Cendy
JF-Expert Member
- Mar 28, 2015
- 1,249
- 2,307
Mwanafunzi wangu mmoja niliyemfundisha labour law ameniuliza swali hili, sijui alikuwa ananitega. Sikia,
Eti mwl, mwajiri wako anaweza kujiamulia tu kushusha mshahara wako kinyume na makubaliano yenu ya awali wakati mkataba wako haujafikia mwisho?
Nikatafakari, nikaona ngoja tu nimjibu bila kufikiria watanzania wengine wanawaza nini kwa sasa. Nikamwambia.
Katika sheria ya mahusiano kazini, mkataba wa kumwajiri mfanyakazi lazima uwe unaainisha haki zote za mfanyakazi na mwajiri ikiwemo wajibu wao kwa kila mmoja. Mwajiri hawezi kubadili masharti ya mkataba wa ajira katika vipengele vilivyokubaliwa wakati wa kuanza kazi mpaka afanye majadiliano na mfanyakqzi husika na makubaliano yafikiwe katika mahitaji ya mabadiliko yoyote pendekezwa.
Kama mabadiliko pendekezwa hayatakubaliwa na mfanyakazi na yakawa yanaathiri haki zilizokubaliwa awali wakati wa kuingia mkataba, huo utakuwa ni ukiukwaji wa mkataba endapo upande unaopendekeza mabadiliko utaamua kulazimisha kutekeleza. Hiyo italeta kitu kinaitwa DISPUTE OF RIGHT. Upande ulioathirika utaenda mahakamani kulalamikia kukiukwa kwa masharti halali ya mkataba, violations of terms and conditions of employment. This will be an action for a breach of contract.
Ila endapo mabadiliko pendekezwa hayahusiani na haki ambazo tayari zilikuwa zimeshakubaliwa awali, yaani ni maboresho ya maslahi zaidi ya kazi au kuongeza vitu vipya zaidi kwenye mkataba wa awali, hayo pia huhitaji majadiliano ila mkishindwa kukubaliana upande ulioathirika unaweza kuchukua hatua ya mgomo yaani Strike kwa mfanyakazi or Lock out kwa mwajiri, kushinikiza upande mwingine ukubali. Hii inaitwa DISPUTE OF INTEREST.
Kwahiyo mwanafunzi wangu, mwajiri hana mamlaka ya kukushusha mshahara kwa utashi wake tu kama mkataba wa ajira haumpi yeye mamlaka hayo. Anachoweza kukifanya, na hili nakuomba umfikishie bosi wako kama mnampango huo hapo ofcn kwenu kuwa, anaweza kusubiri mtumishi husika amalize mkataba wake, then atakapomwajiri mtumishi mpya ampe masharti mapya ya kazi yenye kiwango cha chini cha mshahara.
Pia kama mishahara hiyo ipo kisheria, anatakiwa afanye mabadiliko ya sheria husika kwanza ili kuweka ukomo na viwango vipya vya mishahara lakini mabadiliko hayo, kwa vyovyote vile hayawezi kuwaathiri wafanyakazi waliofaidika na sheria ya zamani kwani wao wataendelea na masharti yao kama kawaida. Mabadiliko hayawezi kuoperate retrospectively to affect substantive rights unless kiudikteta zaidi.
Basi mwanafunzi wangu akaamua kuniuliza swali ambalo sikulipenda, eti mwl sasa Rais anaweza kushusha mshahara toka m40 mpaka M15 kwa mfanyakazi ambaye mkataba wake unamwambia ni M40?
Nikamjibu sikia dogo una bahati sana umeshamaliza chuo, hilo swali ningekuletea kwenye zile test zangu za pale NAH nikuone ungejibuje. Nikamwambia haya nenda kawaambie watanzania wenzako haya uliyoyasikia na kuyaona. Akacheka na kuniambia Ticha bwaaaaana. Hahahaha.