mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Prof. Issa Shivji: Nilihudhuria birthday ya Mwalimu, sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha
"Nilihudhuria 70th (1992) birthday ya Mwalimu. Sikumbuki alipewa zawadi yoyote. Hata kukata keki alifanya kwa mzaha. Alipokuwa anaondoka, mama mmoja kampa portrait yake aliyechora mama huyo mwenyewe. Akamambia msaidizi wake apokee. Zawadi ya Benz kwa Mzee wetu ikanishtua kidogo." -- Issa...
www.jamiiforums.com
Wakati mwingine nadhani hata katiba mpya haitotusaidia sana, hii nchi wajinga ni wengi sana kiasi kwamba hata tukiandikiwa katiba kutoka mbinguni hatutoweza kusimama
Kinachohitajika ni mass education kwa umma huu ambao una utapiamlo wa maarifa
Elimu Elimu Elimu is what we need.
Nashawishika kusema tunahitaji kuwa makini na kauli & matendo katika kuchagua viongozi. Hawa watu wanatuita majina mengi tu wanyonge, mara hakuna hela kwa sababu ya Corona na mishahara haiwezi kupanda wakati ni takwa la kisheria. Kwa sheria hizo hizo kama viongozi tunapeana anasa & zawadi za kisheria etc
Hii kwetu kama mada ya kufikiria nchi yetu , hatuwezi kuwapa watu masikini nchi kuligana na nature za binadamu kwasasa. Ndio maana kwa kanuni hii wenzetu waliliona hili na kulifanyia kazi.
Kuwa mzalendo ni kuipenda nchi, sio lazima Serikali. Wakati mwingine Serikali hushikwa na kundi la waasi,wahuni au matapeli
Siku zote nitaendelea kuwaheshimu vijana wa kitanzania wanaoendelea kuikosoa serikali hadharani, pale inapotenda ndivyo sivyo. Pamoja na matukio ya kutisha yanayowakuta vijana/watu wanaoonesha upinzani, kama kutekwa, kupotezwa na kuuawa, lakini bado idadi ya wanaopinga maovu ya serikali...
www.jamiiforums.com
Kinachouma ni kuona walio wengi wanashindwa kujua kuwa kilichofanyika pale ni abuse of power na unjustifiable uses of taxpayer's money.
Elimu yetu ilivurugwa purposely ili kuwafanya watu washindwe kuwaza critically, haya ndio madhara yake sasa.
Huwezi kumpima kiongozi kwa kutaja jina Mungu kila wakati hakuna narudi hakuna , eti kiongozi kila wakati anataja vifungu vya bibles ndio nipate jiba kuwa huyu ndio kiongozi!! Ni ujinga narudi ni ujinga.
Tuna viongozi wengi walioweza kufanikiwa katika maisha hawa kwasasa tunapaswa kuwangeukia na kuwapa nchi. Mfano Mbowe..Kwa kiufupi sana Mbowe hana njaa na hajawahi kuwa na njaa
1980s Mbowe anasafirisha matunda nje ya nchi kwa Gulf Air.wakati wewe na babako mkipanda basi mnatapika.
1985, Freeman MBOWE ana boti la uvuvi, anaenda deep sea... sidhani kama DC Sabaya, yule mtangazaji mwenye kitambi clouds au Simalenga walikuwa wamezaliwa.hawa wanatumika tuu, Mbowe hayupo kwenye league yao
Kama haitoshi gari La mbowe La kwanza alipewa kibali na nyerere ili aingize nchini na ni BMW enzi hizo.
Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?
Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA? Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kumchagua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa...
www.jamiiforums.com
Hoja ya kupeana muda ni hoja mfu, siipendi na siikubali kamwe. Hakuna muda wa kupena wakati viongozi wakigawana zawadi na anasa nyingine za kisheria huku wavuja jasho wakiambiwa wasubirie stahiki zao za kisheria. Sasa wanasubiri nini haswa? Watumishi wa Umma wasubiri hadi lini? Hawa viongozi tuliokuwepo nao wana NJAA JAMANI HAKUNA KIONGOZI HAPA.
Mwaka 1967, Nyerere alikataa kutumia gari la Rolls Royce akidai kuwa lilikuwa ni anasa tupu. Akaenda mbali zaidi mpaka kwa Mlinzi wake, Peter Bwimbo, aliyekuwa anatumia Mercedes Benz 190 na kumshawishi aliuze ili ajenge nyumba yake huko Mara! Leo, Samia anagawa Benz! Ujinga! Japokuwa wakati huo kweli idadi ilikuwa ndio so siwezi kupiga lakini kwa wakati huu tunapaswa kubadili direction mapema.
I totally agree with you kwamba viongozi wanaojali maisha ya watu should walk the talk. Na hawa lazima wawe mfuko wana hela sio za kukopa ili upate uongozi ziwe inner money.
Hapo tunaweza kutoka katika maji haya.
mr mkiki.