hazole1
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 4,319
- 3,911
Siku zote imekuwa ni kawaida mitandao ya kijamii kubadilishana habari na ninadhani utamaduni wa habari ndio upo hivyo kwa sababu hii dunia ni kubwa sana kwahiyo chombo kimoja cha habari tu hakiwezi kujikamilisha.
Na ninawashukuru sana uongozi wa JF ukileta hapa habari lazima waombe na chanzo cha hiyo habari. Kufungwa kwa JF wengi tulipata tabu sana kutafuta habari na kuangalia kila mtandao wanasemaje kuhusu JF.
Na tunashukuru vyombo vya habari vikubwa kwa mfano kama BBC, Mwananchi na kadhalika walikuwa wanatueleza kila hatua waliyofikia uongozi wa JF. Wakati JF imefungiwa nilidhani hao walionesha ukomavu wao katika tasnia ya habari na walijua hili swala ni la kupita tu. Na lazima waoneshe mshikamano wa habari.
Lakini cha kunishanga kuna blog kama Muungwana na Mpekuzi n.k. ambazo zina wasomaji wengi na nilikuwa naziamini kwa kupata habari lakini sijawahi kuona wameandika kuhusu habari ya kufungwa JF au kufunguliwa. Na hapa ndipo nilipokuja kugundua hawa jamaa wanafanya habari kibaguzi halafu wameonesha usaliti kwa umoja wa vyombo vya habari.