Kwa kuanzia iwe kwa wale wanaokunywa juice ya ngano

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Kwa kuwa Wakenya hawataki bidhaa za Tanzania ziuzwe kwao (japo ni hodari kwa kutaka soko huru EAC) basi nasi tuzigomee bidhaa zao KWA KUANZIA NA TUSKER. Na asitokee mtu kudai kuwa tusker ni ya Serengeti breweries hiyo ni ya Wakenya!
 
yap hawa jamaa tusipowaangalia vizuri watafyonza sana uchumi wetu, kwasasa wanatuuzia 16bilion wakati sisi tunawauzia 4bilion tu export sales
 
We utakua umetumwa na TBL,
na jua tu kwamba dhambi ya ubaguzi hua haiishi, mwisho utasema tugomee hata Magazeti ya Mwananchi au pengine hata Precision Air
 
TBL hawanifahamu kwa hiyo hawana namna ya kunituma. Huu ni mtazamo wangu binafsi (naamini Bujibuji & co mnaukubali maana zaidi ya kunituhumu kutumwa na TBL hamjakanusha hoja yangu)
 
Jamani, P air si ya shirima wa pale Rombo?! Au nimejidanganya!. Hata hivyo kimsingi naungamkono hoja.
We utakua umetumwa na TBL,na jua tu kwamba dhambi ya ubaguzi hua haiishi, mwisho utasema tugomee hata Magazeti ya Mwananchi au pengine hata Precision Air
 
Siungi mkono hoja, walete Bidhaa zao sisi watumiaji ndiyo tuamue aidha kununua bidhaa za nyumbani au za Kenya..
Binafsi ningefurahi kuona tunawashinda Wakenya kwa kupitia ushindani na siyo kwa kuwabania na kubebana..
Watanzania tuna tatizo moja, tuko too relaxed ndo maana tunaogopa ushindani (kuanzia Rais mpaka mtanzania wa kawaida)..
Tuboreshe bidhaa zetu ili ziweze kukubaliwa kwenye masoko ya nje siyo kulalama tu..
Binafsi ni mhanga wa Ubwetekaji wa Watanzania wenzangu na ninaamini wakija wakenya zaidi tutaamka (tusipoamka basi acha ile kwetu)..
 
Back
Top Bottom