiberali ulioanzishwa hapo visiwani, na mabadiriko ya katiba ya mwaka 1984, ni mpakakazo usio na maudhui, zoezi zima likiwa ni kuhadaa jumuiya ya kimataifa, ili iweze kuamini kuwa katika visiwa hivyo uongozi wa nchi unaingia na kutoka madarakani, kupitia sanduku la kura.Hata hivyo katika halisi mambo hayako hivyo. kwakuwa Seif ni mwadhirika wa mpakazo huo kwa mara tatu mfululizo, safari hii ameona vema akasalimu amri na achie harakati za kuleta demokrasia pana visiwani hapo kwa vizazi vijavyo.
   
 2. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  it seems there is a truth inside
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Jamani penye heri tusitie chumvi..
  km mwanaharakati mpinga udhalimu nilifuatilia mchakato mzima wa uchaguzi visiwani..kwa namna zoezi lilivyoendeshwa siwezi kutia neno sana ila matokeo yalivyoanza kutoka esp kwa Pemba nilidhani Dr Shein is fired..ila Unguja ndo hali imebadilika..tukubali,kwa kua hata km kuna mchezo mchafu ulichezwa umechezwa kiungwana kwa kua alofanya na kufanyiwa karidhia.
  Jina Mapinduzi ni la kawaida tu km mengine,ifike mahali tuangalie current situation kuliko kuhukumiwa na historia za ansestors..natoa hoja!
  Mungu ibariki Tanzania! umoja daima!
   
 4. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa unachozuungumza mkuu ni funika kombe mwanaharamu apite. Lakini mambo si laini kama unavyodhani. Maalim alivyomwambia Shein ".... hakuna kubezana" anlikuwa anajua mioyo ya Wahafidhina wa CCM. Angalia tu Matokeo yalivyo. CCM - Unguja, CUF - Pemba. Wapemba wamezidiwa kwa idadi tu na si utashi. Usijidanganye kirahisi hivi. Mgogoro wa Zanzibar si kati ya CCM na CUF, na wala si kati ya Unguja na Pemba, ni kati ya "Uunguja" na "Upemba". Na kwa taarifa yako, Uunguja na Upemba haujaanzishwa na CUF na CCM ila kwa kuwa kuna mambo ya habari huru siku hizi ndo maana unausikia sana. Ugomvi wao uko mioyoni mwao, utaisha pale kizazi fulani kitapoisha katika uso wa dunia.
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  HTML:
  [QUOTE]Hapa unachozuungumza mkuu ni funika kombe mwanaharamu apite. Lakini mambo si laini kama unavyodhani. Maalim alivyomwambia Shein ".... hakuna kubezana" anlikuwa anajua mioyo ya Wahafidhina wa CCM. Angalia tu Matokeo yalivyo. CCM - Unguja, CUF - Pemba. Wapemba wamezidiwa kwa idadi tu na si utashi. Usijidanganye kirahisi hivi. Mgogoro wa Zanzibar si kati ya CCM na CUF, na wala si kati ya Unguja na Pemba, ni kati ya "Uunguja" na "Upemba". Na kwa taarifa yako, Uunguja na Upemba haujaanzishwa na CUF na CCM ila kwa kuwa kuna mambo ya habari huru siku hizi ndo maana unausikia sana. Ugomvi wao uko mioyoni mwao, utaisha pale kizazi fulani kitapoisha katika uso wa dunia.[/QUOTE]
  Nadhani tuombe inayoitwa amani izidi kuwepo japo kinafki hivyo hivyo hadi kizazi hiki tupotee,nadhani mambo yatakaa sawa tu baadae..kuna tetesi nilizonazo kuwa baada ya wamarekani weusi wa enzi za 1960 kuona kwamba wamezidiwa sana na wenzao weupe ambao ni wengi kwenye vyombo vya kimaamuzi..walianzisha ushawishi kwa kila mweusi kuzaa angalau watoto kuanzia watatu na kuendelea,lengo likiwa ni kuongezeka na kua na maamuzi baada ya miaka 30 mbele..yet,tunaona matunda ya wazo hilo sasa..
  Maana yangu si kukubali yaishe,ila ndugu zetu hawa ni diplomasia na busara tu inaweza kumaliza mzozo wao..labda na hilo la kizazi kimoja kufutika kwanza! One love!
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mimi naona ni jambo jema sana kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu hakufa mtu Pemba.

  Tuwaombee ili ushirika wao uwe wa dhati siku zote zijazo.
   
Loading...