Mtemi Mojo
Member
- Dec 17, 2017
- 39
- 44
Mwaka '78 Wakati mtukufu Rais J. K Nyerere anawatangazia waTanzania kuhusu uamuzi wa baraza lake kuingia vitani, kiwango cha uzalendo kati ya makundi yote ya jamii Ulikua ni wa kiwango kikubwa.
Wananchi walijitolea mali zao, fedha, Mifugo, na hata kujitolea maisha yao kwa ajili ya kumuondoa nduli Amin. Ukitazama taswira ya Kipindi kile ukalinganisha na sasa utabaki unaisikitikia nchi.
Ni kweli tunapaswa kupaza sauti zetu pale uhuru wetu unapowekwa hatarini, tunapaswa kudai haki zetu za msingi maana hakuna kamwe mipaka ya haki. Lakini ukiangalia kwa ndani, hii inayoitwa vita dhidi ya ukandamizaji wa haki tunaidai visivyo, na kamwe hatutashinda.
Yamekua yanatumika matusi ya nguoni dhidi ya yeyote anayekuwa na maoni tofauti. Yaani sometimes unajiuliza, kama hawa wanaodai haya wakipewa mamlaka si watawachoma moto wanaowapinga. Tunadai tunapambania uhuru wa maoni wakati tunawatukana wenye maoni tofauti na maoni yetu, this doesn't make sense.
Tumekua na Tabia nyingine ya hovyo ya kupinga hata miradi ya maendeleo. Yaani watanzania tunakua tunaombea tushindwe kwenye Mambo ya kitaifa ili tu waliopo madarakani waonekane wanashindwa. Angalia mifano hai kwenye issue ya kufufua Air Tanzania, issue ya makinikia, watu wanapinga hata ujenzi wa Bwawa la kufua Umeme. Tizama leo Zitto anapinga ujenzi wa flyovers dsm. Yaani ni sawa na kuiroga nchi yako. Unatamani nchi ifeli ili upate cha kuattack. Ni uchawi. Nchi zote hupingana pia, ila kwenye issues za nchi hushikamana.
Najiuliza, hivi ikitokea nchi inatuhitaji, watakuepo walio tayari kujitolea mali, fedha, Mifugo, na hata uhai kwa ajili ya Tanzania? Naamini wapo, TUPO,. tupo tunaoamini kuna vitu vitatu tu vya kuweza kutoa uhai wako kuvilinda, Mungu, Familia, Nchi. In that order. Ila najua kabisa wapo ambao watakua wanatusaliti. Wapo watakaokuwa wanatamani nchi ishindwe.
Mungu ibariki Tanzania.