Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 299
- 58
Baada ya kusoma hii habari kweli nimesisimka mwili kwa moyo huu nasema Hongera JK na wako wengi wenye matatizo ila ndiyo hivyo wako zaidi ya Sikonge .
2006-09-10 09:55:19
Na Mwandishi Maalum
Rais Jakaya Kikwete, ameahidi kusaidia kutafuta wafadhili wa kuwezesha upatikanaji wa mashine katika Idara ya Upasuaji Bandia katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais Kikwete ametoa ahadi hiyo baada ya kufurahishwa na namna madaktari wa hospitali hiyo walivyomtibu mtoto Bakari Hamis Katumbaku, mkazi wa Sikonge, mkoani Tabora.
Aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo, hususan Profesa Atef Amin na Dk. Laurean Rwanyuma kutokana na kufanikisha upasuaji kwa mtoto huyo na hivyo kumrejesha katika hali yake ya kawaida.
Rais Kikwete alisema kutokana na furaha yake hiyo na kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na madaktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili, anauagiza uongozi wa hospitali hiyo, kufanya utafiti wa kina wa gharama za baadhi ya mashine muhimu zinazohitajika katika Idara ya Upasuaji Bandia (Plastic Surgery).
Alisema yeye atawatafuta watu wenye mapenzi mema ili wagharamie mashine hizo.
Alitoa shukrani hizo na agizo hilo juzi jioni wakati akimkaribisha mtoto Bakari Ikulu kwa lengo la kumjulia hali na kuagana naye baada ya kukamilika kwa matibabu yake.
Mtoto huyo alifika Ikulu akifuatana na mama yake, Bi. Aziza Katumbaku, Daktari wake, Laurean Rwanyuma na Muuguzi, Bi. Ritha Kitama.
Profesa Atef Amin ambaye ni raia wa Misri hakuweza kufika kutokana na majukumu hospitalini hapo.
Rais alimuona mtoto Bakari akitembea vizuri bila dalili zozote za kujikunja au maumivu kama alivyomuona mara ya kwanza kule Sikonge.
Nashukuru sana, umepona kabisa? Daktari nashukuru sana. Nilipomuona mara ya kwanza Sikonge, hali yake ilikuwa mbaya, alikuwa akitembea kwa kuinama na akajitahidi kunikimbilia kama watoto wenzake lakini kwa taabu sana. Nikasema Mungu akijalia nitakusaida, Mungu mkubwa, nimefurahi sana, alisema.
Akitoa shukrani zake kwa Rais, mtoto Bakari ambaye alikumbatiana kwa furaha na Rais kama Baba na mwanae, alisema; nakushukuru sana, Rais, Mungu akujalie, sina cha kusema nakushukuru sana. Nimefurahi sana,
Naye Mama wa Bakari alisema Nakushukuru sana na kukupongeza kwa kutimiza ahadi yako, haikuwa rahisi kwangu kuamini pale nilipoletewa taarifa kwamba umeagiza tuje Muhimbili kwa matibabu. Sikutegemea kama mtoto wangu leo angeweza kutembea vizuri kama watoto wenzake, alisema.
Katika maelezo yake kwa Rais kuhusu upasuaji aliofanyiwa mtoto Bakari aliyeungua moto wakati akiwa na umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali yaliyomfanya ashindwe kutembea vizuri, alisema, Idara ya Upasuaji katika hospitali hiyo, haina mashine muhimu ambazo zingesaidia sana kuokoa maisha ya Watanzania wengi hususan wale wanaopata ajali za kuungua moto na kupoteza asilimia kubwa ya ngozi zao.
Dk. Rwanyuma alisema Idara hiyo ambayo hadi miaka ya hivi karibuni ilikuwa haina wataalamu wa upasuaji bandia, isipokuwa wale wa kutoka nchini Misri, inahitaji mashine zinazoweza kuotesha ngozi au kuitanua hususan pale mgonjwa anapokuwa amepoteza asilimia zaidi ya 80 ya ngozi yake.
Aidha, alisema pamoja na kupatikana kwa mashine hizo, pia mafunzo yanahitajika ili kuweza kupata wataalamu wengi zaidi katika idara hiyo.
Alisema hali hiyo itasaidia mno katika si tu kuokoa maisha ya Watanzania bali pia kurekebisha viungo.
SOURCE: Nipashe