Kwa kuirudisha CCM kwa wanaCCM tunakupongeza Rais wetu, wanaopingana nawe wanapingana na CCM ya wanaCCM.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Tumetoka kule tunaelekea kule sasa tupo njiani. Tukubali kwamba njia ya kutoka misri kwenda kanani kwa wana wa Israel ilijaa vikwazo, changamoto na kukata tamaa ila walisonga mbele bila kujali ili kuifikia nchi ile yenye wingi wa maziwa na asali, nchi ile ya raha na furaha. Safari ya Kanani ilianza, tupo njiani na tutafika hakika chini ya uongozi wa Joshua.

Joshua wa kuwapeleka watanzania Kanani ni Rais Magufuli. Watanzania wana Imani sana nawe Mhe.Rais na tunaamini kwamba wewe ni kusudi sahihi la Mungu kwa watanzania. Kuanzia upatikaji na upitishwaji wako ndani ya CCM mpaka kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu tuliamini wewe ndio Joshua wa kuwavusha watanzania. Ulishinda vita ambavyo Mungu alikupigania na kupigana upande wako nasi tutakuwa upande wako tukipigana nawe .

Wakati wa uchaguzi ule pesa pekee uliyotumia ni ile ya kuchukulia fomu tu, hukutoa rushwa wala hongo ya kununua wajumbe, hukuwa na wapambe wa kukupambania Zaidi ya Mungu pekee kuwa mpambe wako, hukuonesha kuwa na uchu na tamaa ya urais na ulichukua jukumu hili zito la kulivusha taifa letu. Hukuingia wala kuingizwa na kundi lolote na badala yake makundi yote hasimu yakaungana kwa ajili yako na Tanzania.

Uliingia madarakani katika namna ya kutotilia shaka uadilifu, uzalendo na uchapakazi wako. Hukuwa na kundi hivyo ukawa na nia ya kuondoa makundi ndani ya CCM, hukutoa pesa hivyo hukutaka wagombea waje kutoa pesa, ulionesha uwezo na uchapakazi hivyo huktaka wazembe wawe upande wako. Ukaanza kuunda na kutengeneza CCM mpya ambayo wagombea watachaguliwa kwa uwezo na uchapakazi na sio kwa makundi na pesa zao.

CCM mpya kimekuwa ni cha wanaCCM wote. Wote wenye uwezo wa kuongoza wanaweza kupata nafasi ndani ya CCM mpya bila kujali upo kundi Fulani au una pesa kiasi gani. CCM mpya haizungumzii makundi kama kipindi kile, CCM mpya imeondoa majina mengi ya walioonekana kutafuta vyeo kwa makundi au pesa na hili tumeliona kwenye chaguzi ndogo za marudio. CCM mpya inamuhakikishia kila mwanaCCM nafasi ya kushinda iliyo sawa na mwingine bila kujali mfuko wako unasomaje. CCM mpya inapendwa na wasomi wengi na wazee wetu wanasema CCM ya mwalimu imerudi.

Katika CCM hii ambayo kila mwanachama ana nafasi sawa na mwingine imeonekana kuwa ni changamoto na kikwazo kwa wengine waliokuwa wamezoea kula keki ya taifa chumbani. Wachache ambao wanaona CCM imekuwa ni kikwazo cha wao kufanikiwa kisiasa kwa sababu walizoea makundi na pesa, wachache ambao wanaona wanajukumu la kulisha wengine keki na si bwanaharusi wanaona CCM mpya ni kikwazo na wanataka kurudisha Misri kwa Farao. Sisi wanaCCM tunasema kwamba Misri haturudi na Rais Magufuli kama ilivyokuwa kwa Joshua atatupeleka Kanani.

Kitendo cha Mhe. Rais kuirudisha CCM kwa wanaCCM ni cha kupongeza sana na wanaCCM wamefurahi sana na wengi( wasomi) wamehamasika kujiunga kwenye siasa za CCM kwa sababu kwa sasa wanahakika ya kushinda bila kutegemea kundi wa la pesa ila uwezo wao. CCM mpya itatupatia viongozi bora ambao hawatokani na pesa wala makundi na kwa sasa pekee lililopo CCM linaitwa CCM.

Umekirudisha chama mikononi mwa wanaCCM nasi kama wanaCCM tunakuahidi kuwa tutapambana na yeyote kwa ajili yako kwa maslahi ya CCM na taifa letu. Hatutaruhusu CCM kuwa ya wachache na yeyote anayepambana nawe mwenyekiti kwa maslahi yake binafsi au ya kundi lake iwe ndani ya CCM au nje ya CCM, atapambana na wanaCCM.
 
Kaa kimya, unafikiri hatujui namna biashara ya madiwani na wabunge toka upinzani kuja CCM ilivyofanyika?
 
Kaa kimya, unafikiri hatujui namna biashara ya madiwani na wabunge toka upinzani kuja CCM ilivyofanyika?
unadhani kipindi kile cha makundi wangeshinda hao? Rais na Mwenyekiti wa CCM aliona kwamba wana uwezo hivyo walipojiunga wakapata nafasi sawa na wengine lakini wengine wakaona wawaachie kwa sababu wanaweza ndio maana wakapita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom